Tuesday, September 16, 2008

Bongoland II itaonyeshwa Uingereza


Kutoka: Kibira Films Blog:

BONGOLAND II INAKUJA EDINBURGH - UINGEREZA - MWEZI UJAO

Haya wadau wa Uingereza Bongoland II inakuja mwezi ujao wa Oktoba tarehe 30 saa mbili . Pata habari kamili hapa . Bongoland II imechaguliwa katika sinema za Kiafrika (Africa in Motion) ambazo zitaonyeshwa Uingereza kuanzia October 23 Mpaka November 2, 2008

Kama uko Edinburgh au mitaa ya karibu unaombwa ujitahidi kuwakilisha Tanzania na ujionee mwenyewe jinsi wasanii wa ki-Tanzania walivyotuwakilisha katika ngazi za kimataifa. Kuhudhuria kwako kutaonyesha waandalizi wa festival hii kuwa wadau na marafiki zao wana nia ya kutaka sinema za kwao zionyeshwe katika festival kama hizi.

Kama hutaweza kuudhuria siku hiyo, unaombwa kupitisha ujumbe huu kwa marafiki wote walio karibu na mji wa Edinburgh.

Kwa sasa sinema hii inapatikana katika DVD. Unaweza ukaagiza mtandaoni kwa kubofya hapa. Kumbuka kuwa wengi wetu kwa mara nyingi tuna-rent sinema kutoka Hollywood videos au Blockbusters. Tukumbuke kuwa ku-renti kwetu kunachangia katika kuendelea kutengeneza sinema nyingi za Kimarekani. Ni kwa sababu hiyo hiyo na sisi tujitahidi kuwaunga mkono wasanii wa Kibongo ili fani hii iendelee kukua ili utamaduni wetu nao uwakilishwe katika ngazi zaidi nje ya Bongo.

Kwa habari zaidi kuhusu sinema hii au sinema nyingine kutoka Kibira Films tafadhali bofya hapa.

SHUKRANI!!

1 comment:

Anonymous said...

Kwanza kabisa Edinburgh haiko Uingereza. Wa-skotish wenyewe wangekusikia unasema kuwa eti "Kapito site" yao iko Uingereza wangekuonyesha kilichomtoa Kanga manyoya.
Mdau wa Scotland hapa.

Ingawa ujumbe umefika na nitakwenda kuiangalia senema hiyo.