Wednesday, February 16, 2011

Mabomu Dar!

Habari nilizopata nikuwa Julius Nyerere International Airport imefungwa!

Watu watano wamekufa na 4o wameumia. Wanasema idadi itaongezeka.

Kuna bomu ilielekea Ubungo/Magomeni/Kigogo.

Wananchi wameelekezwa waende Uwanja wa Taifa kulala leo. Barabara ya kwenda uwanja wa ndege, Nyerere Road (Pugu Road) Imejaa watu.

Simu hazipatani. Najribu kuwapigia watu pamoja na wazazi wangu Tenki Bovu Dar siwapati.

3 comments:

Anonymous said...

Ni hatari sana. Mabomu yamelipuka kuanzia saa tatu kasorobo mpaka saa hizi saa tano kasorobo ndiyo yametulia. Watu wengi wanaoishi huku G'mboto wamekimbia kwenda maeneo ya Buguruni kwa ndugu zao.

Anonymous said...

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote. Nchi ayngu Tanzania jina lako ni tamu sana.............!

Anonymous said...

Hizo kambi nyingi za jeshi zilijengwa wakati jiji la Dar likiwa bado ni dogo. Jiji linaendelea kukua na sasa hizo kambi zimeingia katikati ya mji kabisa. Wapiga plana wa jeshi na jiji nadhani walikuwa na ukiwa wa ya miaka mitano tu badala ya hamsini. Kusema kweli tumechelewa kuligundua tatizo hili na sasa muda umefika kambi hizi zihamishiwe mbali na jiji na penginepo kule ziliko kama zinazungukwa na makazi ambayo mengi hayana mpangilio. Kando ya hivyo basi hizo silaha nzito zisihifadhike kabisa katika hizo kambi za mjini. Uhamisho wa hizo kambi utaleta kazi, utasaidia kusambaza uchumi na huduma kwa wananchi waishio huko vijijini ambako kambi zitahamishiwa, na mwisho utayaweka matatizo haya kulala.