Tuesday, May 19, 2009

Rest in Peace Justin Cosby

UPDATE : 5.26.09

Mnaweza kupata taarifa zaidi hapa! Yaani tunashangaa kama hizi habari ni kweli. Yaani alikuwa haelekee kabisa! Na huyo ambaye wanadai walimwua ni Jabrai Jordan Copney, mtoto wa polisi mstaafu wa New York. Nadhani na hao mabinti wa Harvard hawasemi wanachojua!http://www.nydailynews.com/news/ny_crime/2009/05/22/2009-05-22_harlem_man_arrested_in_murder_in_harvard_university_dorm.html


(pichani Justin na mpenzi wake)


Wadau, nina habari ya kusikitisha. Kijana ambaye namfahamu tangu akiwa mdogo na rafiki wa mwanangu ameuawa katika bweni Harvard University. Navyosikia alikuwa anawakimbia hao waliomwua. Kwao ni karibu na napokaa mimi. Lazima niseme kuwa huyo kijana alikuwa mpole na hakuwa na matatizo niliyofahamu. Nimesikitishwa mno. Alikuwa anasoma Chuo Kikuu cha Salem State, lakini wanasema kwa sasa alikuwa hasomi pale. Tutasikia mambo yalivyokuwa. Yaani siwezi kuamini.

REST IN PEACE JUSTIN

***********************************************************

CAMBRIDGE, Mass. — A 21-year-old man shot inside a Harvard University dormitory Monday while students studied for finals died Tuesday.

Justin Cosby, of Cambridge, was shot in the abdomen late Monday afternoon while standing on a stairway leading to a common area inside the Kirkland House, an undergraduate dorm. He was found outside the building by police.

The dorm has an electronic security system, and Middlesex District Attorney Gerry Leone said authorities were looking into how Cosby got into the building.

Cosby's mother, Denise, said her son attended Salem State College. He lived a few blocks from the Harvard campus.

"It's just so strange. He was fine, healthy yesterday," Denise Cosby told The Boston Globe. "I just can't believe my son is not here today. Inside I'm just torn up, I feel like someone has murdered me."

No arrests had been made by Tuesday afternoon.
Harvard referred all questions to the district attorney. Leone said it appeared the shooting was isolated.

After the shooting, students were told to remain in the dorm for several hours as police interviewed potential witnesses.

Harvard police added security, mainly as a precaution, and students were allowed to move freely inside the dorm Tuesday.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.thecrimson.com/article.aspx?ref=528246

http://www.boston.com/news/local/breaking_news/2009/05/man_dies_after_1.html

8 comments:

Anonymous said...

Pole kwa msiba Da Chemi na familia husika!

EDWIN NDAKI (EDO) said...

POLENI SANA KWA MSIBA.MWENYEZI MUNGU IPUMZISHE MAHALA PEMA ROHO YA MAREHEMU.AMINA

Simon Kitururu said...

Poleni!

Unknown said...

Pole sana ndugu yangu, maisha yetu na njia panda siku zote

Anonymous said...

Poleni sana kwa masahibu hayo. Pamoja na hayo ninakaombi kadogo tu, umetamba kumfahamu sana kwani alikuwa rafiki wa mwanao sasa je hata ka picha hakuna halafu tuamini kweli ulikuwa ukimfahamu?
Naamini kwetu sisi ambao hatukumfahamu ka picha kake kangetupa mwanga. Who knows pengine nishawahi kukutanaye Salem lakini sikumfahamu kwa jina.

Anonymous said...

Asante kwa kutuwekea picha. Ni uungwana tu kukiri kuwa ulipitiwa kutoweka picha, badala ya kuweka picha na kutokiri kuwa umekumbushwa.

Anonymous said...

Poleni.

Jamaa aliuliwa kwa sababu jamaa walitaka kumpola hela zake za kuuza madawa ya kulevya kwa wanafunzi wa Havard. Habari ni kuwa jamaa mmoja amekwisha kamatwa.

Chemi Che-Mponda said...

Siko Boston kwa sasa lakini na mimi nimesikia juu juu kuhusu hiyo habari ya madawa ya kulevya. Kama ni kweli ni habari ya kusikitisha mno. Sidhani kama mama yake alikuwa na habari.
Mimi sikujua kama walimnasa. Alikuwa akiniona ananisalimia kwa hashima zote, yaani hakuelea kabisa kuwa yuko hivyo. Duniani kuna mambo. Na ni kweli Cambridge kuna biashara nzuri ya kuuza madawa kwa wanafunzi wa Harvard na MIT. Inasikitisha mno.