Monday, May 25, 2009

Hongera Mwanangu!


Wadau, ninapenda kuwajulisha kuwa mwanangu Camara Kadete, amepokea digrii (shahada) yake ya kwanza, Bachelor of Arts, kutoka McDaniel College, Westminister Maryland, juzi jumamosi. Baba yake ni mume wangu wa kwanza Prof. Henry Kadete (marehemu). Hongera sana!


Commencement 2009 McDaniel College


Proud Mama
Mimi na mwanangu Camara nje ya ukumbi.


Kushoto kwangu ni mchumba wa Camara, Bi Shalanda naye alipokea digrii Bachelor of Arts.

Tulimaliza kusherekea kwa keki, Camara na Shalanda wakizima mishumaa

28 comments:

Anonymous said...

ndio maana ulikuwa kimya? sasa bachelor of arts katika fani gani? jounalism? sociology? education? sports? or? tufafanulie?

otherwise kijana kaza buti, maisha ni magumu huku mitaani.

Faustine said...

Hongera Mama mtu kwa malezi mazuri pia.
Mdau
Faustine
http://drfaustine.blogspot.com/

Anonymous said...

eh!da chemi ushapata na mkwe tayari!hongera! ni mmarekani mweusi nini huyo?haya mama najua wamwangalia kama anafaa kwa mwanao, kila la kheri dada

MOSONGA RAPHAEL said...

Hongera sana Camara na Mama Camara. Nakumbuka ile picha ya utotoni uliyoiweka wakati anaanza masomo College.
Kila la heri

Unknown said...

hongera sana camara!!

chib said...

Hongera sana

Unknown said...

Hongera Mama, Hongera Mtoto.

Anonymous said...

kiswahili kigumu sana "mtoto wa mume wangu wa kwanza" tumejadili hatujapata jibu,ufafanuzi pliz

Anonymous said...

Hongera sana Da Chemi na Camara!!!!

Faith S Hilary said...

Aaaaw! I can't even imagine how proud you are!! Cnt w8 2 make ma parents proud as well..Congrats!

Yasinta Ngonyani said...

Hongereni sana!

Anonymous said...

Hongera sana Kamara. Hongera na pongezi kwako Da Chemi kwa malezi mema, maana bila malezi mema Kamara asingefika hapo alipo. Hongera pia kwa kupata mkwe. Mungu awajalie wafunge ndoa, wapate watoto wema na maisha marefu ya Amani na Upendo.

Anonymous said...

Hongera Mama,Mtoto na Inlaw

MWANAHARAKATI

Anonymous said...

Hongera sana Da'Chemi,Msisitizie camara afike mahali kama alipofika Baba yake,Da'Chemi itabidi nikutafute nikifika East Coast,nakukumbuka sana Dada kwani nilipokwenda shule Tabora Boys niliambiwa nikutafute pale Girls School kwani wote tulikuwa tunatoka Chuo Dar!nami wakati huo nilikuwa Mugya/njuka.

Chambi Chachage said...

Hongera mama na mwana - na mchumba!

Anonymous said...

Big Congrats!!!!!!

Simon Kitururu said...

Hongereni Wajameni!

Anonymous said...

mtoto wa mumeo wa kwanza, huyo mumeo wa kwanza alimzaa na nani huyo Camara.

kama atakuwa mtoto wa mumeo basi wewe utakuwa step mother.

la kama mlizaa nyinyi ndio wazazi basi hapa umemaanisha kuwa mtoto ni mali mwanaume. dah masikini mfumo dume.

big up camara kwa kadigrii katakuwa ka sport au education.

Chemi Che-Mponda said...

Kwa kufafanua, mimi ni mama yake mzazi Camara na baba yake ni marehemu Prof. Kadete. Niliolewa tena na wakati mwingine watu wanadhani huyo mume ndiye baba yake ndio maana nilisema hivyo.

Anonymous said...

Well wishes

Anonymous said...

Hongera kwako Da Chemi na kwa mwanao kwa mafanikio haya! Mungu amfanikishe zaidi na zaidi!

Anonymous said...

Hongera dada kuzaa si kazi kazi kulea - yaani degree na mchumba bahati sana

Anonymous said...

Hongera dada kuzaa si kazi kazi kulea - yaani degree na mchumba bahati sana. Hongera hongera hongera

Anonymous said...

Chemi,
Naomba nikupe Hongera kwa mafanikio ya mwanao Camara. Nilikuwa nafahamiana na mdogo wake Prof. ambaye alisoma Iyunga miaka ya 70 katikati kwani alikuwa rafiki wa karibu sana na marehemu kaka yangu. Natokea kijiji kimoja baada ya Tutuo kama unakwenda Sikonge na nilishawahi kwenda hadi nyumbani kwao Kadete na niliposoma kwa Michuzi jina Kadete, nikata zaidi kujua kama ni yeye au jina tu. Mpe hongera tena mdogo wetu na kama walivyoeleza wengine, basi tunaombea jina la Prof. Kadete lirudi. Kila la kheri. S. Sambali.

Anonymous said...

Ulituchanganya ulipoma mtoto WA MUME WAKO WA KWANZA. Sio mtaalamu sana wa kiswahili, ila nadhani ingeeleweka vyema kama ungeandika MTOTO WAKO KWA MUME WAKO WA KWANZA. hata hivyo asante kwa kurekebisha

Anonymous said...

Sichelei kusema una mwili wenye udongo mzuri na wale wanaokusimanga kila siku upungue huo ndio mwili wa mama wa kiafrika unavyotakiwa kuwa. Nilidhani umepishana na Jessica miaka miwili kumbe wewe ni zaidi! Hongera sana dada yangu Mungu akujalie wewe na watoto wako, wawe raia wema na uweze kuona wajukuu

Akili71 said...

"The apple doesn't fall far from the tree" kwa hiyo hongera sana kijana lakini pia hongera tele Mama.

mumyhery said...

Hongera mama na mwana