Thursday, December 18, 2008

Tatizo la Maji DSM - Maoni ya Mdau

Tanzania sijui ni Shida sijui ni Umaskini sijui ni nini?

Baada ya wiki nzima ya mateso ya kukosa maji leo asubuhi maji yametoka hapa jijini Dar es saam na umeme ukakatika kwa hivyo vimepokezana,na kutoka kwenyewe yaani yale sio maji ni mchanganyiko wa udongo yaani kama maji ya Cocoa vile.Nikisoma baadhi ya maoni ya wabeba mabox hapa kwenye kijiji chetu cha jamii,uwa wanasema wao wanakunywa maji moja kwa moja toka bombani na bila kudhurika,nikasema lo! Wenzetu wanafaidi sana,na wanapunguza gharama za kuchemsha maji ya kunywa kwenye mkaa,maana ukidhubutu kunywa maji ambayo hayajachemshwa hapa bongo ni kujitakia kupelekwa hospitali ya rufaa kwa kipundupindu na hata kuweza kupoteza maisha kabisa.

Je vipi kuhusu mbanano wa ndani ya mabasi, imagine umepanda basi la kivukoni mbagala au Kariakoo-Mbagala,mwanangu iyo harufu ya samaki na mchanganyiko wa jasho la siku nzima kama ni mgeni lazima utazimia tu,najiuliza ni kwa nini Serikali yetu kama wao hawawezi wakaruhusu wawekezaji wakaja kuwekeza kwenye usafiri wa jumuia hapa mjini ili kuepukana na hii adha ya usafiri ambayo inaweza ikakuambukiza magojwa ya ngozi,mafua,TB na magonjwa mengine ya kuambukiza kwa hewa na mgusongamano?.

Pia uwa najiuliza wapanga miji wako wapi,wewe Mtanzania unayeishi Masaki,Mikocheni,Osterbay Mbezi beach n.k,je umewahi fika maeneo kama ya mburahati ndani ndani ukaona wenzako wanavyoishi huko,choo bado ni passport size,mifereji ya kupitisha maji taka hakuna,mvua ikinyesha vyoo vinatapishwa,unaambiwa utakuta watoto wanaogelea juu ya vinyesi vya binadamu maana ya hapo nenda sasa Amani hosp utakutana na watoto kibao wanapoteza maisha kwa kipundupindu, Tena maeneo kama hayo ukipita usithubutu kifungua kifurushi kilichofungwa cheusi cheusi hivi,wewe yaani kwa jina lingine vinaitwa vibomu huko uswahilini,basi utakutana na kinyesi nyumba zima wamejiachia humo,hii inatokea pale choo kimejaa na hakuna mvua kwa muda kuwezeka kukifungua choo kiondoke mtaani.

Yaani unaweza kusema kipindupindu ni ugonjwa wa maskini,maana idadi kubwa ya wagonjwa ni hao ni wakipato cha chini mno,

Vipi kuhusu Uchafu barabarani na barabara mbovu sizizo na mpangilio hapa town,yaani ni balaa tupu,mimi niliwahi kukaa pale Upanga toka nizaliwe hadi leo,unaambiwa hata siku moja sijaona wakiweka barabara ya rami,kipindi cha kiangazi ni vumbi hadi chumbani,kipindi cha mvua ni kukanyaga maji ya mvua nje yaliyochanganyika na maji taka yaliyoziba kwa sababu ya uchakavu wake ,maana nahisi toka wahindi waijenge enzi hizo hadi leo haijaweza kurekebishwa na watu ndo ivyo wanazidi kuongezeka,Sasa hapo Serikali za mitaa zinafanya nini au ziko kwa ajili ya nini.

Achana na hilo,hadi leo tumekosa kabisa wazoa taka wa kuweza kusema taka zinazolewa hakuna,magari ni mabovu yaani sio Gari la takataka ni Gari taka.na wale wanaozoa wenyewe hawana groves,mabuti wala mask za kuzuia harufu ya uchafu,na utakuta wanakaa juu ya uchafu.

Elimu yetu je ikoje,leo hii ukitaka kuomba kazi lazima waandike uwe unajua kiingereza safi cha kuandiaka na kuongea,mimi kajamba nani vyeti ninavyo lakini School bus huko sekondari na primary sijapanda(yaani sijasoma shule ya kizungu)hivyo kiingereza changu si salama sana. Na watu kama mimi hapa bongo tuko wengi kuliko hao waliopanda School bus,sasa hapo hauoni wametutenga?.

Mimi nasema viongozi wetu wanabahati sana,wanatoa ahadi na hawatekelezi vilevile lakini wananchi wao tumetulia tuli kama maji mtungini tukiomba ipo siku tutakuwa kama angalau mazingira kama Ulaya(Lol)

Umewahi kutembelea mbuga za wanyama kama mkiwa group hivi mmetoka Dar mnakwenda huko,labda vyumba mlivyofikia jirani na vyumba vya wazungu watalii,basi mkiongea na kucheka kwa nguvu,wahudumu wanawafuata,nyie mbona mnapiga makelele kuna wageni watawashangaa.mnyamaze au tutawahamisha,lakini huko mnawasikia hao wageni wazungu wakiongea na kupiga makelele kweli,wangine wanaimba na kucheza hadi usiku kweli,tena nyie mlionyamaza sasa hata usingizi mnakosa kuwasubiri hao wageni hadi nao wachoke walale.Sasa sielewi makelele ya wazungu watalii ni mazuri kuliko makelele ya Wa Tz watalii.

Kuna vitu vingi sana vinaumiza Bongo,kama Rushwa,Kodi kubwa zinazomuumiza mTanzania,Mikataba inayonufaisha wachache n.k

Wadau mimi nafikiri hii Blog inasomwa hata na Serikali yetu sasa tunaweza labda kuwapa maoni wafanye nini ili na sisi tuwe na unafuu hapa Nchini kwetu.

Mdau Dar es Salaam

4 comments:

Anonymous said...

Aisee huyu jamaa amesema everything that really matters to all Tanzanians. I am also very happy that you carried this article on your blog. No reason to carry white women in elevetor and black man entering the elevetor garbage...Lets all deal with real issues that effects all in our beautiful lovely country...Good Job

Anonymous said...

Ni kweli huyu mdau ameongea mambo mengi mazuri, lakini mambo yoote hayo ameyarundika kwene ukurasa huu, mie nazani ingalikuwa vyema kama angesongelea Maji pekee yake kwa leo. Kama anataka kuongelea matatizo mangine basi ayaongelee kivyake.

Sasa hapa sijui hata nichangie lipi kwa sababu kaongelea vifutavyo;
Maji,
Umaskini,
Kipindupindu,
Magonjwa,
Usafiri,
Rushwa,
Kodi,
Mipango miji,
Sewage aka Maji taka,
Uchafu barabarani,
Uzoaji wa uchafu,
barabara za lami,
School bus system,
Elimu, pia
Customer service na
huenda nimesahau mangine yaliyogusiwa na mdau.

Kwa maoni yangu nazani ingalikuwa ni vyema kama mdau angachagua moja tu analotaka kuliongelea kwa sasa ivi kisha tule sahani moja na hilo jambo. Kwa mfano kama angeweka juhudi za mchasngo wake kwenye maji basi labda na sisi wachangiaje tugekuwa na cha kuongezea.

Anonymous said...

Mdau kajaribu kuongea matatizo kwa ujumla ya tz na naona hajafanya kosa lolote,kama utapenda kuchangia changia linalokugusa au changia kwa ujumla.kama kuna mtu anaona anaweza kuchambua moja baada ya lingine ajitolee kutoa makala kila wiki ya matatizo bongo
Uongozi wa TZ unabidi ubadilike sana,wananchi wake wanapata tabu sana.

Kwa mfano Malaria wahusika wanatakiwa wa kukinga malaria kabla ya kugaramika kuharibu mwili kwa madawa kila mara.

Maringira ni machafu sana na maji yanatuama kila mahali hapo Dar es salaam.

Anonymous said...

Anon wa December 19, 2008 10:21 PM umesoma kichwa cha habari lakini cha makala unayoitolea maoni? Kwa kukurahisishia kichwa cha habari ni hiki apa "Tatizo la Maji DSM - Maoni ya Mdau"

Kwa mana hiyo basi mdau aidha maelezo yake yangeeendana na kichwa cha habari au angebadili kichwa cha habari ili kiendane na matatizo aliyoyaandika.