Sunday, December 05, 2010

Safarini Tanzania

Hi Wadau Wapendwa,

Niko Dar es Salaam, Tanzania. Nilifunga safari haraka haraka kuja. Baba yangu mzazi, Dr. Aleck Che-Mponda amelazwa Muhimbili, Mwaisela Room 309. Yuko pale zaidi ya wiki mbili sasa akisumbuliwa na maradhi kadhaa ikiwemo Prostate.

Dar ni joto sana sasa hivi. Pia kuna vumbi sana hasa sehemu ambazo hakuna barabara ya lami. Foleni kwenda mjini and kurudi ni balaa.

Mengine baadaye.

4 comments:

Mkongwe said...

Mola amjaalie nafuu na kupona kabisa. Mpe ugua pole Dr. Chemponda.

Anonymous said...

Miaka michache uliyoondoka ndio umeshaisahau Tanzania

Joseph said...

Karibu nyumbani, mpe Pole sana Mungu atamponya na kumpa afya njema.

Anonymous said...

we ulitegemea nini? ndo kusema umepashau kwenu? huku ni vumbi,joto, maisha magumu na kila kitu kama vp si umebe huyo baba yako ukamtibie huko utokakao kuliko kutubeza hapa kila mtu ajue shida zetu kwenda zako huko na usisahau mkataa kwao mtumwa