Thursday, July 30, 2009

Morgan Freeman Kumwoa Mjukuu Wake! Haki ya Mungu!!!!


Duh! Yaani hii habari inafanya damu ichemke kwa hasira. Mcheza sinema maarufu, Morgan Freeman (72) yuko mbioni kumwoa mjukuu wake, E'Dena Hines (27)! Ingawa si mjukuu wa damu, huyo binti bado ni mjukuu wake! Ni mjukuu wa mke wake wa kwanza.
Habari zinasema alianza kutembea na huyo binti tangu ana miaka kumi na sita na ndo chanzo cha yeye na mke wake wa miaka mingi, Myrna kuachana. Habari ni chafu sana kuhusu huyo Morgan Freeman. Jinsi mke wake alivyogundua anatembea na mjukuu, alivyokuwa anatembea na wanawake wengi. Na kuna habari kuwa ilikuwa ndoto ya huyo mjukuu kuwa mke wa Morgan Freeman na sasa inakamilika!

Mnaweza kusoma zaidi hapa:

13 comments:

Anonymous said...

TOBA!

Nautiakasi said...

Acha unaa huo Da Chemi..! Mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzio! Mie sioni hatari wala nini, madhali si mjukuu wake wadamu tatizo lipo wapi? Age ain't nothing but a number...!Aliimba marehemu Aliyah, na waswahili wanasema ng'ombe hazeeki maini, wacha mzee akale raha kwa dogo dogo!Tunaishi mara moja tu dunia hii!
Ujumbe: "Wanaume ni kama panya kila siku hutafuta shimo jipya..."

TVZ Kicartoon said...

ndo yale yale ya kwetu....
babu anamwita mjukuu wake mchumba! au mke wangu! na bibi nae akazia mke mwenzangu!
huyo kwa sheria anaruhusiwa kumwoa lakini kibinadamu tu tunaona kinyaa!

TVZ Kicartoon said...

Kuota mvi si utu uzima,
Kung'oka meno si utu uzima,
Bora MASHINE iwe nzimaa!!

Bora MASHINE iwe nzimaa!!
Bora MASHINE iwe nzimaa!!
Bora MASHINE iwe nzimaa!!

Anonymous said...

It's a disgrace to God.

Anonymous said...

Mnaosema umri hauna shida nawashangaa sana, siku hizi maadili na mipaka ya ndoa imepotoshwa na sisi sisi binadamu, Morgan akizeeka kupita kiasi huyo binti atatafuta atakae mtimizia, sasa hivi anaona kapata kwa sababu ya pesa za Morgan, keshokutwa huyo huyo binti anataka divorce ya mamilioni ya pesa mzee anazeeka na kufilisiwa kwa aibu, kumbe akijipatia wake wanaoendana labda angezeeka kwa amani, ndoa za hollywood ni pesa hakuna true love, maana ya ndoa imepotea!!

Anonymous said...

Morgan kuoa mwanamke wa miaka 27 sio kitu. Lakini yeye kutembea na hicho kibinti tangu kina miaka 16 tena wakati bado yupo na mkewe? Hiyo noma.

Anonymous said...

Pumbavu kabisa Nautiakasi! samahani lakini

Nautiakasi said...

Anon july 31, 5:31AM,
Kwakuwa umeshindwa kujiheshimu na mimi wacha niendelee kukuvunjia heshima...!
Pumbavu mamiyo alie kubali kufunguwa miguu kwa tahira (babiyo), akaishia kukuzaa wewe mwanaharamu mkubwa wee..!

Anonymous said...

Goddam! Mjukuu tena. Ingawa si mjukuu wa damu alilelea kama mjukuu. Kwa kweli ni aibu.

Anonymous said...

This is a disgrace to GOD, siku hizi watu hawamuogopi hata Mungu kisa wana pesa na kwa sababu ya tamaa za miili yao, hata kama alikuwa mjukuu wa mkewe is he really serious? huyo si kama mjukuu wake tu, viungo vya mwanadamu vinamfanya mpaka ubongo wake usifanye kazi inavyotakiwa, raha za ngono hakuna lolote, inawezekana kampenda lakini ni mapenzi yaliyobarikiwa na Shetani wala si Mungu ndio maana anajionea sawa, very sad!!! Kulala na binti mdogo hivyo tena wakati bado alikuwa ameoa, uchafu mtupu!

Jibs said...

Sidhani kama kuna ubaya kama kama wao wamekubaliana, sie waafrika tuna mila nyingi za ajabu na za kushangaza na hazijaleta maendeleo katika jamii, na bila kuangalia undani wake tumekuwa wazuri kukosoa ya watu wakati yetu yamejaa tele, Eti usifanye lile au hili utalaaniwa na wazazi hiyo hadithi iliishia wapi, wakati tumekuwa na kuona wazazi wetu hasa mababa wakifanya upuuzi je ni nani alikuwa anawalaani, au ndio failure ya mtoto ni lawama kwa mzazi bado.
Morgani ameshangaza lakini sie ni nani wa kumhukumu.

Gio Ve said...

Mipaka ya nchi yako ni inavyoonekana katika http://pillandia.blogspot.com