Wednesday, September 05, 2007

Hongera Miss Tanzania 2007Natoa pongezi kwa mrembo Richa Adhia, kushinda Miss Tanzania 2007. Richa alikuwa pia Miss Kinondoni 2007. Natumaini utatuwakilisha vizuri huko kwenye mashindano ya Miss World, Miss Universe. Siku ya kwanza kumwona Richa nilijua atashinda Miss Tanzania kama majaji watakuwa fair.

Pia natoa pongezi kwa majaji wa Miss Tanzania 2007. Waliweka ubaguzi pembeni na kuangalia sifa za warembo. Nasema hivyo kwa sababu kumetokea mzozo kuhusu asili ya Bi Richa. Yeye ni mTanzania mwenye asili ya kihindi. Lakini ni mTanzania. Kazaliwa Tanzania na kakulia Tanzania na ni nchi yake na yeye hana haya kusema kuwa yeye ni MTanzania.

Mbona kuna waTanzania wengi wenye asili ya kihindi. Tena wengi wanafanya mazuri. Kuna wana siasa kama akina Mheshimiwa Shamim Khan, na marehemu Amir Jamal. Na tunaowaona wengi huko Tanzania ni wafanyabiashara, walimu, na maengineer.

WaTanzania tujifunze kupenda waTanzania wote, awe mzungu, mwarabu, China nk. tuachane na ubaguzi maana ni sawa na ukabila.

Nakumbuka nikiwa shule watu walifundishwa kuchukia wahindi. Nakumbuka kuona mvulana mweyewe asili ya kiafrika akivuta nywele ya mwanafunzi mwenzake mwenye asili ya kihindi. Na tusisahau Rev. Mtikila alivyosababisha wahindi wachukiwe kwa kusema wao ni 'magabachori'. Nadhani sababu moja ya hiyo chuki ni kwa vile kuna wahindi amabao wanajitenga na waafrika na mambo yao yanakuwa siri. Ukienda Carribean utaona wahindi, lakini wako sawa na weusi kwa maongezi, mila, wala hawajioni kama wametoka Asia.

Tukitaka maendeleo tuachane na fikra za kibaguzi tuwe na umoja, tuonyeshe dunia kuwa waTanzania ni tofauti na nchi zingine. Na tumeshafanya hivyo kwa kuishi katika amani miaka mingi. Naomba tuendelee kuwa hivyo.

Pia kuchaguliwa kwa Richa inaweza kuwa ni strategic move mzuri, maana watu wataona kuwa kumbe Tanzania kuna watu wa rangi mbalimbali na tunakaa kwa umoja na amani. Kama Flaviana alivyokuwa na upara na mwaka huu watu watamtazama Miss Tanzania kwa macho mkakubwa, maana watasema hivi Tanzania si African Country?

Richa uendelee na poise yako, na uonyeshe uzalendo wako wakiTanzania huko mbele. Utafika mbali.

Huko Italy walikuwa na Miss Italy mweusi 1996. Mama yake mzungu wa Italy, baba katoka Domincan Republic. Naye alipata upinzani kwa vile alikuwa ni mweusi na watu walisema hawezki kuwakilisha waItaly. Lakini Mungu yupo, waItaly waliungana na kumsupport alivyoshiriki kwenye mashindano ya Miss World. Kwa habair zaidi za Denny Mendez soma:

http://en.wikipedia.org/wiki/Denny_Mendez

19 comments:

Anonymous said...

Asante Da Chemi. Maoni mazuri. tatizo letu sisi waafrika ni kuwa tunawaonea wivu wahindi. Mhindi akipata pesa anaweka kwenye godoro na kusevu. Sisi tukipata tunakwenda kunywa pombe kujionyesha. Tuige wahindi na tuweke pesa yetu kwenye magodoro tuwe matajiri.

Simon Kitururu said...

Hongera Miss Tanzania 2007!
Pamoja na kwamba ukabila bado upo Tanzania naombea tusikuze na ubaguzi wa rangi pia.

Kumbuka ubaguzi wa rangi upo hata kwa watu weusi wenye asili ya Afrika kwa wenzao, watu weusi wenye asili ya Afrika. Nishashuhudia wa maji ya kunde wakibagua weusi tii hata katika kigezo cha nani mzuri.
Ubaguzi hausaidii kitu ! Na niaibu kuwa bado tunauendekeza ingawa tukibaguliwa sisi tunalalamika.

Anonymous said...

Haya Da Chemi umeacha kusisitiza hilo la kujibagua kwa madhumuni yako binafsi. Labda siku nyingine ukipata nafasi utatoa wito wenzetu watzWahindi wapunguze kujitenga na kujiona bora. Hata wewe mwenyewe jitenge na familia yako na kijiji uone kama hutobaguliwa pamaja na rangi yako kama yangu.

Anonymous said...

Huyo Miss Tanzania ana epitaite kubwa kweli. Ona sahani umejaa na anadokoa chakula kwa huyo rasta!

Anonymous said...

hata mie nampongeza huyu binti.
Ni kweli-wabongo tuache fikira za kibaguzi.

Nafikiri na wahindi nao wanajitenga mno, wengine wamezaliwa hapo lakini hata kiswahili hawajui.

Mie nafikiri sisi weusi tuache ubaguzi na hao wahindi waache kujitenga, mfano tunahitaji kuona ndoa za wahindi na waswahili kwa wingi zaidi.

Anonymous said...

Acha ndoto! East Africa sijui wahindi wetu wakoje wanajibagua. Ila sehemu zingine wana mix freely na weusi wazungu. Niliwahi kusikia huko City Centre, dada wa kihindi alipata mimba ya Houseboy mwafrika. Mtoto alizaliwa mixed mbona wahindi walimwua yule mtoto. sisi weusi tunaweza kuwakubali wahindi ila wahindi hawatukubali.

Anonymous said...

Hongera Bi Richa Adhia, ila sijafurahia ushindi wako , ila hata nisipokupa Hongera , tayari umekwisha shinda.
Mimi sijui utaenda kuwa kilisha nini watu weusi.
Pili, wewe richa ni mfupi sana, najua fika hutoshinda kwenye miss world na huko hakuna cha wahindi wenzako kukusaidia ushinde kama Tanzania, pole sana.

Anonymous said...

Da Chemi hakuwa Miss Kinondoni huyo, alikuwa mshindi wa 2, Miss Kinondoni.
Wao wahindi ndio wameanza kutubagua, kwanini na sisi tusiwabague?.
Ushindi wake ni dili limechezwa.

Anonymous said...

chemi hebu nenda kwenye blog
ya www.haki-hakingowi.blogspot.com
ukaone maneno ya hoyce temu juu
ya miss tanzania huyu 2007,
yaniii tumefikia pahala pa kubaguana kiasi hikiii..
Mimi nasemaa baba wa taifa
haki ya mungu anageuka kaburini....
BY
WAZO

Anonymous said...

kelele nyingi sana mnaniumiza kichwa na huyu mhindi wenu mimi sitaacha ubaguzi kwasababu wao ndio wabaguzi wakubwa wanataka tuwapenini tumewakaribisha tumewapa pakuishi bado heshima hakuna pita upanga ukute wanavyopelekeshwa dada zetu wakina fatuma na juma mpaka watoto wadogo mimi kunasiku nilienda kwenye party ya Familia mtoto wa kihindi akatema mate kwenye chakula changu ikabidi nijizuge nitawatenga sana tu na wenye tabia nzuri nitawapenda sana maana hata mimi nina rafiki wahindi kama ndugu zangu watu wote walio soma India mnawajua wahindi sio sinala zaidi

Anonymous said...

Ni muda mrefu dada chemi sijakutembelea hapa, kuhusu huyu binti mjadala hauwezi kuisha kijuu juu tu, wahindi waliopo hapa Tanzania wamejitenga katika tabaka lao.Wanaishi uhindini,wanasoma uhindini,wanatibiwa uhindini,hawaendelezi nchi yetu,wanachuma tu kwetu, ni waajiri walaliaji kwa walalahoi wa nchi hii, wao ni walala heri ndani ya nchi ya walala hoi.Kila siku iendayo tabako lao la waajiri linakua nasi tukiendelea kuwa chini yao, wanaposema nchi imeuzwa usifikiri ni masihara.Wahindi nitawaona kama watanzania watakapoanza kuishi nasi uswahilini, kusoma shule zetu uswazi,pale vingunguti 'A', kusali makanisani na sisi kucheza mpira na sisi, kujiunga na upolisi, ualimu shule za msngi vijijini,ushaona muhindi trafiki?,ushaona mhindi polisi,open your eyes guys,
Acheni kusimamia hoja dhaifu.Utanzania lazima uwe na utambulisho nao ni utanzania wenyewe, kama mzazi wake mmoja angekuwa mtanzania mi nisingejali, lakini huyu binti ni mhindi kabisaaaaaaaaaaaaaaa.IKO SIKU ATACHAGULIWA MZUNGU ALIYEZALIWA TANZANIA MTATUAMBIA POA TU!, jamani mambo ya hovyo tuyakemee. Mi si mbaguzi nachukia zaidi katabaka kao hawa. Hawajichanganyi na sisi.
Mtake msitake ukweli unabakia kuwa hawezi kuwa muwakilishi wa Tanzania kwa kuwa habebi sura ya watanzania, uwakilishi wake unapwaya!, tena sana. Ni lazima tuwe na PRINCIPLES tuzifuate na kuziheshimu.
Tumejidhalilisha kuwakilishwa na muhindi!!!!!!!!
Ningekuwa waziri mwenye dhamana na utamaduni ningeubatiisha uamuzi huu
Mjadala uendeleeeeeeeeeeeee!
Mtu mzima.

Anonymous said...

Yani sijapata watu wabaguzi kama wahindi, wako hapa nchini kwetu lakini badowanatubagua kwa kila kitu karibia. Mi nashangaa Chemi anavyokazana kuwasapoti hivi unategemea siku moja MTANZANIA akapata nafasi ya kushiriki Miss India acha kushinda kushiriki tu. Ni wabaguzi ajabu. Kwanza wanaona ngozi nyeusi ni takataka tu. Kama kweliwanaupenada uraia wa Tanzania mbona wanakuwa na passport mbili, moja ya Canada moja ya Tanzania. Wako hapa kuchuma tu then wakaishi Canada.Mi naungana na Hoyce Temu na watanzania wengne walioguswa na ubabaishaji huo kwa asilimia 100.

Anonymous said...

Hakika nawaambieni PUNDA HAWI FARASI, mhindi ni mhindi na mtanzania ni mtanzania tu. Suala la uzawa ni lazima lipewe kipaumbele haiwezekani hata siku moja mtanzania apewe nafasi ya kugombea umiss huko India. Hawa wahindi wa Bongo wengi wana uraia zaidi ya miwili mpaka mitatu, utakuta mhindi mmoja anamiliki pasipoti zaidi ya tatu Tanzania, Canada, United Kingdom na India, sasa bado tu mnakazana hao magabachori ni wenzetu. Niambie kuna mhindi gani yuko jela au keko? kwani wao sio wezi? Naunagana na Hoyce Temu kupinga matokeo kwa nguvu zote, hata kama angekuwa na vigezo vyovyote vile bado hastahili kuiwakilisha Tanzania. Nyie manaojifanya sio wabaguzi hebu nendeni India mkaone weusi wanavybaguliwa.

Namsifu Mhe. Idd Simba pale alipoibua suala la uzawa. Ni lazima watanzania wapewe nafasi ya kuwakilisha nchi yao sio Gabachori. Watanzania ni wakarimu na sio mbumbumbu kama wahindi wengi wanavyofikiria, wanakuja hapa masikini wana-iba-iba rasilimali zetu, wanafungua mabiashara makubwa makubwa halafu wanatunyanyasa. Angalieni na huko Bungeni jinsi wahindi wanavyojipenyeza sasa kuna siku tutapata Raisi Gabachori. Siwapendi Wahindi wote wa Bongo sababu ni wabaguzi, wanafiki, wanawatumikisha watanzania kwa ujira mdogo,na huku wao wanatajirika, pia hawana urafiki wa kweli. Anakuhitaji pale ana shida akipata anakubwaga. Watanzania amkeni magabachori sio wenzetu ni adui zetu!!! Na ndio sababu Idi Amini aliona mbali akawatimua Uganda. Na iko siki na sisi tutawatimua Tanzania mrudi kwenu India mkalale barabarani.

Hongera Hoyce Temu kwa kusema kweli tupu!!!

Anonymous said...

We anonymous wa September 06, 2007 5:49 AM umejaa ubaguzi maana una chuki, hasama, hasira na inavyoonyesha hata skuli hujasoma. Unaposema Idi Amini alipofukuza wahindi Uganda - ulisahau kwamba wakaitwa baadae kuja kuchukua mali zao - kumbe nchi waganda iliwashinda.. wewe huna uwezo wa kumfukuza mhindi hata mmoja mtanzania hapa TZ - kama unachuki kaa nazo - wahindi wanapata utajiri kwa kufanya kazi na kujitahidi sio kulala tuu kutwa nzima.. mbona wewe ulishindwa kwenye nchi yako kuupata huo utajiri?

Watu wanajitahidi kujiendeleza wewe ndio kwanza unawarudisha nyuma.. jee akishinda huyu Richa atabeba bendera ya TZ au ya India? Si atarudi nao huku TZ? hatoingia mitini huko China - ushasahau kisa cha wasanii kutoka zanzibar ambao walikwenda kuiwakilisha ulaya wakakimbia kambini ili wapate kujichoma huko? walikuwa ni wahindi hao? hawakuiabisha Taifa hapo? ukizungumzia wahindi kuwa na pasipoti mbili basi hao wazanaibari wakataka uraia wa nguvu bila hata pasipoti.. ona haya, kwanza sio unaropoka ovyo tuuuuuuu

Anonymous said...

Anon September 08, 2007 2:03 wewe acha kumshupalia mwenzio yeye ndio maoni yake hata mimi na msupport nasema hata Tanzania ikishinda mwaka huu roho itaniuma sanaaa yaani round ya kwanza ya introduction mimi nataka TZ nje shauri yenu na mwindi wenu sijali utanifikiria nini au unanichukuliaje ........... mimi ni mbaguzi sana wa wahindi(gabachoriiii) sifichi waaaawaaaa
mbona mimi nimezaliwa England sasa nijiite mwingereza wakati wazazi wangu wa Tanzania hapa natafuta hela tu na elimu yangu halafu moto chini narudi kwenye asili yangu bongoo

Anonymous said...

We Anon wa September 09, 2007 10:44 PM . Sifikirii kama kweli umezaliwa England na una ishi huko. Kama ni kweli basi usingelikuwa mbaguzi kabisa kwani ungelijua uzito wa kukaa nchi ya kigeni na kubaguliwa hasa kama ni black kama wewe basi wazungu wanakuona taka taka tu, bado wewe una ubaguzi kiasi hicho. Sifikirii hata kama skuli huko uingereza umekwenda - pengine ni mtu wa njiani tuu

acha ubaguzi kabisa - nchi haitaendelea ikiwa ina watu kama wewe. Richa keshashinda, ni Miss TZ, ni mrembo na anayaweza mambo - wewe utabaki kukodoa macho tuuu - unafikiria huyo hoyce temu aliyelia machozi alifika wapi? mbona kaa alikuwa ana vigezo na kuchaguliwa kuwa miss TZ miaka hiyo hakuambua kitu

acha ubaguzi - nenda ukasome, poa moto

Anonymous said...

Hongera Sana Richa (Miss Tanzania 2007). I see her on Sundays and to be very frank, she has fantastic feet and Toes. Yani, i love her toes.

See you on Sundays (S.J)

Anonymous said...

Hongera Sana Richa (Miss Tanzania 2007). Mimi namwonaga Richa kila jumapili na kusema kweli, huyu mrembo ana miguu and vidole vyamiguu bab kubwa.

Mwema ukweli ni mpenzi wa mungu.

Anonymous said...

Jamani, kusema kweli Richa HAFAI KABISA kutuwakilisha watanzania. Unajua tatizo letu huwa tunajifanya wakarimu kupita kiasi ndo maana hatuendelei. Hafai kwa kila hali, hana vigezo kulinganisha na baadhi ya washiriki wenzake na pia tungependa kuwakilishwa na mtanzania halisi kwa kila kitu. Nyie mnaojifanya si wabaguzi hebu nendeni India mkajaribu kugombea kama mtaingia hata zile hatua za awali!!! Toeni unafiki hapa.