Tuesday, May 11, 2010

Kifaru Atoroka Zoo Florida

(Pichani - Archie Kifaru aliyetoroka Zoo Huko Florida)

Leo kuna habari kuwa kifaru alitoroka kutoka kwenye hifadhi yake kwenye Mbuga ya wanyama (Zoo) huko Jacksonville, Florida. Kifaru huyo anaitwa Archie na ana miaka 41. Wafanyakazi wa zoo walipoenda kazini asubuhi hawakumkuta kwake. Kwa bahati walimkuta kwenye eneo la tembo. Lakini wanasema Archie alikuwa mbishi na alikuwa hataki kurudi kwake. Ilibidi wampigie risasi enye dawa ya usingizi.

Hebu mwone huyo Archie (pichani). Mbavu zake zinaonekana, anaonekana mnyonge pia. Anajua maisha nje ya hiyo zoo kweli. Lakini sidhani kama anaelewa kuwa kama angekuwa porini asingeishi muda mrefu maana wale poachers wangemwua kwa ajili ya hiyo pembe yake. Eti unga wa pembe ya kifaru inaongeza uwezo wa mwanamme kufanya ngono!

Hapa Boston sokwe alitoroka kutoka Franklin Park Zoo. Walimkuta kakaa kwenye kituo cha basi karibu na zoo. Siku nyingine sokwe huyo huyo alitoroka na kuzaba vibao kila mtu ambaye alikutana naye!

Kwa habari zaidi someni:

http://jacksonville.com/news/metro/2010-05-06/story/archie-rhino-spends-morning-lam

3 comments:

Anonymous said...

thx kiswahili chako cha leo kinaeleweka kuliko kile ulichotumia kwenye ile habari y yule mrundi.

Anonymous said...

Bora Archie akae huko Zoo aishi maisha marefu maana wachina wangechinja mara moja. Hiyo pembe mali kweli si mchezo.

Bennet said...

Nampa pole kwa sababu anaishi maisha marefu lakini yasiyo na ladha hayuko huru, kwa sababu kama angeishi porini bila kuwindwa angeinjoi zaidi