Monday, December 22, 2008

Mwalimu Nyerere Dodoma 1995

Da Subi ametuletea hii:

J.K.Nyerere, Dodoma - Tanzania 1995

Marehemu Baba wa Taifa la Tanzania, Mwl. Julius Kambarage Nyerere alipozungumza na WanaCCM mwaka 1995 katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi huko Dodoma (nadhani ilikuwa ni Chamwino) kwenye mchakato wa kumtafuta mgombea wa kiti cha uraisi kwa tiketi ya CCM, Mwalimu alisema yafuatayo:http://nukta77.blogspot.com/2008/12/jknyerere-dodoma-tanzania-1995.html

Subi

3 comments:

Anonymous said...

Ukumbi wa CCM (Makao Makuu) uko Dodoma mjini, Kuu Road. Chamwino ni makazi ya mkuu wa nchi (ikulu ndogo).

Bado sijasikiliza hiyo hotuba kwa Subi, ila nadhani Mwalimu aliitoa hiyo hotuba kule Mbeya - siku ya Mei Mosi 1995.

Kila nikiingia kwa 'nesi' Subi huwa nakuta mwana-mama ana mtungi kichwani, nasubiri weee (kama alivyosema Subi -tuwe tunasubiri) ila hakuna kitu!

Anonymous said...

Nimeona 'somewhere' kuwa hotuba hiyo ilitolewa ukumbi wa Chimwaga (sio Chamwino) ktk kuchuja wagombea urais 1995 kupitia tiketi ya CCM.

Hapo juu niliandika kwa kuhisi kuwa ilitolewa Mbeya kwa vile siamini kuwa vikao vya chama yanaweza kufanyika ikulu!

Subi Nukta said...

Mdau wa DaChemi, December 23, 2008 2:28 AM,
Tumia hiyo linki aliyoitoa daChemi itakupeleka moja kwa moja kwenye posti yenye hotuba yenyewe.
Ile unayotembelea na kumkuta mwanamama mwenye mtungi kichwani ni ukurasa mkuu wa tovuti, ukitizama juu utaona 'menu' zinazofungua kurasa tofauti za tovuti ambapo mojawapo ni iBlog inayobeba blogu yenye hotuba na posts nyingine.
Ama nitumie anwani pepe (ya gmail) ukitaka nikutumie hotuba kwenye email inbox yako (subi.nukta77 [at] gmail.com)