Tuesday, December 09, 2008

Machifu wa Kingoni walivyonyongwa 1906

Wadau, niliwahi kuanzisha mada hapa kuhusu machifu wa Kingoni walionyongwa na Mjerumani hapo zamani za kale. Niliona hii article kwenye Habari Leo. Ushenzi wa Mkoloni!

*********************************************************

Mashujaa ya Kingoni Walizikwa bila Sanda katika Kaburi Moja
Juma Nyumayo
Daily News; Sunday,August 10, 2008

Wiki iliyopita tuliona vivutio mbalimbali vilivyopo mkoani Ruvuma, kama vile mto Ruvuma, Ziwa Nyasa, Mlima Matogoro na mji mdogo wa kihistoria wa Peramiho. Pia, tuliona kwa ufupi juu ya Jumba la Makumbusho lenye sanamu za machifu 12 wa Kingoni. Leo tunaendelea na sehemu ya mwisho ya simulizi hii.Upande wa kulia wa Jumba hilo la Makumbusho, kuna majina ya mashujaa waliopigana Vita ya Maji Maji mwaka 1905-1907na majina yote hayo yanaanza kufutika.

Katika jumba hilo kwa nyuma, kuna kaburi la pamoja ambalo walizikwa mashujaa 57.Miongoni mwa mashujaa hao 57, kulikuwa na Chifu mmoja na machifu wasaidizi (Nduna) saba.Chifu Songea Mbano alizikwa kaburi la peke yake.Mashujaa wengine 10 kati ya hao 57, majina yao hayakupatikana, hivyo majina yaliyopo ni 47 tu.

Mashujaa hao wa Kingoni pia walipigana Vita ya Maji Maji mwaka 1905 – 1907 na walinyongwa jirani na eneo hilo.Eneo hilo kuna miti mitatu na kamba walizonyongewa, kwa ajili ya kumbukumbu. Katika eneo hilo, kuna ukumbi maarufu mjini Songea wa Songea Club.Baada ya kunyongwa katika eneo hilo, mashujaa hao walizikwa bila sanda katika kaburi la pamoja kwenye jumba hilo la makumbusho.

Mashujaa hao walinyongwa Februari 27, 1906, ambapo Februari 27 kila mwaka, Mkoa wa Ruvuma huwa na sikukuu ya mashujaa ya kuwakumbuka mashujaa hao wa Kingoni.Kwa mujibu wa Kitabu cha Harakati za Ukombozi wa Mkoa wa Ruvuma, mashujaa hao walikuwa wakibatizwa kabla ya kunyongwa. Lakini, Chifu Mpambalyoto alikataa kubatizwa, akidai kuwa haina maana yoyote kubatizwa halafu nanyongwa. Padri aliyekuwa akibatiza mashujaa hao wa Kingoni, aliitwa Yohanes.

Katika eneo hilo walikonyongewa mashujaa hao, huimbwa nyimbo mbalimbali za maombelezo katika maadhimisho ya kuwakumbuka mashujaa hao. Nyimbo hizo huimbwa kwa lugha ya Kingoni.Nyimbo hizo za maombolezo ni kama zile nyingine zinazoimbwa kwenye misiba mingine.Kitabu hicho kinasema kuwa mashujaa hao waliaga kabla hawajanyongwa, kwamba wataonana ng’ambo.

Wengine waliomba wavute kwanza ugoro (tumbaku) kabla hawajanyongwa.Katika mashujaa hao wa Kingoni, wanne walinyongwa kwa mkupuo jirani na eneo lililoitwa Boma la Wajerumani, ambako leo ndiko kuna ofisi za Mkoa wa Ruvuma.Leo hii hakuitwi Bomani tena, bali Mkoani; wakati na eneo ambako walinyongewa mashujaa wengine wengi, kunaitwa Songea Club.

Hata hivyo, jumba hilo la makumbusho liko katika hali mbaya, kwani rangi iliyopo kwenye sanamu ya askari aliyeshika bunduki, imechujuka.Jumba hilo la mashujaa limezungushiwa wigo na ndani yake kuna majengo matatu, yaani jengo kubwa na mengine mawili madogo.Jengo kubwa ni la ghorofa moja na liko katikati. Majengo madogo mawili yako pembeni mwa jengo hilo kubwa. Majengo yote hayo matatu, yamejengwa kwa mtindo wa mviringo, kama nyumba nyingi za watu wa mkoa huo zilivyokuwa zikijengwa.

Mwenyekiti Kamati ya Utendaji ya Baraza la Makumbusho, Said Mkeso, anasema kwamba jengo kubwa ni maalumu kwa ajili ya kuhifadhi utamaduni wa kabila la Wangoni, ambao maskani yao ni Songea mjini.Jengo moja dogo ni kwa ajili ya kuhifadhi utamaduni wa kabila la Wamatengo, ambao maskani yao ni wilaya ya Mbinga.Jengo dogo la mwisho ni kwa ajili ya kuhifadhi utamaduni wa kabila la Wayao, ambao maskani yao ni wilaya ya Tunduru.

Mkeso anasema jengo linalotumika ni moja tu kubwa, linalohifadhi utamaduni wa kabila la Kingoni.Majengo mawili madogo, yameachwa tupu, baada ya kukosekana vifaa vya makumbusho vya makabila ya Wayao na Wamatengo.Jumba hilo la makumbusho liligunduliwa mwaka 1962 na Mkuu wa kwanza wa mkoa wa Ruvuma, Martini Haule. Aliligundua likiwa limejaa nyasi. Haule alifariki Januari 17, 1993 mkoani Morogoro na kuzikwa eneo la Mahenge mkoani Ruvuma.

Jirani na eneo hilo, kulikuwa na makaburi mengine 65 ya Wajerumani waliouawa kwenye Vita ya Maji Maji. Makaburi hayo yalikuwa yakitunzwa vizuri na kulindwa, ambapo baada ya Tanzania kupata Uhuru Desemba 9, mwaka 1961 ndugu zao walikuja kuyafukua na kuchukua miili waliyokwenda kuizika kwao.

Nje na ndani ya jumba hilo, kuna mambo mengi ya kuvutia, ikiwemo sanamu 12 za machifu wa Kingoni jamii ya Njelu.Majina ya sanamu za machifu hao, waliowahi kutawala Songea miaka ya 1902 ni Mpambalyoto Soko bin Msarawani, Nduna Songea Mbano bin Luwafu, Nduna Chabruma Gama bin Hawayi, Zimanimoto Gama Bin Fusi, Nkosi Mputa Gama bin Gwazerapasi, Nduna Zamchaya Gama bin Gwazerapasi.

Wengine ni Mtepa Ntara bin Kanyoka, Nduna Usangira Gama bin Mharule, Magodi Mbano bin Mbamba, Njorosa Mbano bin Mbamba, Masese Parangu Mbano bin Songea, Nyunyusea Mbano bin Njenje na Njorosa Mbano bin Mbamba.Ndani ya jumba hilo la makumbusho kuna picha kubwa ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume ambaye Februari 5, 1977 Chama chake cha ASP kiliungana na TANU na kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pia, kuna picha ya Mwalimu Julius Nyerere akikabidhiwa hati ya Muungano na Rais Abeid Amaan Karume. Pia, kuna picha kubwa ya Nyerere akiapishwa kuwa Waziri Mkuu.Aidha, katika jumba hilo la makumbusho kuna picha kubwa ya mkutano wa wajumbe walioanzisha chama cha TANU Julai 7 1954.Ipo pia picha kubwa ya mnara wa kumbukumbu ya Azimio la Arusha. Kuna pia picha kubwa ya Mwalimu Nyerere akipelekwa mahakamani, kufuatia harakati zake za kudai uhuru.

Eneo jingine linalovutia ni misitu ya miyombo, yenye wanyama na wadudu mbalimbali. Misitu hiyo imeenea na kuunganisha Hifadhi ya Selous na ile ya Niasa nchini Msumbiji ambapo katika eneo la Kilimasera kuelekea Tunduru, kuna ushoroba (corridor) wanayopita wanyama kutafuta chakula. Wanyama hao ni pamoja na tembo wanaovuka kwa makundi makubwa.

Katika wilaya ya Tunduru kuna maeneo ya uwindaji wa kitalii. Uwindaji huo hufanywa zaidi na wageni. Wawindaji wa ndani ya nchi wanatakiwa wahamasishwe ili kufaidi raslimali za nchi.Mbuga ya Mwambesi tarafa ya Lukumbule katika wilaya hiyo ya Tunduru, kwenye bonde la Mto Ruvuma, ni eneo maarufu kwa uwindaji huo.

4 comments:

Anonymous said...

Halafu JK na ulinzi wake wanatembea na magari ya wajerumani! LOL ni aibu tupu

Malisa BG

Anonymous said...

dada Chemi, hii habari ya hawa machifu imenitoa machozi leo, sio kwamba nilikuwa siifahamu, ni kwamba imenikumbusha mambo mengi sana, ni habari ambayo naifahamu tangu nikiwa mtoto mdogo kwani marehemu Babu yangu alinisimulia kila kitu kuhusu unyama huu. Kifupi ni kwamba Baba yake huyo Babu yangu alikuwa ni miongoni mwa hao machifu walionyongwa kikatili, kipindi Baba yake ananyongwa Babu yangu alikuwa na umri wa miaka mitatu tu. toka hapo Babu yangu alikuwa anawachukia sana wajerumani,kumbuka Baba yake aligoma kubatizwa na kuuawa eti akiwa kabatizwa, cha kujiuliza huyo padre aliyekuwa anabatiza kwanini hakuwahubiria hao wajerumani wenzake kwamba hicho kinachofanyika sio jambo jema la kumpendeza mwenyezi Mungu, haiingii akili padre aende kubatiza watuhumiwa wa kunyongwa na asiwaambie wale wanyongani kwamba kuua ni dhambi. Baada ya hapo Babu yangu alikuwa na chuki na wajerumani (kaniambukiza na mie, siwapendi hawa watu kabisa!!.
Halafu huko kuagana kwao kwa kusema wataonana ng'ambo hiyo ni imani yetu, tangu zamani wangoni tuliamini kwamba kuna maisha baada ya kifo, hivyo mtu akifa tulikuwa tunasema daima kwamba tutaonana nae "kumwambu", manake ng'ambo, tukiwa na maana ili kufika huko kuna kuvuka hatua fulani ili kwenda ng'ambo ya pili. Na hata sehemu ya kuzikia sisi wangoni original tunaita hivyo hivyo, kumwambu (ng'ambo).

Unknown said...

tuwaombee mashujaa wetu huko walipo kila ninaposoma hii habari naona kama nashuhudia tukio lile hasa yule chifu aliyeomba avute ugoro kabla hajanyongwa mmhh inasikitisha sana kwakweli,naishia kutoa machozi hapa

isaka venance said...

kwakweli ni huruma na huzuni tupu imetawala kichwani kwangu,yaani wengine waliomba wavute ugoro ndipo wanyonwe aiseee ni uzuni sana,kuwakumbuka wazee wetu ni jambo la baraka sana,tuwaombee kwa mungu nina imani iko siku tutakutana nao