Monday, December 15, 2008

Rais Bush arushiwa Viatu


Jana Rais Bush, alienda kutembea Iraq kimya kimya bila kuaga hapa Marekani. Tulivyosikia habari kuwa yuko Iraq walisema kuwa eti alienda kuaga huko kwa hiyo siku zake za kuwa rais karibu zinaisha.

Kufika jioni tukasikia kuwa rais Bush alikuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Iraq na mojawao alimrushia viatu vyake kwa hasira na kumtuka Bush kuwa eti ni mbwa! Kwa kweli watu wengi hapa walicheka. Mbavu hawana. Kisa huyo Bush hapendwi kwa jinsi alivyoharibu nchi na kuchafua jina la Marekani kwa nchi za nje. Kati ya marais wote 43 wa Marekani yeye Bush Jr. ndo hapendwi kuliko wote katika historia ya Marekani.

Watu wengine wanasema kuwa bado ana siku 37 za kukaa kama rais, na tutasikia vituko vinginwe. Mambo Bado. Sijui Letterman, Leno na Saturday Night Live watasema nini kuhusu hii tukio la viatu.

Kwa habari zaidi someni:

2 comments:

Unknown said...

Muhimu sana kueleza wasomaji kuwa kwa mila na desturi za Waarabu kutupiwa kiatu ni dharau na matusi kama ilivyo ukitukaniwa mama au mzazi wako, kwetu sisi.
(Ndiyo maana mwandishi maarufu Shaaban Robert akatunga shairi la Mwanamke Si Kiatu miaka ya hamsini, alikuwa akigusia taathira za utamaduni wa Kiarabu katika KIswahili. Kiatu ni hidhaa au a'dhia, kwa Kiarabu yaani asili ya neno, UDHIA kwa Kiswahili)
Tena jamaa aliyerusha alisema Kelebu ("Kalb") ambavyo tunavyojua Kiarabu ina maana Mbwa.
Lakini ajabu Rais Bush alikuwa eti anastaajabu vipi katupiwa kiatu ( akasema saizi ya kiatu ni kumi) alivyo bwege hakujua kuwa katukanwa (labda baadaye walimweleza? hatujaambiwa) na kuwa lengo la kitendo kile si "kupigwa" bali "kutukanwa." Yaonyesha jinsi ambavyo ulimwengu huu umeharibika kuwa na kiongozi kama huyu mbumbumbu kwa miaka kumi. Na kuwa viongozi ni muhimu wanachukua nafasi ya askari wa Mungu, wakiwa ovyo basi wanatu-keleb!!!
Obama oyeee!!!

Anonymous said...

walinzi walichelewa 'sana' kutoka chumbani. kama ingekuwa ni silaha imetumika walinzi wasingeweza kumwokoa rais!
kwa hiyo mimi nawapiga dongo walinzi wake!
mwisho: hata kama bush amefanya mabaya, staili iliyotumika na huyo mwandishi/reporter sio nzuri. viongozi ni lazima waheshimiwe.