Saturday, December 13, 2008

Kesho nitakuwa kwenye TV show - Brotherhood


Wadau,
Kesho jumapiili Desemba 14, 2008, nitakuwa kwenye TV Show iitwayo Brotherhood. Inaonyeshwa kwenye Showtime. Nimejiona kwenye trela ya kipindi cha kesho saa 2 jioni (8:00pm Eastern). Baada ya kesho itakuwa kwenye cable kwenye On Demand.
Mimi ni 'extra' (background) hivyo siongee. Nitakuwa kwenye scene ambayo mafioso Nozzoli anaongea na Tommy mhusika mkuu wa Brotherhood kwenye mgahawa. Nimekaa nyuma ya Nozzoli nakunywa kahawa, nimevaa koti ya jeans.

10 comments:

Unknown said...

Taratiiiiibu naona hatimaye ndoto zako zitatimia dada.

HONGERA.

Mbele said...

Dada Chemi, hongera. Wahenga walisema: haba na haba hujaza kibaba; pole pole ya kobe humfikisha mbali; ndo ndo ndo hujaza ndoo; mwanzo wa makubwa ni madogo. Nawe kaza buti, kama Waswahili vijiweni wasemavyo; utafika.

Anonymous said...

Nilikuona Da Chemi kazi nzuri!

Unknown said...

Chemi...ndiyo nimekuona katika Bongoland 2. Ilinifikia jana baada ya kuiagiza mtandaoni toka kwa ndugu Kibira. Ama kweli wee mwigizaji mzuri. Na hiyo sinema safi sana. Lazima tujivunie kazi ( au products) zetu Wabongo, na sinema bado ni mali ghafi changa kwetu lakini yenye uwezo mkubwa sana.
Endeleeeni na haya mambo. Tuko pamoja...tutafika tu.

Subi Nukta said...

Hongera da Chemi!
Endelea kufanikiwa na kufanikisha ndoto yako!

Simon Kitururu said...

Hongera Da Chemi!Wembe huo huo!

Anonymous said...

.....GO, Girlie !!

Anonymous said...

sasa wewe chemi mbona unasema wanakuweka nyuma nyuma utafika lini kuwa kama jada piniketi na gaburieli unioni.
Mbollo'
kolumbusi
ohio

Anonymous said...

Halafu haya mambo ya kuecti mamuvi na mavideo dada chemi maboksi unanyanyua saa ngapi mwenzetu?
much love Mbollo

Chemi Che-Mponda said...

Asante wote. Nashukuru sana kwa 'support'. Kwa kweli mmenitia moyo sana.

Mbollo, nitafika kwenye 'A list' Mungu akipenda. Kwa sasa nimekwisha ingia mlangoni.