Thursday, June 06, 2013

Khadija Kopa Yu Hoi Kwa Majonzi - Msiba wa Mume Wake Jaffari Ally

Yaani namwonea huruma Dada Khadija, alikuwa safarini hakupata nafasi ya kumwaga mume wake,  mume wake amefariki ghafla yaani. Mimi mwenyewe kama mjane mara mbili ninaelewa uchungu wake. Sasa hebu cheki hiyo picha ya chini. Huyo jamaa anayecheka anastahili kuzabwa kibao!  Hata haya hana!

Picha hizi ni kwa Hisani ya Ofisi wa Makamu wa Rais


 Mkuu wa mkoa Rukwa Eng. Stella Manyanya kushoto akimfariji msanii na taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija omar Kopa alipokua kwenye chumba maalum cha kupumzikia wageni kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leoa alfajiri kutokana na ugonjwa. Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais).


Picha juu na chini ni Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kupanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar kopa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf.


Siku ya Harusi ya Dada Khadija Kopa na Jaffari Ally Mwaka 2008 (picha za harusi kwa hisani ya Michuzi Blog)

*****************************************
Kutoka Tanzania Daima

Mume wa Khadija Kopa afariki


\na Andrew Chale, Bagamoyo

DIWANI wa Kata ya Magomeni mjini hapa, ambaye alikuwa mume wa Malkia Mipasho nchini, Khadija Kopa, Jaffar Ali Yusuf amefaiki usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Tanzania Daima mjini hapa jana, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, alisema msiba huo umepokelewa kwa masikitiko makubwa.

“Msiba tumeupokea kwa masikitiko makubwa na shughuli za mazishi zinaendelea, ambapo marehemu anatarajiwa kuzikwa, kesho...” alisema Kipozi.

Baadhi ya watu wa karibu wa marehemu, walibainisha kuwa alikuwa akiumwa muda mrefu bila kutaja ugonjwa uliokuwa ukimsibu.

Kwa upande wake, Katibu wa Tanzania One Theater (TOT), Gasper Tumaini, alithibitisha kupokea msiba huo na kubainisha kuwa malaria kali ndiyo iliyosababisha kifo hicho.

Marehemu alinyakua kiti hicho cha udiwani wa Magomeni miezi michache iliyopita baada ya diwani wa awali aliyekuwa anaongoza kata hiyo, Abdalah Mshindo kufariki mwaka jana.


8 comments:

Anonymous said...

R.I.P Diwani Jaffar

Poleni kwa watu wote walioguswa na msiba huu.

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un

Anonymous said...

Rest in Peace Jaffar. Ila ndugu wanaposema mgonjwa kaugua kwa muda mrefu kama mleta mada alivyosema kwani wanashindwa nini kuutaja huo ugonjwa wa muda mrefu. Tunapotoa general and undefined statements zinasababisha maswali mengi sana kwa wasomaji wa habari. Pole sana mama Hadija kwa kufiwa na mume wako uliyempenda sana. Mlipendana hadharani bila kujali binadamu maana hatuna dogo. Hivi msanii Lulu alipotuhumiwa (sijui kama ni kweli maana sikuona hata picha moja wakiwa na Komba) kuwa anatembea au ni mpenzi wa mheshimiwa huyu ni kwa nini hamsemi? Mwanamke akimzidi mwanaume basi utasikia mara mama yake mara bibi yake mara vile. Hivi wale wanaoa wanawake zaidi ya mmoja nipeni umri range wa mke mdogo!!!! Wengine ni sawa na watoto wao na hawasemwi!!! Kabla hatujakosoa basi tuangalie pande zote za shilingi.

Anonymous said...

Kufiwa ni kitu kigum sana na katu hakitozoeleka kamwe .........
hamna haja ya kukufuru sana zaidi kumuombea marehemu mema
huko aendako!

Anonymous said...

Du kweli asiye na Bahati habahatishi! kihisroria alikuwa akiolewa ndoa haidumu kwamadai kwamba walikuwa hawaendani kifupi walikuwa wakimzingua nae anawazingua akapata waliepatana nae anafariki tena bila hata kuacha mtoto naye MASIKINI KIJANA WA WATU!!behind death is something wrong!tupeni sababu za kifo chake isiwe rahisirahisi iviivi.Wadau tujue ili tuchangie kwa kina .Too young to DIE!

Maria said...

Mama khadija nakuhurumia kwa jinsi mlivokua mmeshibana na mumeo, na jinsi ulivokua ukimrusha hewani kila wimbo. Mume anauma, sisi wenye waume tunajua. Uchungu wa mume hakuna mfanowe, pole mama!

Anonymous said...

Aliekuwepo kabla nae alifariki,na pengo lake likazibwa na mme wa khadija koppa nae kafariki,who is next then?

"bagamoyo hii hatutaki upinzania kabisa hasa chadema haitakiwi hapa"by riz1 kupitia gazeti la jamhuri.

RIP BROTHER

Anonymous said...

inna lillahi wa inna ilayhi rajiun, Muumba amrehemu. Tuliyebakia nyuma tujiandae kwa kuwa nasi tutatamkiwa mfu muda wowote na kwenda kuoanana na Aliyekuumba.

Bruce said...

Mungu amlaze mahali pema peponi mume wa Khadija Kopa.

Jamani alizi ya dar inamaliza watu

Usije mjini! Utakufa!