Thursday, July 23, 2009

Achapwa Vibaya na Mwalimu


Sikatai kwa asilimia 100 kuchapa mtoto kiboko cha maonyo, lakini inapofikia hatua kama hii, kweli kuonya kwa kiboko ni fundisho ama ni ukatili?

Huyu ni mtoto wa kike, amechapwa na mwalimu wake wa kiume, ni katika Sekondari moja huko Iringa, imetokea jana July 22, 2009, mtoto akaogopa kwenda polisi au hospitali kwa kuhofia kwa mwalimu atamwadhibu zaidi. Aliyenitumia picha hii anasema kisa cha kuchapwa hivi ni hasira iliyojificha kwa mwalimu huyo kwa kushindwa kutimiza azma yake nyingine toka kwa binti huyu.
Nimetumiwa picha hii toka Iringa, aliyenitumia hajajua jambo muafaka la kufanya, naomba kuweka kwenu ili watu wajadili na kutoa mapendekezo kipi kifanyike kuhusiana na hali hii.
Mapendekezo yenu nitayafikisha kwa aliyenitumia picha hii kwa hatua zaidi atakazoweza kuchukula kulingana na maoni yenu.

Subi
**************************************************
Da Subi,

Nilivyokuwa nasoma Zanaki nilichapwa hivyo na Mwalimu fulani. Nilienda nyumbani na maumivu, mama kuangalia kasema hii nchi ya namna gani kuchapa watoto hivyo. Mama yangu anatoka Jamaica. Basi, kesho yake baba alinisindikiza shule. Yule mwalimu alivyomwona alianza kutetemeka na aliomba msamaha. Sikuchapwa hivyo tena!
Kisa cha kuchapwa kwangu - Mwalimu alisema eti nina kiburi cha KiMarekani! Wakati huo miaka ya sabini wengi walikuwa hawajasfiri nje ya nchi na ilikuwa enzi za Ujamaa na Mwalimu Nyerere. Kusafiri mpaka kibali cha Ikulu. Basi hizo gere! Bora siku hizi watu wamesafiri na wanaona dunia ilivyo kweli.

2 comments:

Subi Nukta said...

Pole daChemi kwa kisa chako.
Kwa kweli inabidi jambo lifanyike kuzuia uchapaji unaopindukia hivi.

Anonymous said...

Da Subi naomba ushauri kwa aliyekutumia hii, nimemkuta mtoto ameanguka barabarani ameumia, je nifanyeje? nimuache tu aendelee kuumia au nimpe msaada, au nimpeleke hospitali au nitume maswali kwa wanajamii wanishauri nifanyeje?