Tuesday, April 07, 2009

Skandali ya Ngono kwenye Shule ya Oprah


Wasichana wanne wamefukuzwa kwenye shule ya fahari ya wasichana ya Oprah Winfrey huko Afrika Kusini. Wasichana watatu wamesimamishwa kwa muda. Kisa? Walikuwa wanafanya ushoga na kulazimisha wanafunzi wenzao kufanya vitendo vya kishoga!

Wasichana waliofukuzwa wamelia baada ya kunyanganywa simu za mikononi, nguo, viatu na vitu vingine walivyopewa shuleni.

Hiyo shule inaitwa Oprah Winfrey Leadership Academy. Wanafunzi wanasoma katika madarasa ya fahari kuliko hata vyuo vikuu vingi duniani, wanalala kwenye malazi yanayozidi five star hotel, na wanakula chakula kizuri kuliko unachoweza kununua kwenye restaurant. Hela aliyotumia Oprah kujenga hiyo shule ingetosha kujenga shule 10 nzuri sana Afrika Kusini.

Oprah mwenyewe anachagua wasichana wanaosoma pale na wengi wanatoka kwenye maisha ya dhiki.

Nawapa pole hao wasichana. Wameharibu wenyewe! Wenyewe wanaomba wasamehewa kwani bado wanakuwa na walitaka kufanya 'experimentation' (majaribio)!

Kwa habari zaidi someni:
7 comments:

Anonymous said...

Kwakweli huu usagaji na ushoga unaathiri sana teenagers. Wazazi tuna kazi kubwa mno.

Anonymous said...

Ufahari wote huo na watoto bado wanashikwa na ashki! Oprah amepoteza pesa kwenye hiyo shule. Anaelimisha wasichana wachache wakati anageweza kusomesha wengi zaidi kwa hela hiyo hiyo! Rich and stupid!

Anonymous said...

Huyo mzungu ndo kiongozi wao.

Maggie said...

Nakushangaa sana annony wa April 07,11:43 kwa hiyo comment yako. Hao watoto kufanya waliyoyafanya hayana uhusiano na ufahari wa Oprah au uanzishaji wake wa hiyo shule. Tunajua wazi kuwa shule nyingi za boarding za wasichana suala la usagaji lipo kabisa tena haswa kwenye shule zetu za kitanzania pia. Pili uamuzi wa kuanzisha hiyo shule ni mapenzi yake, ni hela yake na hakuna aliyemtuma kufanya hivyo zaidi ya roho yake.
Tatu, macelebrities wangapi wanafanya anayoyafanya Oprah, this woman gives millions of dollars to charities hapo hapo Marekani kama za orphans,mashule,organisations za watu binafsi,shelters za wanyama, AIDS research institutes etc more than any black woman we all know of. Wakazi wengi wa marekani walimpiga vita kama wewe kuwa kwanini afungue shule moja ya kifahari badala ya kufungua shule pale pale marekani, FYI akitaka anaweza kufungua shule hata ishirini katika kila state Marekani lakini huo si uamuzi wake. I believe pia ni uozo wa media za kimarekani kutaka kuwaharibia weusi wachache waliopiga hatua za juu Marekani. Kuweni waangalifu sana na propaganda za media za US za sasa otherwise mtakosa muelekeo na mtashidwa kuona kazi nzuri zinazofanywa na malaika wachache kama Oprah. Mimi naona bora alichokifanya Oprah kuliko baadhi ya wale macelebrities wanaoenda Africa kuaddopt watoto ili kujipatia sifa za kibinafsi badala ya kuwasaidia na basic needs wakiwa hapo nyumbani kwao, mnawajua sina haja ya kuwataja majina. God bless this woman, I think she has done enough on this earht!!

Anonymous said...

we unaesema oprah ni rich na stupid, Mungu akusaidie kwa kweli u dont know wat u saying.afrika wangapi wenye asili halisi ya kwetu afrika wamefanya hivyo? kwanza its a shame kwa afrika mtu toka marekani asomeshe watoto kwetu afrika wakat wapo matajiri sana lkn wanafadhili mambo yasiyo hata na maendeleo acheni mama tajiri afanye ambavyo moyo wake unamsukuma, waafrika wengi wamekalia awe tajiri ili aionekane na watu kama ufahari tu na kusaidia ndg zake tu. huyu aliejitolea Mungu amzidishie sana aendelee kufadili sehemu mbali mbali.

Anonymous said...

wanafrika kusini hawana shukurani. bora angejenga Bongo.

Anonymous said...

Duh tru kabisa Anonymous April 08, 9:42, tena ingekuwa vizuri ajenge Bukoba.