Tuesday, March 01, 2011

Askari Wa Vita Vya Kwanza ya Dunia - German East Africa

Hii ni meli ya kivita Mjerumani SMS Konisberg ikiwa imita nanga bandarini Bagamoyo. Bagamoyo ilikuwa mji mkuu wa Tanganyika enzi za MJerumani
Askari kwenye foleni
Waliopitia JKT wataelewa hii...ROUTE MARCH!

Sijui ni Tanga au Bagamoyo hapo au Itakuwa kwenye Ziwa Victoria au Nyasa

Hao watakuwa wale Asakri wa kwanza kabisa. Hawana viatu!

Askari wakisfisha bunduki zao

Enzi za MJerumani walikuwa wanatumia Rupia siyo Shilingi


Bahati mbaya hatuna majina ya hao Askari pichani



The Force Publique in German East Africa during World War One

3 comments:

Anonymous said...

Hongera sana kwa kutuletea historia yetu wakati wa kipindi hiki cha mjerumani. Watu wengi Tanzania sio wasomi wa historia na watu wengi hawajui kabisa kilichotokea na historia iliyochangia kutufikisha hapa tulipo. keep up the good work.

Mchungaji Dar es salaam

Anonymous said...

Picha ya Meli hapo juu ni hiyo hiyo Konisberg. Manowari hii bomba tatu haikuwahi kwenda lake Nyasa wala Victoria.

Meli hii ilipigana vita bahari ya hindi na mwisho wake iliharibiwa na wajerumani wenyewe Mto Rufiji baada ya kuwekewa "blockade" na waingereza katika juhudi za kuiangamiza. Mwenzake alikuwa ni MHS somali naye amezamishwa maeneo ya kusini Tanzania bahari ya hindi

Anonymous said...

Sasa naanza kuelewa, kumbe ule mnara wa askari kimavazi anafanana na askari hawa!