Monday, July 13, 2009

OMT at Harriett Tubman Statue

Jumamosi iliyopita, Oscar Micheaux Family Theatre wa Boston ilifanya photoshoot, hapo kwenye sanamu ya kumkumbuka mama aliyesaidia kutorosha watumwa, Harriet Tubman. Sanamu iko kwenye kona ya Columbus Ave, na Concord St. hapa Boston, MA. Mwezi wa tano tulifanya onyesho la Harlem Renaissance Revisited. Sasa tunajiandaa kuicheza tena Boston College tarehe 16 Oktoba.

Clockwise kuanzia mwenye kofia nyeupe: kiongozi wetu Haywood Fennell Sr., Chemi, Ruby Hill, Stanley Everette, David Bowden, Vanessa, Belinda McIlvaine, Joe Banks, Linda Henderson na Maurice Smith aka. Big Moe Da Comedian.

3 comments:

Anonymous said...

Da Chemi habari za kazi na hongera sana na mahangaiko yako ya kila siku.Huwa napenda sana blog yako na wewe pia nakuzimia unavyopambana na maisha. Mimi nina maswali machache hapa;

1. Je, ulisomea kucheza Sinema? Kama ndio wapi?

2. Ni filamu gani uliyowahi kucheza ambayo unaona umeuzwa sana na tunaweza kuipata Bongo?

3. Hizo TV series unazocheza huwezi kuzi-introduce kwenye TV za Bongo tukuone? Maana nadhani huwa unapendeza sana.

4. Hiyo alama ya Star hapa kwenye Blog yako ulioyoandikwa Chemi Chemponda. Huwa ina maana gani? Niliona hata Michael Jackson amewekewa.

5. Nikiomba CD zenye filam zako utanitumia?

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 3:03am, asante kwa maoni na maswali. Majibu ni haya:

1. Ndiyo. Nimesomea kuigiza katika sinema hapa Boston, Massachusetts na walimu kadhaa.

2. Sinema ambayo utaiona Bongo ni Tusamehe, Bongoland II na Maangamizi the Ancient One. Pia nimekuwa 'extra/background' katika sinema kadhaa za Hollywood lakini naonekana kwa sekunde tu. Pia niko katika dakika 20 za mwanzo wa sinema, Aftershock:Beyond the Civil War.

3. Niko katika TV show, Brotherhood, Season Three, Episode 7. Siongei lakini.

4. Hiyo Nyota ni mfano wa Hollywood Walk of Fame, na mtu yeyote anaweza kutengeneza yake kwenye computer. Ila stars ndo wana nyota zilizochongwa katika mawe huko Los Angeles.

5. Sina DVD ila naweza kukuelekeza sehemu za kuagiza.

Anonymous said...

i like u da chemi,uko simple huringi kabisa na unamafanikio,naona wewe ni mfano wa watu wachache waliosoma na wakaelimika,maana kuna watu huku majuu wamefanikiwa kidogo basi maringo ndugu yangu mpaka unachoka.