Friday, December 31, 2010

Heri ya Mwaka Mpya 2011

Nawatakia wadau wote Heri ya Mwaka Mpya!
Kwa heri Mwaka 2010! Karibu Mwaka 2o11!

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

nawe pia dadangu!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Asante na kila la heri nawe Da Chemi. Mapya na mazuri zaidi kwa mwaka huu. Pamoja daima!!!

Anonymous said...

LEO ndiyo siku ya mwisho. Jumatano ya mwisho gazeti hili kutoka likiwa na makala za porojo zangu za Jumatano maana ndiyo Jumatano ya mwisho ya mwaka 2010 maana Mwaka 2010 imebidi uondoke na kuupisha mwaka 2011. Acha uende. Uende kabisa maana mwaka 2010 niliupenda mwanzoni, lakini mwishoni hasa baada ya mchakato wa Uchaguzi Mkuu kukamilika na hata chaguzi nyingine zilizofuatia zikiwamo za taasisi mbalimbali kama Bunge, nimeuchukia mwaka 2010 na sitaki kuuona tena, wala kuusikia.

Kwa huruma tu, ninaupa hadi Ijumaa uwe umeondoka; nisiouone tena kwenye macho yangu wala kuusikia masikioni kwangu; acha uende. Acha uende maana lazima mbegu ife ili mazao yapatikane.

Mwaka 2010 tulioupokea kwa shangwe nderemo na kila aina ya ushangiliaji, unaondoka huku ukiwaacha wengine wakiwa na tabasamu nyusoni na vicheko midomoni mwao.

SIMON KITURURU said...

Heri ya MWAKA MPYA kwako pia Dada CHEMI!