Tuesday, July 07, 2009

Historia ya Toilet Paper

Wadau, hapa Marekani watu hawawezi kuishi bila toilet paper. Na nasema hivyo kwa sababu mwaka 1999, watu walienda dukani na kuzoa toilet paper zote kwa sababu kulikuwa na uzushi kuwa mwaka 2000 toilet paper itakuwa adimu. Haikutokea.

Ukienda dukani hapa unakuta kila aina ya toilet paper na hata rangi tofauti. Unakuta karatasi laini, nzito, enye losheni, ngumu, enye vipande viwili (2 ply) nk. Ni hela yako tu.

Sehemu nyingi za dunia bado wanafanya 'usafi' kwa kutumia maji. Lakini wakianza kutumia vyoo vya 'kizungu' vya kukalia wanaanza kujifunza kutumia toilet paper.

Hata nilipokuwa Tanzania nakumbuka karibu kila sehemu toilet paper ilikuwa inapatikana. Lakini enzi za Mwalimu na kabla watu walikuwa wamezoea 'kopo'. Na wengine walikuwa wanatumia vipande vya magezeti kuchambia. Na hebu jiulize hapo zamani za kale kabla ya vyoo vya kizungu watu walikuwa wanatumia nini? Hata hapa Marekani walikuwa na vyoo bya shimo, na walikuwa wanachambia vipande vya magazeti, mabunzi, majani nk. Sema, watu wamesahau au hawataki kufikiria kugusa huko mahala na vitu wanavyoona vya ajabu.

Mnaweza kusoma historia ya Toilet Paper hapa:

http://www.cnn.com/2009/LIVING/wayoflife/07/07/mf.toilet.paper.history/index.html

4 comments:

Anonymous said...

Wakati Warumi (Roman Empire)wanatawala Uingereza walianzisha matumizi ya vyoo, vyoo vyao vilikuwa ni mfereji uliotengenezwa sehemu ya kukalia na kulikuwa na chombo mfano wa mtungi wenye maji katikati, juu ya mtungi huo kulihifadhiwa mti uliokuwa na mfano wa sponge, mti huo ulitumiwa na kila aliyejisaidia kusafisha zile sehemu na ukimaliza unautumbukiza kwenye mtungi (kuusuza) ili mwingine autumie, ukifikiria sasa hivi utaona ni kinyaa sana lakini kwa wakati huo ulikuwa ni ustaarabu.

Anonymous said...

Niko marekani lakini bado naendeleza kutawaza na maji....haya mambo ya toilet paper ni uchafu mtupu...toilet paper haiwezi kutoa harufu ya mavi ukilinganisha anayetumia maji kutawazia anakuwa msafi zaidi.

Anonymous said...

Nipe toilet paper! Ukitumia toilet paper hushiki uchafu. Ingekuwa vizuri kwa wanaotumia kopo watumie sabuni na kuhahikisha wananawa mikono na sabuni baada ya kumaliza shughuli. Hiyo kopo ni rinse job tu. Kuwa msafi kabisa ni laazima kuoga hata ukitumia maji au TP!

P, Umangani said...

Toilet paper ni uchafu tu, sasa unaogopa kushika nyaa then unatembea nao matakoni, maana hata ufute vipi na tissue, hayaishi zaidi ya kusambaa katika mfereji wa nya. Ndo maana watu wametengeneza pipe special za kuchambia, siku hizi hata vyoo vya uswazi wanaweka pipe, unapiga maji kwenye sehemu then unaosha, mtu unakuwa swafi!