Saturday, February 19, 2011

Picha na Video za Maafa ya Mabomu Dar

Hivi jamani, jeshi inafanya nini kuondoa hayo mabomu yaliyoanguka uraiani? Kuna mengine ambayo hakulipuka, si wananchi wako hatarini? Kuna uwezekano mkubwa kuwa watoto wataende kuyachezea halafu yakalipuka na kuwaua.

************************************************************
Picha kwa hisani ya Bongo5.com na email:

Kombora iliyoanguka kwenye shamba la mchicha

Kombora lililowekewa uzio wa usalama na jeshi la polisi
Wananchi bado wakiwa katika hali ya mshtuko siku baada ya mlipuko wa Mabomu katika kambi ya jeshi Gongo la mboto
Nyumba iliyoathirika na mabomu yaliyolipuka

Picha Kutoka Pugu Secondary School

Mnaweza kuona picha na video zaidi kwa KUBOFYA HAPA:

4 comments:

Bart said...

Jana wale wataalam wa jeshi walielezea sana. Kitu kimojawapo walichoeleza ni kuwa si Tanzania pekee yake ambapo kuna kambi za jeshi na silaha za milipuko maeneo ya makazi ya watu, na hiyo ni kweli. Tumeona nchi mbalimbali Duniani ambapo kambi za jeshi na maghala yao (japo hatujui yana ninin) zipo mijini.

Tatizo hapa siyo tu maghala ya silaha za kivita kuwa maeneo ya mijini bali ni kulipuka kwa silaha bila ya mpangilio. Silaha hizo hazistahili kulipuka bila ya kulipuliwa. Hilo ndiyo tatizo kubwa. Hawa wanajeshi ni binadamu, nao wanastahili kuwa salama. Hata kama maghala na kambi zao zikiondolewa mjini lakini huko zitakakopelekwa, mabomu au silaha nyingine zikaendelea kulipuka bila mpangilio, zitawaua askari wenyewe, familia zao, na kupoteza pesa nyingi za umma. Jambo la kujiuliza zaidi, ni je, jeshi letu lina uwezo wa kuzitambua silaha zilizofikia viwango vya usalama, kuzitumia, kuzihifadhi, kuzikagua, na kuzuia madhara yanayoweza kutokea kutokana na silaha za milipuko? Wana miundombinu sahihi ya kuhifadhia?

Makamanda wale waliozungumza na waandishi wa habari, japo hawakutaka kuilaumu serikali, kitu ambacho najua jeshi haliwezi kuthubutu kutokana na nidhamu yao kwa amiri jeshi Mkuu, lakini maelezo yao yalionesha wazi kabisa kuwa hawana bajeti ya kutosha ya kutengeneza miundombinu inayostahili na iliyo salama kwaajili ya kuhifadhi silaha za milipuko. Sasa cha kujiuliza ni kuwa inapokuja suala la uamuzi uchague, kati ya kujenga barabara mpya au kujenga maghala salama ya kuhifadhia silaha, kipaumbele chetu inakuwa ni nini? Kwangu mimi ningeona aheri niendeshe gari kwenye barabara yenye vumbi lakini watanzania wote angalao tuendelee kuwa hai. Kama mlifuatilia maelezo ya makamanda ile jana, utagundua kuwa baada ya maafa ya Mbagala, mapendekezo yalitolewa lakini utekelezaji wake haukuwa timilifu kwa vile hakukuwa na hela ya kutosha kutekeleza kila jambo. Kwa maelezo ya Brigedia Jenerali Paul Meela, 'Baada ya tukio la Mbagala kulikuwa na mapendekezo mengi. Tulijitahidi kuyafanyia kazi, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa baadhi ya makombora lakini huwezi kumaliza kazi hiyo mara moja maana hata huko unakoyapeleka kunahitaji kuandaliwa, na bajeti yetu kama mnavyojua, haitoshelezi. Njia nyingine ni hiyo ya kuhifadhi silaha chini ya ardhi, tuna baadhi ya maghala yetu chini ya ardhi lakini gharama ya kutengeneza ni kubwa, na bajeti yetu kama mjuavyo ni kidogo.'

Swali muhimu hapa ni kujiuliza kama tuna uhakika wa kuishi na silaha za hatari na tukawa salama. Kama hatuna uwezo wa kuyatunza, ipi ni busara zaidi, kuwa na yale tu ambayo tuna uwezo wa kuyatunza au kuwa nayo mengi ambayo tunafahamu wakati wowote yanaweza kulipuka na kuua raia wetu, askari wetu na kuzidi kupoteza fedha ya umma bila ya kuyatumia? Mimi binafsi lawama zangu zaidi zipo kwa serikali kuliko jeshi letu. Nina imani jeshi lingependa sana silaha hizi zihifadhiwe vizuri ili na wao pamoja na familia zao, wakati wote wawe salama, lakini ili hilo litimie ni serikali ndiyo inayotakiwa kugharamia ujenzi wa maghala na mafunzo kwa askari wetu. Kama serikali inaweza kupata fedha za kununua silaha, kwa nini washindwe kutoa pesa kwaajili ya kujenga miundombinu sahihi ya kuhifadhia?

Bart

Anonymous said...

KUZUIA MAAFA NA MAJANGA:
Inategemewa kamati hizi kuhakikisha kuwa zinashauri na kuhimiza kutekelezwa kwa USHAURI na MAPENDEKEZO yao ili kuzuia maafa kutotokea. Hii ina maana kuwa kamati hizi hazisubiri tukio kutokea ndipo wahamasishe misaada ya kibinadamu; la! Jukumu lao ni kufuatilia taarifa za vyombo vingine kuhusu uwezekano wa kutokea maafa na kushauri serikali na wananchi kufanyia kazi. Mathalan; ni jukumu lao kufuatilia taarifa za Mamlaka ya hali ya hewa na endapo iko tahadhari ya kimbunga, mafuriko, ukame, nk wao (kamati za maafa ) huwa na jukumu la kuhimiza serikali na vyombo vyake pamoja na wananchi kuchukua hatua za kupunguza athari za maafa. Mfano: Kuhama mabondeni, kulima mazao yanayovumilia ukame, kuweka chakula cha akiba, kuzuia wavuvi kwenda baharini, nk.
Kukagua na kuona maeneo gani ni hatari kwa maisha ya watu na mali zao: Mfano kuzuia uendelezaji wa makazi karibu na kambi za jeshi, kuzuia ujenzi wa vituo vya mafuta ktk makazi ya watu, nk.

2. KUPUNGUZA ATHARI ZA MAAFA NA MAJANGA PINDI YANAPOTOKEA.
Yako majanga na maafa yatokanayo na shughuli za binadamu (milipuko ya mabomu, ajali za vyombo vya usafiri, vita, nk) na mengine ni ya kiasili (mafuriko, ukame, kimbunga, tetemeko la ardhi, nzige, nk). Jukumu la kamati za maafa katika hili ni kuhakikisha na kuhimiza kuwepo kwa mikakati ya makusudi na vyombo vilivyowekwa tayari ili kuhakikisha kuwa majanga yanapotokea hayaleti athari kubwa sana kwa watu na mali zao au miundo mbinu iliyopo. Hii ina maana kuwa kila wakati tunakuwa na timu za uokozi zilizo tayari na zenye vifaa (timu huhusisha madaktari, wauguzi, zima na vikosi vingine vya jeshi, vyombo vya habari, raia waliofundishwa) njia za dharula,akiba ya vifaa vya dharula, maeneo yalitambuliwa kuwa ni salama pindi kukitokea hatari.

Kwa kujiweka tayari hivi endapo kunatokea janga lolote lile timu hizi za uokozi huingia kazini mara moja (maana ziko tayari na zina vifaa vyote).WANANCHI walio karibu na eneo la hatari hupewa taarifa kupitia VYOMBO VYA HABARI. Taarifa itakayotolewa kwao huwa fupi yenye MAELEKEZO YA NINI WAFANYE, WAPI WAENDE, NA WAENDEJE.
Nikichukulia tukio la jana kama mfano: Mlipuko umetokea kwenye ghala la kwanza. Jeshi (kiongozi wa kambi y Gongolamboto) linatoa taarifa (na isiwe lazima kuzunguka hadi tumpate msemaji wa jeshi) kupitia vyombo vya habari na hata vipaza sauti au vingora vya tahadhari. Taarifa yake INATOA TAHADHARI KWA WANANCHI KUHAMA HARAKA na ITAELEKEZA WAENDE UELEKEO UPI UNAOONEKANA KUWA NI SALAMA. Vyombo vya usafiri viko tayari kubeba wananchi na kuwapeleka eneo salama na wenye usafiri wao wanaelekea huko. Barabara zote muhimu za kuingia na kutoka eneo la hatari zina askari wa usalama wa barabarani wa ziada ili kurahisisha usafiri (tunajua foleni za miji yetu). Timu ya madaktari ziko tayari katika hospitali zote za jirani zikiwa na vifaa na timu nyingine ya huduma ya kwanza iko eneo la kupokelea watu. Kuna magari ya kubeba wagonjwa wenye vifaa katika eneo la tukio ili kubeba majeruhi.

Kwa kuzingatia hayo ni dhahiri tukio limetokea lakini idadi ya watu watakaopoteza maisha au kujeruhiwa itapungua. Jana wananchi walikuwa wanaambiwa waondoke eneo la jirani na jeshi; Yako maswali ya kujiuliza: WAENDE UELEKEO UPI ULIO SALAMA? WAENDEJE? (Maana si wote wenye usafiri). Hakukuwa na chombo cha habari kilichobeba tukio hili kwa uzito wakati huo wa usiku (je, yule ambaye alikuwa katikati ya jiji au mbali na G'mboto na familia yake iko huko angewezaji kujizuia kwenda nyumbani?). Mwananchi anaambiwa akimbie je, usalama wa nyumba na mali zake uko wapi? Je, akikimbia vibaka wakaiba nani atamlipa gharama hiyo?

Mwisho niseme na wanaoamini katika Mungu; wakati huu tunapowaombea walijeruhiwa wapone na waliofiwa wapate faraja. Tuendelee kuomba REHEMA ZA MUNGU kwa ajili ya Taifa hili. Maana "Tanzania ya leo TUNAMUHITAJI MUNGU kuliko WAKATI MWINGINE WOWOTE". Fuatilia vyombo vya habari; HAKUNA TAARIFA YA TUKIO LA KUTIA TUMAINI.

Anonymous said...

Kwa mara nyingine milipuko ya mabomu iliyotokea Gongo la Mboto
imeingiza jeshi la Tanzania kwenye taasisi zenye ombwe la kiungozi.
Kwa taarifa za chini ya kapeti za mama moja aliyempoteza mume wake
inaonyesha Jeshi lilikuwa na taarifa za hatari ya ulipukaji wa mabomu hayo siku tatu or more before.

Yasemekana bomu la kwanza lilipuka mida kati ya saa nne na tano
asubuhi masaa ya afrika mashariki. Mama huyu anasema alikuwa pamoja na
mumuwe nyumbani muda huo na anasema walikuwa wanabishana kwamba ni radi ama sio radi.

Na ilipofika mida ya saa saba waliona magari ya jeshi na yale
yanayomilikiwa na wanajeshi binafsi yakipita huku yakiwa yamebeba wanajeshi na wanafamilia wao.Pia inasemekana baadhi ya wanajeshi waliwapa marafiki zao wa karibu ya kambi habari hiyo lakini kwa siri na jamaa hao waliondoka kwa siri.

Mama huyu ameendelea kulonga kuwa ilipofika mida ya saa mbili za usiku mlio mwingine kama ule wa saa za asubuhi ukiwa umelia na kishindo kikali kikafuata ndipo mumuwe akasema huu ni mlio kama wa asubuhi walio kuwa wanabishana huku mama akiiendelea kudhania ni radi, mumuwe alitoka nje na mlipuko wa pili uliofuata ndio uliondoka na mumewe aliyekuwa kesha toka nje ilikuthibitisha yanayojiri.

Mpaka sasa hivi kuna watoto zaidi ya 1000 amabao bado hawajatwaliwa na wazazi wao katika makambi ya dharula sabasabana kwa watu binafsi, pia kuna wazazi zaidi ya 160 wanaowatafuta watoto wao- katika hili inaonyesha watu wal ioripotiwa kufa ni changa la macho yaani idadi ni ndogo ukilinganisha na sintofahamu iliyopo. Pia kuna mnyetishaji anasema siku baaada ya tukio muhimbili walianza kukataa maiti za watu waliotokea katika mlipuko ili kuweza kudhibiti idadi ya watu waliokufa watakaoripotiwa. Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani serikali yetu ipo tayari kupotosha habri hata pasipokuwa na sababu ili tu kuonyesha dhahama hii ilikuwa ni ajali ndogo kama ilivyosemwa na mkwere.

Itakumbukwa jeshi jana lilimwambia Hamad Rashid Mbunge wa wawi(CUF)
kuwa kulifanyika ukaguzi wa mabomu hayo siku tatu kabla. Je hii
inamaanisha hatuna wajuzi makini wa kuhifadhi mabomu hayo? Kwanini
hawakusense dalili za hatari? Pia ikumbukwe hakuna mwanajeshi wala
mwanafamilia aliyejeruhiwa wala kufa, hii inaonyesha taarifa za
kijeshi zilikuwepo za uwezekano wa kutokea maafa hayo ndio maana
waliondoka na kwenda eneo salama bila kuwapa raia waishio maeneo ya
karibu hatari itakayofuata.

Anonymous said...

Kuna swali moja limejiuliza lakini sijapata jibu: hivi ni kwanini matukio haya yanatokea Tanzania tu? Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti na ninasikiliza sana redio na kuangalia TV, lakini sijawahi kusikia makombora yaliyohifadhiwa katika kambi ya jeshi yakilipuka yenyewe Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi au hata Somalia. Hapa kwetu mabomu na makombora yamelipuka si mara moja, bali mara mbili katika kipindi kisichozidi miaka miwili na kuua na kujeruhi watu wengi na kusababisha uharibifu mkubwa. Hii sio bahati mbaya. Hapa lazima kuna kitu kitakuwa kimefichwa, lakini watawala wetu hawana budi kuelewa kuwa Watanzania wa sasa si wale wa miaka iliyopita. Ukweli lazima utajulikana pamoja na kwamba mambo mengi ya kijeshi huendeshwa kwa siri. Mwaka 2009 ilikuwa ni Mbagala, mwaka huu ni Gongo la Mboto. Matukio kama haya yatatokea wapi tena jijini Dar es Salaam? Mwenge? Lugalo? Kigamboni? Temeke (kambi ya Twalipo)?