Wednesday, April 29, 2009

Ghala La Silaha Lalipuka Mbagala, Dar es Salaam

BBC wanasema watu kadhaa wamekufa!

http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/8024656.stm


Kutoka MICHUZI BLOG:

BREKING NYUZZZZZZ: GHALA LA SILAHA LALIPUKA MBAGALA, DAR
GHALA LA SILAHA LA JESHI LIMELIPUKA NA KUSHIKA MOTO KWENYE KAMBI YA JESHI ILIYOKO MBAGALA KIZUIANI NA KUSABABISHA MILIPUKO MIKUBWA YA MABOMU NA KULETA KIZAAZAA JIJI ZIMA.

GLOBU YA JAMII ILIYO KATIKA ENEO LA TUKIO IMESHUHUDIA ASKARI WA JESHI LA ULINZIM POLISI NA ZIMAMOTO WAKIWA WAMEJAZANA NJIA PANDA KUELEKEA KAMBINI HUKO AMBAKO MOSHI MZITO NA MILIPUKO IMEKUWA IKISIKIKA TOKA ASUBUHI.

KUNA HABARI KWAMBA BAADHI YA MABOMU YANARUKA MAZIMA MAZIMA NA KUTUA KILOMETA KADHAA TOKA MBAGALA NA KULIPUKA. KATIKATI YA JIJI TAYARI WATU WAMETANGAZIWA WASHUKE MAGHOROFANI.

HABARI ZINASEMA KWAMBA MOTO HUO WA AINA YAKE UNAWEZA KUZIMIKA KWA UTAALAMU WA HALI YA JUU ILA USALAMA DHIDI YA MLIPUKO WA MABOMU NI MDOGO. WAKAZI WENGI WA MBAGALA WAMESHAONOLEWA SEHEMU HIYO WAKATI JUHUDI ZA KUTHIBITI MOTO NA MILIPUKO IKENDELEA.

GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUWA ENEO LA TUKIO NA INAAHIDI PICHA NA HABARI KEDEKEDE BAADAYE KIDOOOOO....

No comments: