Friday, July 27, 2007

Picha zaidi za Bongoland II Film Shoot Dar es Salaam

Cameraman and Cinematographer Sam Fischer, akifanya vitu vyake mitaani Dar es Salaam.
Moja wa Interns kutoka kampuni ya Sofia Records akirekodi somo kuhusu film editing kwenye shoot ya Magomeni.

Some of the UCLA interns at the shoot at Manzese. Manzese was the location for Uncles's house.



Mama Thecla Mjatta akisome script kabla ya scene huko Tanki Bovu.



Gayle alikuwa in charge kwenye msawala ya chakula. Hapa yuko Manzese.
Bwana Kibira alimdraftio baba yangu kuwa extra kwenye scene. Nyuma ni Mzee Olutu na Mama Thecla Mjatta .


Mbele ni mcheza sinema maarufu wa Bongo, Shafii. anaposi na interns wa UCLA, baba yangu na Peter Omari.


Mama Mjatta na Mzee Olotu wakipata maelezo kutoka kwa Mwuongoza sinema, Josiah Kibira kabla ya kufanya scene Manzese.


Stelingi Peter Omari, kama Juma, ambaye ni mhusika mkuu katika sinema ya Bongokand II.

Kwa kweli nashukuru kuwa nilipata nafasi ya kushiriki katika sinema ya Bongoland II. Ninamshukuru hasa Bwana Josiah Kibira, kwa kuandika script nyingine safi na kufanikisha kutengeneza kwenye sehemu halisi (authentic location) Dar es Salaam. Kwa kweli safari ilikuwa ndefu mpaka kukamilisha lakini yeye na timu yake walikamilisha.

Natumaini sinema ya Bongoland II ikitoka mtaifurahia mno.

Hizi ni picha zaidi na bado sijasafisha mikanda mingine.


Kwa habari zaidi za Bongoland II someni:

7 comments:

Anonymous said...

KWANI MPAKA LEO BADO UNATUMIA KAMERA ZINATUMIA FILM (FUJI, KONICA, KODAK NK).
KWA NINI USUBIRI KUSAFISHA WAKATI UNGEKUWA UNATUMIA DIGI CAMERA, HUNA HAJA YA KUFANYA HIVYO. UNAINGIZA KWENYE BLOG AU PC YAKO MOJA KWA MOJA NA KUZI-EMAIL KWA UWAPENDAO.
MI NILIDHANI KUKAA MAJUU NDIYO KUWA NA VITU VYA KILEO. ETI MPAKA USAFISHE NDIYO UZITIE KWENYE BLOG YAKO. HAHAHAHAAA....HALOOOOOOOOO. UTAJIJU

Chemi Che-Mponda said...

Asante kwa mchango wako. Nina tumia camera mbili, moja film, moja digital maana sometimes za digital zinatoka vibaya. Pia Bongo sikupenda kutembea sana na hiyo digital maana niliogopa ingeibiwa. Hata hivyo picha ukiweka kwenye CD imekwisha kuwa digital, ila sema inachukua muda zaidi.

Anonymous said...

Nani angekuibia Bongo Digital camera? Mbona watu kibao wanazo.
Unajua comment zako za bongo wakati mwingine zimebore.Hoo vumbi,mara Manzese kuko je-Huko ndio kwenu.Kwanza wewe pamoja na kukaa kote majuu unaonekana mshamba sana kuliko hata hao dada zetu walioko bongo

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 5:07 am, asante kwa maoni yako. Ila ungeniambia kuwa wizi hakuna Bongo hapo ningesema sawa sikuwa na haja ya kuwa na hofu.

Anonymous said...

Hivi huyu dada inaelekea ni mshamba sana yaani hata yeye alivyo wewe umezaliwa mjini kweli yaani unavijimambo kama ujaenda shule nasikitika sana nilikuwa na ku admire sana katika watu walioko hapa states nimesikitishwa

Anonymous said...

Na hao manaonymous kwa kujidai. Eti hakuna wizi Bongo. Upo sana. Chemi bora ulijihadari, maana nilishuhudia mzungu akiibiwa kamera Dar. Vibaka wapo na wanongeka sana maana hakuna kazi.

Anonymous said...

Mungiki` waibuka Jijini Dar

2007-08-13 15:58:31
Na Janneth Kiure, Kibaha


Kijana Ramadhani Kigebele,30, ameuwawa kwa kupigwa mawe sehemu mablimbali za mwili na wananchi wenye hasira, baada ya kukwapua simu ya mpita njia.

Kijana huyo alikutana na mauti hayo jana mishale ya saa 4:30 asubuhi, huko Kongowe wilayani Mkuranga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Henry Salewi, amesema mpita njia huyo alikuwa ni mwanamke ambaye aliviziwa na kijana huyo aliyemvamia na kumpora simu yake ya mkononi.

`Mwanamke huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja alipiga mayowe ya kuomba msaada ndipo wananchi wenye hasira kali walipojitokeza na kuanza kumpiga kijana huyo kwa kutumia mawe na kumjeruhi vibaya` akasema Kamanda Salewi.

Kamanda Salewi amesema askari polisi walifika kwenye eneo la tukio kumnusuru kijana huyo ambapo walimkimbiza hospitali ya Mkuranga, lakini akafariki dunia akiwa njiani.