Friday, December 10, 2010

Muhimbili Wanahitaji Fluoroscopy X-Ray Machine

Ofisi ya X-Ray Fluoroscopy huko Muhimbili National Hospital

Wadau, nimehangaika na baba yangu hapa Muhimbili siku kadhaa sasa ili afanyiwe Cystourethrography. Bado hajafanyikiwa, mashine inaharibika kila saa. Kuna backlog ya wagonjwa wanaohitaji kufayiwa x-ray na hiyo mashine lakini haijawezekana.

Jana ilikuwa sikukuu hivyo walikuwa wamefunga. Ile juzi tulimtoa baba wodini Mwaisela na kumpeleka kwenye X-ray. Kakaa masaa kadhaa ndo wakasema mashine imeharibika na fundi anitengeneza.

Alitokea Acting Head wa Idara, Dr. Flora Lwakatare, alisema kuwa wana mashine mbili za fluoroscopy. Moja ndo mbovu kabisa na nyingine ndo hiyo inayoleta matatizo mara kwa mara. Alisema wametarifu Waziri kuhusu tatizo lao lakini bado hawajapata mashine mpya.

Haya leo, tumemtoa baba wodini kumpeleka huko kwenye x-ray. Mashine ikaleta matatizo. hivi sasa wanasema fundi anakuja kutengeneza. Isipowekezekana leo basi mapaka juamatatu. Tunaomba mungu kuwa watafanikwa kutengeneza mshine na itaweza kufanya kazi.

Na si zaidi ya saa moja iliyopita, babu ambaye alitolewa wodi nyingine kwa ajili ya vipimo alizimia (fainting) na kuanguka hadi kwenye sakafu! Nesi aliyemsindikiza baba yangu kamhudumia yule mzee mara moja. Wamerudisha wodini. Inasikitisha kweli kuona wagonjwa wamelundikana pale x-ray.

Kwa kweli huduma hapa Muhimbili umekuwa mzuri, ila ndo tumekwama kwenye hiyo x-ray. Je, serikali inampano wa kuleta mashine hiyo, maana wagonjwa wanateseka.

9 comments:

Anonymous said...

Chemi, the problem of equipment in the third world is overwhelming. This is distressing to patients and frustrating to relatives and even health care workers. Governments either do not have the priority or ability to meet these challenges. However some charities can help specifically if they are approached with specific need and request. Try aid to hospitals worldwide.
Regards
Mimi

Anonymous said...

DaChemi bora mzee angechunguzwa alipokuwa huku, Muhimbili sio kabisa wanasema ukitakuwahi paradiso hapo ndio mwake, poleni sana Mungu atampitisha

Anonymous said...

Pole Sister,My advise is to fly mzee to India.Qatar and Emirates fly daily.or fly him to Nairobi Agakhan Hospital and see the difference.I am talking from my experience.Wish your dad fast recovery.

kiona mbali said...

serikali ya ccm haina mpango wowote wa kuweka mashine mpya;kwani wao viongozi wa ccm hawaendi hapo muhimbili..wanaenda nje kutibiwa na wanapeleka familia zao ktk hospitali binafsi kwa kuwa wana pesa za rushwa...wananchi kama wanataka kubadili hali hiyo ni kutoichagua ccm ktk chaguzi zijazo.Kwani haingii akilini serikali inayoweza kununua mashangingi zaidi ya 300 hadi 400 kila miaka mitano ishindwe kununua mashine moja ya x-ray.Hapo ndio utaona priorities zao.

Anonymous said...

Kwanza kabisa pole sana na usumbufu huo na tunamwombea mzee wako Mungu amrejeshee afya yake. Hayo ndiyo maisha bora kwa kila Mtanzania - miaka 50 ya uhuru. Huwa ninasoma blog yako mara kwa mara na wewe ni mmojawapo ya walio mstari wa mbele kuipongeza serikali ya CCM. Afadhali hapo Muhimbili wana mashine zilizoharibika - kule vijijini huduma inayotegemewa sana ni ya waganga wa kienyeji. Nina uhakika mashine zitatengenezwa pengine wakubwa walikuwa bize na kumtunuku Mhe Rais Dr. JK shahada ya kutambua mchango wake mkubwa katika kuboresha huduma za afya nchini!!!!!!!

Anonymous said...

Da Chemi, poleni na hekaheka hiyo ya kuuguza. Kuna changamoto nyingi sana bado zinaikabili nchi yetu. Pengine changamoto kubwa kabisa inayokwamisha utatuzi wa changomoto nyinginezo, ya afya ikiwemo, ni politicization ya kila kitu. Tumeweka siasa mbele katika kila jambo ... matokeo yake professionalism haina nafasi ... Lakini tunamtakia Mzee apone mapema. Hiyo ndiyo hospitali ya Taifa ... sijui kule kwetu Kasulu Kigoma watu wenye matatizo ya afya mambo yanakuwaje ... ee Mola tuepushe.

Kithuku said...

Chemi kwanza pole kwa kuuguza, namuombea babako apone haraka. La pili, kwa nini unaruhusu babako alazwe Muhimbili hiyo ambayo hata wenye nchi wanaikimbia kwa jinsi inavyotisha kwa huduma mbaya! Wewe unaishi US na unafanya kazi ya maana yenye hela nzuri, unashindwa nini kumtibia babako majuu? Hebu fanya haraka ondoka naye kabla hayajawa mengine!

Innocent said...

Hi Chemi,
Pole sana kwa kuuguza,those are some of 3rd world problems. It's normal, there is nothing under Public can be efficient and effective. Nenda Nairobi Hospital, you will be surprised why are we saying that Muhimbili is the state of the art while it's not yet there.

Baraka Mfunguo said...

Inasikitisha sana lakini ndio hali halisi. Inabidi watu wapaze sauti zao hadi ngoma za masikio yao zipasuke ndipo watakapojua umuhimu wa maisha ya watu. Hiyo ni Muhimbili hospitali kubwa ya rufaa. Mikoani, Wilayani hali ikoje?

Hakuna ama utaratibu wa Planned Preventive Maintanance upo lakini kwenye makaratasi tu. Watu wakienda kwenye hayo mafunzo wanaenda kuuza sura na kula posho kiufupi hakuna mtu ambaye ana moyo na kazi siku hizi kila mtu anavuta kwake. Utaenda hospitali utaambiwa kipimo hiki hakipo lakini nenda sehemu fulani kumbe mhusika ana hisa ndio mambo ya Tanzania.

Daktari, Mtu wa Maabara(Radiology, Microbiology/Immunology etc),Wauguzi na wahudumu wa afya hawana umuhimu hata tukiwaona mabarabarani umuhimu wao unaonekana ukiwa na tatizo. Hata posho zao sio za kuridhisha.

Ocean Road nako wana mashine yao ya mionzi iliharibika kwa kipinndi kirefu na ikawalazimu wagonjwa kusubiri mpaka mtambo upone. Je maisha ya binadamu yanaweza kuwa Compromised? Ni wangapi wanamudu gharama za hospitali binafsi achilia mbali kuchangia gharama?

Kwa kuhitimisha mimi nimeona matatizo haya Mosi hakuna uwajibikaji ama utendaji wa kuridhisha kwa watendaji wakuu wa serikali pili vifaa hivyo vinatumika na kuzidi vile inavyotakiwa kutokana na uwingi wa wagonjwa Tatu hakuna mipango mahsusi ya kutengeneza mitambo hiyo(PPM) ama imekaliwa tu nne watendaji wengi sasa hivi wanathamini pesa kuliko utu- Maadili ya kazi yameshuka tano urasimu serikalini unakwamisha mambo mengi. Hali ya urasimu ipo mpaka leo na ndio maana hata hao wafanyakazi wanakuwa frustrated kwa sababu tatizo likitokea wao wanakuwa kafara wakati wao walishafuatilia ngazi husika.

POLE KWA PROF NA APATE AFYA NJEMA