Friday, September 21, 2007

Ubaguzi wa rangi bado upo Marekani


Hii picha hapo juu haijapigwa mwaka 1960. Umepigwa usiku wa kuamkia leo huko Louisiana!
Vijana wa kizungu walikuwa wanazunguka na hiyo pick-up enye 'noose' (kamba ya kunyonga watu weusi) katika mitaa ya Alexandria, Louisiana.
Weusi wengi walifika katika huo mji baada ya maandamano makubwa ya weusi kudai haki kwa ajili ywa vijana wa shule sita waliofungwa jela zaidi ya miezi tisa huko Jena, Louisiana. Walikuwa wanangojea mabasi ya kurudi makwao ndo hao vijana walianza kuwapita na kuwatishia! Polisi walikamata hiyo gari na vijana wa kizungu waliokuwemo. Vijana hao walisema kuwa wao pamoja na familia zao wako katika kile kikundi cha kigaidi hapa Marekani Ku Klux Klan (KKK). Hao KKK wameua maelefu na maelfu ya watu weusi Marekani bila kuchukuliwa hatua yoyote!
History ya Marekani kwa watu weusi ni mbaya na bado wanazidi kuonewa. Wanaume weusi wengi wamefungwa gerezani. Weusi wanapata elimu duni na pia wanabaguliwa hata katika kazi!

Kwa habari zaidi ya hiyo tukio someni:

6 comments:

Anonymous said...

These are ridiculous "trailer trash" teens who have nothing better to do than cause trouble! They should be concentrating on school and furthering their education instead.

Anonymous said...

The kid who the Jena 6 allegedly beat up has dropped out of school. Before that he was in trouble for bringing a loaded gun to school!

Anonymous said...

Poleni sana mnaobaguliwa.Msilipize kwa kubagua.Inasikitisha kwa nchi inayosimama na kujinadi kuwa wao ndio baba wa Democracy.

Tujifunze kutoka kwa Martin Lether King.

'I HAVE A DREM'

Anonymous said...

aluta continua!

KakaTrio said...

Hio gari mbona haioneshi kama ni ya miaka 1960's?

Anonymous said...

Ni kwa sababu ilitokea juzi 2007.