Thursday, May 20, 2010

Mtumishi wa Mungu Mama Habiba Atakuwa Dallas!

Wapendwa katika shamba la Bwana. Ninayoheshima kukukaribisha ili uweze kukutana na mtumishi wa Mungu Mama Habiba.Inawezekana umewahi kumsikia huyu mtumsihi kwa namna moja au nyingine au hujawahi kumsikia.Mama Habiba ni mama aliyepewa karama ya maombezi na Mungu na amekuwa akiifanya hii kazi kila Mungu alipompeleka.Watanzania wengi wanaoishi hapa Marekani wamekuwa wakisafiri kwenda Houston ili kuombewa na mama huyu na wengine wengi kwa mamia wemekuwa wakiombewa kwa njia ya simu.Mama Habiba atakuwa mgeni wetu kuanzia Jumamosi mpaka Jumapili (22&23/5).

Mama Habiba atafuatana na ujumbe wa watu kama 20 ukiongozwa na Dr.Jerrry Mng'wamba.
Kutokana na uwezo wa ukumbi wetu na ushauri tuliopewa hatutaweza kuchukua watu zaidi baada ya ukumbi kujaa.Ninakushauri ujitahidi kuwahii ili uwe na uhakika wa kupata nafasi ya kukaa bila usumbufu.Milango itakuwa wazi kuanzia saa kumi na moja kamili jioni.

Kwa Maelezo zaidi; 214 554 7381, 682 552 6402, 214 773 6697

Mungu akubariki sana na naomba ufoward huu ujumbe kwa kila mtu bila kujali dini,kabila au nchi anayotoka.

Pastor
Venue:
Trinity Church
12727 Hillcrest Road
Dallas, Texas 75230

Jumamosi kuanzia saa 12 jioni 6:00PM

Jumapili 9:00AM to 11:00AM (saa tatu hadi saa tano asubuhi)
na 5:00PM - 8:00PM (saa 11 hadi saa mbili jioni)

1 comment:

stevie said...

mimi ni mkristo na mkazi wa houston ,huyu mama anapatikana wapi hapa?