Tuesday, July 14, 2009

Apostle Vernon Fernandes atakuwa Texas

Nninapenda kuwajulisha watanzania na watu wote kutoka mataifa mbali mbali kwamba watumishi wa Mungu APOSTLE VERNON NA MKE WAKE PASTOR ANN kutoka nyumbani Tanzania watakuwa na semina kubwa ya Neno la Mungu katika jiji letu la DALLAS- TEXAS kuanzia tarehe 21-23 mwezi wa nane. Tunategemea kuwa na wageni kutoka sehemu mbali mbali za hapa Marekani, Uingereza pamoja na Canada.

Huu ni mkutano wa kwanza wa aina yake kuandaliwa na watu kutoka mataifa mbali mbali kwa ajili ya watumishi kutoka Tanzania.Kwa tangazo hili tunaomba watu wote kutoka nje ya Dallas wawasiliane nasi kwa mipango ya malazi na usafiri kutoka Airport. Mwisho, kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wetu,Dada Rose Mhando hatutaweza kuwa nae. Kwa maelezo zaidi juu ya semina naomba usome kwa makini hiyo flier ambayo itakupa mwanga zaidi.

Pastor Abisalom Nasuwa
Kwa niaba ya kamati ya maandalizi

Kwa maelezo zaidi wasiliana na hawa wafuatao;
Pastor Absalom Nasuwa-Umoja Church
Pastor Nosa- Arise and Shine Church
Pastoe Amen-DaySpring Church
Pastor Emmie-DaySpring Church
Evangelist Julius-All Nations Church
Evangelist Neema Akyoo-Maranatha Ministry

2 comments:

Baba Sangara said...

Dear dada Chemi,
Nakufurahia kwamba unamtangazia huyu jamaa "apostle Vernon Fernandez".... This is not one than Charles Taylors "trusted advisor", Dr Paul... Tafuta footage yeyote ya Charles Taylor 2003 kwenye youtube umgundue mwenyewe... ni tapeliwa hali ya juu
samahani kwa ujumbe huu... Huyu nyoka anajificha Tanzania sasa hivi kwa jina jingine... you are free to discard my message, mimi ni mdau anayeishi Abidjan, Cote d'Ivoire

Baba Sangara said...

Dada Chemi,
Jitazamia mwenyewe...

http://www.youtube.com/watch?v=6e6JB0cxJaA