Saturday, July 04, 2009

Tembo Washinda Bindamu katika Mashindano ya Kula 'Hot Dog'
Jana huko Coney Island, New York kulikuwa na mashindano ya aina yake. Binadamu walishindana na tembo katika kula mahot dog. Hapa Marekani, Hot dog ni aina ya sausegi ambao inapendwa sana. Hot inawekwa ndani ya mkati maalum (bun) uliopasuliwa, na inapakwa mustard, tomato, vitunguu, sauerkraut (kabichi), chili, na vitu vingine chaguo lako.

Katika dakika sita, tembo watatu walikuwa hot dog 505, wakati binadamu walikula 143 tu. Tembo waliweza kula na matunda pia katika kipindi hicho.

Duh! Yaani mtu wa kawaida sana sana anaambulia mbili. Hao bindamu walikuwa na matumbo ya ajabu!


Kwa habari zaidi someni:

1 comment:

Anonymous said...

Haikuwa mashindano. Walijua tembo watashinda!