Wednesday, December 15, 2010

Mifugo Wodini MwaiselaWadau, nilikuwa pale Mwaisela Ward namba 8, majuzi ghafla nikasikia watu wanapiga kelele kwenye wodi ya vitanda vitano (viko vitanda tisa). Halafu nikasikia wagonjwa wakisema kuwa kuna mifugo wodini. Kumbe walimwua panya!
Watu walienda kuangalia ni nini? Mgonjwa huyo alisema aliwua kwa kumpiga na kiatu. Manesi walisema kweli panaya wapo wanapanda kwenye mabomba ya vyoo.

Pichani ni mgonjwa aliyemwua huyo panya akienda kumtupa kwenye takataka za Biohazard.

3 comments:

Anonymous said...

Hii Kali! Sehemu nyingine wangemgeuza huyo panya buku kitoweo.

Simon Kitururu said...

Naamini ingekuwa Marekani PETA wangemyanyasa huyo mgonjwa kwa kuua panya.:-(

zitto kiaratu said...

hospitali ya taifa? HAYO NDIO MAENDELEO YA 49 YA UHURU, panya mpaka kwa wagonjwa, kuna walalahoi wanaishi buguruni au chamwino lakini hawaishi pamoja na panya, walalahoi wakitaka kuandamana na kupigania haki zao wanapigwa mabomu ya tindikali na fungu fanta uone, Ahsante zangu kwa baba mtakatifu nyerere kwa dhuluma za kial siku, itafika siku tuu!!!!