Wednesday, September 24, 2008

Wabaguzi wachachamaa dhidi ya Obama!

Huko New Jersey, kikundi cha wabaguzi wenye siasa kali (white supremacists) wametoa na kusambaza maandiko dhidi ya anayegombea rais wa Marekani, Senator Barack Obama, ambaye ni mmarekani mweusi.

Flier hizo zina picha za Obama kama Osama bin Laden (photoshop), halafu inauzlia "Je, unataka Rais Mweusi?" Wanampakazia matope kwa kusema eti mweusi aliruhusiwa kuwa rais basi Marekani itageuzi maskini kama Haiti na Afrika Kusini. Inasema kuwa mtu mweusi ataharibu Marekani na haitakuwa nchi kama tunavyoijua.

Jamani, wadau tuwaombea usalama, Senator Obama na familia yake maana hawa wabaguzi wa hapa hawana mchezo.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.usatoday.com/news/politics/election2008/2008-09-23-anti-obama_N.htm

http://ap.google.com/article/ALeqM5j7UY5oKmggDTRdl48uQr5OPRboXwD93CLOV80

1 comment:

Anonymous said...

Hello America. With my recent plunge in the National Polls and this Economic Crisis that I am partially to blame for, I have decided to suspend my campaign and hide out in Washington for awhile until my advisors can figure out what they want me to do next! I have also decided that Barack Obama is way too smart for me to debate and doing so would be a no win situation for me so I am cancelling our debate. Apparently you have figured me out, therefore I have decided to run FROM President. See you all on November 4th. I am John McCain and I approved this message!