Friday, March 25, 2011

Dawa ya Babu Sasa Habari ya Kimataifa



Watu Wanaaapa Inafanya Kazi! Nasikia hata wazungu wanakwenda Loliondo sasa!

Kwenye Part 2 msikie Babu akisema mwenyewe kuwa dawa yake inatibu, HIV/AIDS (UKIMWI), Diabetes (Kisukari), Cancer (Saratani), Asthma (Pumu), Kifafa (Epilepsy). Anasema kuwa mtu anahitaji kikombe kimoja tu cha dawa. Mungu ameweka dawa kwenye. Anaseme kuwa lazima unywepale Loliondo, huwezi kupeleka nje ya pale la sivyo haitafanya kazi. Anasema kuwa Mungu amemwambia kuwa watu watatoka mbali hadi Ulaya, Asia kuifuata.

Kwa UKIWMI anasema mwenye UKIMWI atapona baada ya siku saba.

10 comments:

emu-three said...

Duh, kweli babu sasa maarufu!

Anonymous said...

"Hapa Arusha KILA HOSPITALI IMEPOKEA WATU WA MAGONJWA YA PRESHA, KISUKARI, PUMU, N.K. AMBAO WALIKWENDA LOLIONDO "KUTIBIWA" MARADHI HAYO NA BAADA YA KUPATA "NAFUU" (PSYCHOLOGICAL) KWA KAMA WIKI MBILI TU WAMEANZA KUUMWA SERIOUSLY NA KURUDIA DAWA ZAO ZA HOSPITALI TENA.

Pili, mimi nikiwa mfanyakazi wa maabara ya hospitali ya MT Meru, sijaona hata mgonjwa mmoja wa ukimwi aliyepata "seroconversion" yaani kurudi "seronegative from serpositive status". Kinachosikitisha ni kuwa kuna watu hawataki kabisa kusikia yanayosemwa na madaktari na wafanyakazi wa hospitali mbalimbali hapa Arusha ambao kila siku tuna-deal na watu wanaozidiwa baada ya kwenda Loliondo.

Mbaya zaidi kuna magazeti, tv na redio hayataki kabisa kusikia ukweli wa majanga yaliyowafika watu waliokwenda huko. Ajabu pia ni kuwa kuna watu ambao ukitaka kuwaeleza ukweli wanakuona wewe ni mpagani usiyemwamini Mungu. Naomba waandishi wa habari wawe proactive katika kutafuta ukweli na si kutegemea mass hysteria iliyowakumba maelfu ya watu wanaotafuta miujiza kwa nguvu

Anonymous said...

"hata wazungu wanaenda loliondo"...duh!!! mpaka leo wazungu badi tuu kipimo chako cha ustaarabu? I used to think you are better than that chemi. Na kwa ninavyokujua kama huyu babu angekuwa m-nigeria basi ungemshambulia ile mbaya.

Anonymous said...

Tafadhali, tunataka nyie waandaishi wa habari mfanye uchunguzi. Mpata watu 10 waliothibititshwa ni wangonjwa. Halafu tupate vipimo vyao kama miezi mitatu baada ya kwenda kwa babu. Hapo tutaamini dawa infanya kazi.

Anonymous said...

Pamoja na kuwa tofauti na misimamo ya mtu lakini huwezi kuwa tofauti siku zote.
Kwa hili naungana na dada yangu Hildegarda kwa maoni yake.
Tukiangalia katiba yetu ingawa si yote yanafuata katiba Serikali ya Tanzania haina dini na dawa ya Babu inaenda kwa imani ya kidini kuwa lazima uwena imani kuwa dawa hiyo imeshushwa na MUNGU kupitia babu na lazima unywe kwa babu nasi vinginevyo.
Kama tutaanza kutoa hoja za kuwa serikali itengeneze miundo mbinu, ipeleke huduma kama vitanda vya wagonjwa na viti vya kukalia wakati wanasubiri huduma kama hospital nadhani tutakuwa hatutendi vyema.
Nadhani kama serikali ina ratiba ya kupitisha road huko ifanye hivyo lakini si kwa kukumbatia imani fulani. Kesho akipatikana wa romani katoliki, TAG,EAGT, zaoist, buddhist, Ahamadiya, Confuzianism,uzoroast, jainism, bahai, uhindu, african traditional religions etc na zote hizi ni imani na anaponyesha za watu na wamesimama huko kama ulivyo wewe na mwingine aliko. Huyo mtu naye anatoa dawa kama babu Je? serikali tuiombe ipeleke miundombinu?

Mie nadhani fungu la kumi lifanye kazi hiyo kuimarisha miundo mbinu vinginevyo babu aseme kama amembiwaje katika dawa yake masharti yamo naya kujengewa au kupelekewa huduma.

Kwanza yeye hataki watu watolewe sehemu za huduma kama hospital maana yake wanaowatoa wakiwa hoi na kufia njia wao ndio wanatenda dhambi ya kusaidia kuua. ingawa siwahukumu. wanasikia huko hakuendeki lakini mtu analazimisha kwenda na kwa sababu serikali kwa kuwa haiwezi kuingilia na kwa sababu hata wakubwa wanaenda huku kwa taarifa ya vyombo vya habari.

Mie nadhani tunatakiwa kuelewa kwa kuwa tunaimani na dawa hiyo na hasa wale tunaoiamini tujipange vyema katika kwenda tusije laumu serikali.

Kwa wabunge wanaopeleka watu wao hakuna kosa kama wakipona heshima kwao lakini wakipata madhara wasijeigeukia serikali kuwa kwa nini iliruhusu. Pia kumbuka hawa wana hisa za kisiasa. na wabunge wakimaliza zoezi hilo warudi majimboni kujenga shule , kuweka vitanda katika hospital, maji, watengeneza njia hata kwa greda pekee inatosha watu kutumia na kuwahi hospital wazazi wasijifungulie njiani. Pia wakumbuke kupeleka ambulance hospital kama wanvyotaka iende kwa babu.

NB: SIPINGANI NA TIBA YA BABU NA NINAUNGA MKONO LAKINI UKWELI TUUWEKA BAYANA NANI AFANYE NINI NA NANI ALAUMIWE KWA NINI?

Anonymous said...

No wonder we Tanzanians are ranked as the most superstitious people in the world. You can image even national leaders openly going for the magical healing. I can see very little reasoning here.

Anonymous said...

Kama Tiba ni haifanyi kazi kwa nini watu wanazidi kwenda? Acheni kuchanganya watu. Hata Hospitalini watu wanakufa na malaria au Typhoid ambako dawa zimeshagunduliwa. Sababu za mtu kufa ni nyingi tu. Mchungaji hazuii watu wasife sema anatibu na "Success Rate" yake ni kubwa sana. Sasa huwezi kutumia wale wasiopona kama kigezo. Tunawafahamu wengi waliopona na kupata nafuu pia. Sukari inaposhuka kotoka 18 mpaka 4 usiniambie hiyo ni Psychology. It is real.

Anonymous said...

Video hii imeshutiwa na kuwekwa na wakenya. Sijawahi kuona hata mara moja Wakenya wakiisifu Tanzania kwa lolote. Wao huwa ni kubeza tu. Watu walioshuhudia kupona ni wengi sana na ndio hao wanaofanya na wengine waende kupokea tiba. Hapa Dar Muhindi alikuwa amenunua soda na kugawa kwa watu akifurahia kupona kisukari. Hapa mtaa wa Jamuhuri. Sasa wale ambao hawajapona labda wamevunja masharti. Mchungaji amesema ukipona ukimwi uache uzinzi. Na Sababu zinazofanya wengine wafe ni nyingi tu. Mbona muhimbili watu wanakufa kwa magonjwa ya kawaida tu ambayo tiba yake ipo. Mpaka sasa Mlaria ndiyo ugonjwa unaoongoza kuuwa watu ijapokuwa dawa zake zipo nyingi. Sasa Msishambulie mchungaji kwa sababu ya vigezo vingine tu. Watu siyo vichaa waanze kupanga foleni msituni eti " Mass hysteia" Madaktari bingwa wa Muhimbili walikwenda kunywa dawa tena ni madaktari wa kisukari.

Inferiority complex siyo nzuri watanzania. subirini muone wazungu watakapoongezeka kupanga foleni na vyombo vya magharibi kuanza kuripoti ndiyo hapo mtakapoona watanzania wenye kasumba nao wataanza kuisifia hii dawa

Anonymous said...

Da Chemi, Nilikuwa naomba uweke mada tuwajadili wa kenya " Our neighbors from Hell".
Wakenya wanatuonea wivu sana na siku zote wanafanya mikakati ya Kutuzamisha.

1. Wametuibia Tanzanite na wao ndio wanaongoza kuisafirisha overseas

2. Walituzuilia kuuza pembe za ndovu zilizokamatwa kwa maharamia tusiziuze kwa manufaa ya nchi. Wakalazimisha zichomwe

3. Wanapinga tusijenge barabara ndani ya Serengeti kwa wivu tu ili tusinufaike

4. Wamejenga uwanja wa ndege mpakani (Moshi) ili kuihujumu Kilimanjaro Internationa Airport. Ili watalii wasiwe wanakuja moja kwa moja KIA.

5. miaka yote wamedanganya mlima kilimanjaro uko kenya.

6. Wamaendaa "Loliondo Wonder" video kuiponda dawa yetu na kuzuia watu mataifa ya mbali wasije huku Loliondo kwa wivu tu.

7. Wakenya ni majirani kutoka Kuzimu "Neighbors from Hell

Mdau Dar es salaam, Tz

Anonymous said...

hiyo dawa ni imani yako kuna ambao nawafahamu wamepona kuna mmoja alikuwa na kisukari mwingine alikuwa na canser hajaenda kazini kwa mwaka mzima kwa kuumwa lakini kaenda kwa babu anaweza tembea kapata nguvu na kidonda kinakauka kwa hiyo kwa hali ayokuwa nayo mwanzo na sasa ni tofauti kubwa sana maana ameweza kurudi kazini anamshukuru mungu azidi kumpa nguvu na kupona alienda na mwanae wa kike ambaye kaasilika hiv point zake zimepungua sana na kapata nguvu naye anasubiri zifike siku 21 arudi tena hospital kucheck.na kuna jirani mwingine ambaye hali yake hajapona kwahiyo nenda huko ukiamini mungu atakuponya