Monday, July 20, 2009

Mdau Richard Magumba Amaliza Kozi ya Filamu


Habari za siku nyingi ndugu zangu...

Samahani kwa ukimya.. ninawaandikia kuwajulisha yakuwa mwezi wa tatu mwaka huu nilipata nafasi ya kwenda Nairobi kushiriki training iliyoandaliwa na watu wa M-Net training iliyoshirikisha waandishi wa script kutoka A-Mashariki, tulijifunza njia mbalimbali za uandikaji wa script kwa ajili ya michezo ya kuigiza (TV Series) Binafsi nilijifunza mambo mengi sana.

Ninachukua fursa hii kuwashukuru na kuwaomba muendelee kuweka habari na taarifa mbalimbali zinazohusu mafunzo katika blog zenu. Nilipata taarifa za mafunzo hayo kupitia blog zenu, asanteni sana na endeleeni kufanya vivyo hivyo.

Ninawatakia kila la kheri na yote mema katika utendaji wa kazi zenu.
Richard.

NB: Ambatanishwa ni picha ya washiriki, mimi nimeketi chini, mtu wa pili kutoka kushoto.

1 comment:

Anonymous said...

bila shaka mdau richard nimekuona na pia nimekutambua vizuri maana umetabasamu sana....
alex kidende