Wednesday, July 29, 2009

Rest in Peace DJ Eddy Sally (Adam S. Mwambile)

Adam akiigiza kama Dr. Moshi (Maangamizi the Ancient One)

Nimepokea habari za kusikitisha. DJ Eddy Sally aka. Adam S. Mwambile, alifariki dunia leo asubuhi huko Dar es Salaam.

Kaka Adam alikuwa mmoja wa wale maDJ wa mwanzo Dar. Pia, Adam aliigiza kama Dr. Moshi katika sinema, Maangamizi the Ancient One. Nakumbuka tulivyokuwa kambi Bagamoyo College wakati wakushuti sinema Aprili 1994. Alikuja na mke wake MZambia. Adam alikuwa mcheshi kweli na alichangamsha kweli kambi.

Natafuta picha yake nibandike hapa. Lakini kama mmeona sinema Maangamizi yeye ndiye aliigiza kama daktari mkuu wa hospitali na aliwapa madkatari wengine shida sana.

REST IN ETERNAL PEACE!

**********************************************************
Kutoka Michuzi Blog:

DJ EDDY SALLY, DJ MASHUHURI NCHINI, AMEFARIKI DUNIA LEO ASUBUHI KATIKA HOSPITALI YA MKOMBOZI JIJINI DAR AMBAKO ALILAZWA KWA MATIBABU TOKA JANA.

HABARI KUTOKA MSIBANI AMBAKO NI NYUMBANI KWA MAREHEMU SINZA KUMEKUCHA HAPA JIJINI ZINASEMA MAZISHI YATAFANYIKA KESHO KIJIJINI KWAO KISARAWE.

HAYATI DJ EDDY SALLY ATAKUMBUKWA KUWA MIONGONI MWA MA-DJ WA MWANZO KABISA NCHINI, AKIWA AMEANZIA DISCO LA SEA VIEW KABLA YA KUHAMIA LUSAKA, ZAMBIA, ALIKOTOKEA KUWA DJ WA KWANZA MMATUMBI NCHINI HUMO.

MIAKA YA 80 ALIREJEA NCHINI NA KUANZISHA LIBENEKE LA 'EM THREE DISCOTHEQUE' KWENYE UKUMBI WA KEYS HOTEL AKIWA NA DJ SWEET FRANCIS AMBAO KWA PAMOJA WALITETEMESHA JIJI KWA VIFAA VYA KISASA NA SOUND SYSTEM ILIYOKUWA BORA KULIKO ZOTE ENZI HIZO

1 comment:

Anonymous said...

Rest in Peace. Alikuwa DJ kwenye arusi ya ndugu yangu Dar mwaka 1995Ilifana kweli.