Saturday, January 17, 2009

Wabaguzi wachoma Moto Kanisa la Weusi

Wazungu wabaguzi watatu wamekamatwa huko Springfield, Massachusetts kwa kuchoma moto kanisa la weusi huko. Hao wabaguzi walisema kuwa walichoma moto kanisa hilo kwa vile walichukizwa na mtu mweusi kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani.

Mnaweza kusoma habari zaidi hapa:

http://www.boston.com/news/local/massachusetts/articles/2009/01/17/church_arson_tied_to_racism/

Na Obama anavyokaribia kuapishwa weusi Marekani wameonywa kuwa matendo ya kibaguzi dhidi yao yanaweza kuongezeka.

2 comments:

Mbele said...

Hivi ni vitendo viovu. Kwenye taarifa hii, suala ni ubaguzi wa rangi. Ni vitendo viovu, vya kulaaniwa. Lakini Waafrika wasisahau kuwa wengi wao nao ni wabaguzi, kwa misingi ya ukabila, dini na kadhalika, na wanafanya vitendo viovu sana kwa misingi hiyo. Tumeshuhudia hujuma hizi sehemu kama Rwanda, Burundi, Congo, Liberia, Sierra Leone, Nigeria, Kenya, Sudan, na Somalia. Kwa hivi, tunapojadili suala hili, tusizame katika kuwalaani hao wazungu tu, bali tuwalaani pia wale Waafrika nilioongelea, na kisha tujiulize kwa nini wanadamu wanafanya vitendo hivi? Niliwahi kutoa hoja hii katika kujibu suali moja kwenye mahojiano haya. Tuendelee kuelimishana.

Anonymous said...

UTawala Bora mashakani

Date::1/23/2009
Pinda ataka jino kwa jino
Na Victor Kinambile, Tabora

KATIKA hali ya isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana aliwaambia wananchi kuwa wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja vikongwe ni hawana budi kuuawa kwa kuwa wakisubiri mahakama kuwahukumu, watakuwa wanakosea.


Waziri Pinda, ambaye ameanza ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kuhamasisha vita dhidi ya mauaji ya vikongwe na albino, aliutaka Umoja wa Vijana wa CCM kuongoza vita hiyo, akisema lina jeshi zuri.


Mauaji ya albino yamekuwa ni tatizo kubwa nchini na hasa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.


Pamoja na serikali kutangaza hatua kadhaa za kupambana na wauaji hao, bado matukio ya kuuawa kwa watu hao wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa yakiendelea kuripotiwa, lakini Waziri Pinda ameenda mbali zaidi katika kukabiliana na tatizo hilo alipotaka wauaji hao wauawe badala ya kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.


Kauli ya Pinda, ambayo inaweka maswali katika suala la utawala bora, imekuja wakati ambao wananchi wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi na kuua vikongwe kutokana na imani za uchawi.


Akihutubia wakati wa kufungua mkutano wa 16 wa Shirikisho la Vyama vya Kuweka na Kukopa (SCCULT) kwenye ukumbi wa Chuo cha Utumishi Umma mkoani hapa, Waziri Pinda alisema iwapo wananchi wataendelea kuwahurumia wauaji hao ambao wanatafuta viungo vya albino wakitegemea mahakama itatenda haki huku nao wakiongeza kasi ya mauaji kwa Watanzania, watakuwa wanakosea.


Hivyo alisema kwamba kuanzia sasa mtu yeyote atakayemuona mtu amemkata shingo au mkono mweziwe basi naye auawe papo hapo hii itakuwa ndiyo dawa kwani vingozi wote tumechoka na mauji hayo.


"Mkimuona mtu akamkata mwingine shingo naye muueni kwani sasa viongozi wote tumechoka... no more, I can't tolerate anymore (imetosha, siwezi kuvumilia tena)," alisema Pinda huku akiwaacha watu midomo wazi.


Aliviomba vyama vya siasa kushirikiana na wananchi kuhakikisha suala hili la mauji linakwisha kwani wauji "tunaishi nao na ni rahisi kulimaliza iwapo tutakuwa kitu kimoja katika kuondoa kashifa hii ambayo imekuwa mbaya kwa nchi yetu".


Aliuagiza Umoja wa Vijana wa CCM kuhakikisha mauaji hayo yanatokomezwa kabisa, akisema kuwa ni jeshi zuri ambalo likiamua kutokomeza kabisa mauaji ya vikongwe na ndugu zetu maalbino inawezekana.


"Umoja wa vijana mna jeshi zuri ambalo naamini mkiamua mnaweza kutokomeza mauaji ya wazee wetu pmoja na ndugu zetu maalbno na kazi hiyo nawaagiza muanze leo msisubri auawe mwingine tena," alisema waziri mkuu.


Baada ya kumalizika kwa mkutano huo, baadhi ya watu wanaoonekana kuwa ni wa "serikali" waliwafuata baadhi ya waandishi wa habari, akisihi suala hilo lisiripotiwe magazetini kwa madai kuwa kauli hiyo ya Waziri Pinda inaweza kusababisha matatizo.


Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia amekuwa mstari wa mbele kupiga vita mauaji hayo, alitofautiana na Waziri Pinda katika moja ya hotuba zake aliposema kuwa adhabu ya kuua haitofautishi muuaji wa albino na muuaji mwingine na kwamba watakaopatikana na hatia ya kuua albino, atakabiliana na adhabu ya kifo kama ilivyo kwa muuaji mwingine.


Waziri Pinda alionekana kukerwa na mauaji ya albino wakati alipopata taarifa kwamba kuna mama mwingine aliuawa usiku wa kuamkia juzi.


"Nimeambiwa kuwa juzi wilayani Sengerema kuna mama mmoja ambaye ni mlemavu wa ngozi amekatwa mkono na wauaji wakaondoka na mkono huo na tayari mama huyo amekufa," alisema Pinda na kusisitiza kushughulikia wauaji hao.


Akitoa takwimu za mauaji ya vikongwe na malbino alisema mwaka 2003 waliuwawa vikongwe 517, mwaka 2004 waliuawa vikongwe 444, mwaka 2005 (494), 2006 (vikongwe 386), mwaka 2007 (vikongwe 526) na albino sita na mwaka 2008 (vikongwe 526 na albino 28).


Alisema tayari mwaka huu wameuawa albino watatu hivyo kufanya albino na vikongwe waliouawa kufikia kuwa jumla 2,900.


Waziri mkuu ameanza ziara ya siku nne kutembelea mikoa ya Shinyanga, Tabora na Mwanza ili kuhamasisha wananchi watokomeze vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu weye ulemavu wa ngozi.

Source: Gazeti La Mwananchi