Friday, January 30, 2009

Republicans Wamchagua Mwenyekiti Mweusi!!!!


Naibu Gavana wa Maryland, Michael Steele, amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Chama cha taifa cha Republicans (Republican National Committee). Ni mwuesi wa kwanza katika historia ya chama hicho kuongoza chama.
Kama mnakumbuka walivyofanya mkutano mkuu wao mwezi Agosti, weusi walikuwa wachache mno huko, uliweza kuwahesabu kwenye mkono. Na weusi wengine waliokuwepo walidai kuwa walitukanwa matusi ya kibaguzi. Kipindi hicho vyombo vya habari vilihoji uhaba wa weusi katika chama cha Repbulicans na kuuliza kama Republicans ni chama cha wazungu tu.
Huenda Republicans wanadhania kuwa wakiwa na Mwenyekiti mweusi basi labda weusi watavutiwa kujiunga na chama hicho.
Lazima kuna watu hapa ambao hawana raha kutokana na kuchaguliwa kwake. Wazungu walikuwa na usemi, "A Black Man will be President when Hell Freezes Over" yaani mtu mweusi atakuwa rais kipindi motoni kunageuka barafu tupu. Basi huo barafu umeingia motoni. Obama ni rais na Steele ni mwenyekiti wa Republicans.
Lazima wabaguzi wa KKK wanalia.

*****************************************************************

Michael Steele Becomes First black RNC Chairman

WASHINGTON – The Republican National Committee has elected former Maryland Lt. Gov. Michael Steele the first black Republican National Committee chairman. Steele was the most moderate candidate in the field and was considered an outsider because he's not an RNC member. He beat back four challengers, including incumbent Mike Duncan, who was forced to withdraw from the field midway through the balloting in the face of a lack of support.


http://news.yahoo.com/s/ap/20090130/ap_on_el_ge/republicans

5 comments:

Anonymous said...

Too little, too late....

Chemi Che-Mponda said...

Prof. Matondo, umesema kweli. Republicans wameshajiharibia. Watu wanawaona kama chama cha kibaguzi. Pia ni chama cha manufaa ya matajiri. Ona Bush alivyotajirisha marafiki zake, huko watu wa kawaida wanzaidi kuwa maskini!

Anonymous said...

Huyu Steel ni miongoni mwa wale when a master is sick, they say "we're sick". Kuna mwenzake mwingine anaitwa Alan Keyes. Huyu Keyes alijaribu sana kumshambulia Obama kuwa hafai kuwa Rais kwa vile yeye siyo Decendent Of Slaves. Na wamarekani wengine weusi walitekwa na upuuzi wa Keyes. Huu ni udhaifu mkubwa sana wa watu weusi na ndo maana tunatawaliwa karne nenda, karne rudi. Tukipiga hatua kidogo tuu basi wazungu wataanza kututenganisha na watatumia wachache baadhi yetu na tutaingia mkenge.

South Afrika, mtendaji mkuu wa Apartheid alikuwa mpuuzi mmoja aliyeitwa Hendrik Verwoerd. Huyu wala hakuzaliwa South Afrika, alizaliwa Amsterdam, The Netherlands. Lakini alipogombania u-waziri mkuu wa South Afrika, hakuna hata mzungu mmoja aliyesema "hafai kwa sababu kazaliwa nje ya nchi". Wakamchagua na akawatekelezea sera zao vizuri sana.
tusubiri siku urais wa marekani utakapogombewa na m-nigeria, utauona upuuzi wa waafrika. Wataanza "oooh, tapeli, muuza ubuyu, n.k".

Wanzalambongo

Anonymous said...

Steele is an UNCLE TOM! Shame on him!

Anonymous said...

hehee sarah Pallin style wanaumwa kweli naona hawataki kummiza vichwa wafikirie au inaweza kuwa ni insult kwasababu hawaoni sababu kuwa na kiongozi mweusi Democracts na wao wawe na mweupe republican I just havent figured out nia yao ni nini