Wednesday, January 27, 2010

Bibi Titi Alivyotutembelea Mwaka 1965


Wadau, nilivyokuwa Tanzania mwaka jana, nilichukua hii picha kutoka nyumbani. Ni wazazi wangu Dr. Aleck & Rita Che-Mponda na marehemu Bibi Titi Mohamed. Naona alikuwa kwenye ziara Marekani. Picha ilipigwa Washington D.C., wakati huo baba alikuwa Mtangazaji wa Voice of America Swahili Service na pia mwanafunzi Howard University. Picha naona ilipigwa 1965, baba anamhoji kwa ajili ya kipindi chake. Nakumbuka kulikuwa na picha Bibi Titi amenipakata lakini sikuiona. Nikiipata mbona nitafurahi mno.

13 comments:

Anonymous said...

Hii ni kumbukumbu nzuri sana. Unafanana sana na wazazi wako Chemi.

Mzee wa Changamoto said...

Taswira / Picha ni kitu chema saana. Imagine sasa hivi ukiiangalia hiyo picha ama wazazi wakiiona wanakumbuka mangapi? Pengine hata watoto an wajukuu wa Bibi Titi nao wakiiona wanapata mengi ambayo hakuna ambaye angeweza kuyaeleza.
Hongera kwa wazazi kwa kutunza kumbukumbu namna hii
Blessings

Anonymous said...

Wamama wa zamani walikua wanapendeza sana, That's totally awesome

Kaka Trio said...

Nice memory and nice photo too

Anonymous said...

mama yako alikuwa bomba kinoma.

Anonymous said...

Mzee kumbe alikuwa mrefu zamani au ni picha?

Anonymous said...

Dah! Bibi TITI alivyokubeba akakuambukiza mwili! maana naona wazazi wote englishi figa!
(samahani lakini najua tuko kwenye msiba lakini kutabasamu kidogo rukhsa kupunguza mawazo)

Chemi Che-Mponda said...

Wewe Anony wa 2:58pm, I never thought of that! LOL!

Anyway, maskini ya Mungu nilikutana na Bibi Titi kwenye mwaka 1990 nikiwa Daily News. Aliniomba sana nitafute hizo picha na nimpatie copy, lakini bahati mbaya sikuziona. Ndo juzi kwenye search ya picha za marehemu Rev. nikaona hii.

Baba Sangara said...

You have your beautiful face from your mother!

Anonymous said...

Miaka hiyo alipokuwa m-Bunge wa Dres Salaam, Mama Titi, mbali na umahiri wa lugha ya Kiingereza, hakusiota kuipiganuia magomeni wawekewe taa mabarabarani:

Alisimama akadai, "We want fire in the bottles in Magomeni..."

Wa-Bunge wenzxake wakacheka ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Nyerere, ambaye baadaye alisimama na kuzidi kutetea hoja hiyo kwamba ni lazima Magomeni wawekewe taa za barabarani!

Kwa Mama Titi electric bulbs ni moto ndani ya chupa. What a metaphor....si umeme unawaka ndani ya chupa (bulbs)!


BAP

Chemi Che-Mponda said...

Mimi nilisikia alisema, "We want fire in Magomeni...Fire in Small bottles." Ni kweli ukitcheki vizuri ni moto ndani ya vichupa.

Na ndo baada ya hapo Mwalimu alisema kuwa watumie Kiswahili Bungeni.

zitto kiaratu said...

cha maana hapa at least bibi titi kapata mtaa wenye jina lake dsm!!! alipigania uhuru wetu lakini baadae nyerere alimsingizia kutaka kupindua sirikali yake, ukitazama nyerere alikuwa waziri mkuu, walivunja katiba ya kidemokrasi ili awe rais bila upinzani kama alivyofanya mugabe, kaunda alitumia formula hiyo pia na kumtia ndani simon kapwepwe, obote alijaribu matokeo yake akatokea jamaa anaeitwa idd amin dada ,the rest is history, jamani viongozi wengine walikuwa wajinga, kenyatta, moi wote wamepitia njia hiyo, AFRIKA NAKUPENDA SANA!!!!

mgeni said...

DU! picha nzuri hii . wakati Baba yako anatangaza VOA na kusoma ,baba yangu alikuwa bado anacheza kombelela temeke. NICE MEMORY