Thursday, September 13, 2007

Ujumbe kutoka Kaka Lazurus Mbilinyi 'Mawaidha kuhusu Ndoa'

Wapendwa wasomaji nimepata ujumbe huo kutoka kwa Kaka Lazarus Mbilinyi ambaye aliandika somo la NDOA NA UNYUMBA ambayo umeisoma kwenye blog hii:

http://swahilitime.blogspot.com/search/label/Mbilinyi

**************************************************************************
Dada Chemi,

Mimi ndo Lazarus Mbilinyi niliyeandaa hilo somo la ndoa na nyumba na kwa bahati mbaya nilikuwa sijui kama linaweza kusomwa na mtu yoyote kwani katika kuliandaa niliandaa katika mazingira ya Tanzania na hasa vijijini na sehemu ambazo mwanamume anafanya kazi (ameajiriwa) na mwanamke ni mama wa nyumbani (anayejishughulisha na kazi zingine) na pia limeegemea zaidi katika familia za kikristo.

Naamini maoni ninayopata kutokana na hilo somo basi nitayafanyia kazi na kama inawezekana siku nyingine nitoe kitabu cha Ndoa na nyumbaHata hivyo nashukuru sana kwa kueneza ujumbe kwa watu wote ili wajue ndoa ni nini hilo nashukuru.

Kwa sasa nipo Canada kwa ajili ya shule niemfika hapa tarehe 1 Sept 2007 na naamini tutazidi kuwasiliana na pia nimsomaji wa blog yako kwa muda mrefu.

Asante sana kwa kazi njema ya kuelimisha jamii:

--
Lazarus P. Mbilinyi

3 comments:

Anonymous said...

Nadhani kama utaandika kitabu itabidi ukifanyie utafiti mzuri vinginevyo kitakosa wasomaji na kukumbana na upinzani hasa .Changamoto ulizopata humu ni sehemu ndogo tu.Zingine tumeona tunyamaze maana blogu nazo siku hizi mtu kuchapisha maoni mpaka apende aseme sawa mmiliki wa blogu.

Anonymous said...

Nimepata muda kidogo kupitia ulichoandika Mbilinyi.Nadhani mtizamo ulionao na ulioutumia si "Mtizamo Kikiristo" hasa ,bali mtizamo ulioathirika na "mtizamo pagani"

Ieleweke kuwa Mama wa nyumbani kisheria ni mfanyakazi kama wafanyakazi wengine.Yeye anaangukia kwenye sekta ya DOMESTIC WORKERS.Na hata Tanzania mama wa nyumbani anaangukia kwenye kundi hilo na kuna hata vyama vya wafanyakazi wa majumbani vilivyosajiliwa kisheria.

Mama kama Domestic Worker akiamka asubuhi ana kazi nyingi za ndani na nje.Kituo chake cha kazi si wakati wote kiko ndani bali huwa nje pia.Mfano anahitajika kwenda kulima,kuchota maji,kutafuta kuni,kwenda kutafuta mboga,kupeleka watoto kliniki na kadhalika nje ya nyumba.

Kama hoja yako ya kuthibitisha "ufanyakazi" ni "kwenda kufanya kazi nje ya nyumba" na mwanamke pia yumo katika kundi hilo.Hivyo ni mfanyakazi kama wewe na kazi zake ziko hivyo kila siku kama za mwajiriwa zilivyo hivyo kila siku.

Wote huhitajiwa kuanza kazi asubuhi awe mwanaume au mama wa nyumbani.

Na mwanamke huyo wa kijijini akiamka kuwahi hayo majukumu yake huwa haamki tu na kwenda na matongotongo machoni bali huwa anaoga au kunawa sawa na huyo mwanaume aliyeajiriwa kama Mwalimu au Nani hapo kijijini.

Suala la kusema mwanamke ndiye anatakiwa amwandalie mume huyo anayeitwa mfanyakazi maji ya kuoga asubuhi nadhani linahitaji marekebisho.Ni Kwa nini mwanaume naye asimwandalie mkewe maji hata kama ya kupigia mswaki tu mkewe ambaye ni mfanyakazi mwenzie anayewahi shambani au kufagia nyumba asubuhi,kudeki au kuogesha watoto au kuwaandalia kifungua kinywa asubuhi? Kwa nini iwe ni wajibu wa Mke tu wakati wote kuandaa hayo maji ya kuoga wakati wote wawili mume na mke wanaelekea kwenye kazi hiyo asubuhi?

Kwangu mimi naona kwa mtizamo wa Kikristo na dini zingine zote labda kasoro ya kwako Mbilinyi mwanaume na mwanamke inabidi wasaidiane kuandaliana hayo maji .Maana wote ni wafanyakazi na wote kazi zao zinaanza asubuhi.Za mwanaume zinaanza subuhi na za mwanamke zinaanza asubuhi.Ikiwezekana hata kuwe na ratiba.Hata kama hakuna ratiba basi si vibaya kila mtu akajiandalia maji yake wakati mwingine akiendelea naye kujiandaa ili awahi majukumu mengine ili wasipoteze muda sana After all time is money.

Nadhani Mbilinyi una "mtazamo pagani" wa kuona mwanaume ndiye hasa mfanyakazi na wengine wote akiwemo mke na watoto ni vibarua wa "mfalme mwanaume" na hili tatizo haliko kwa wanaume wa vijijini tu liko kwa wanaume wengi wa Kitanzania wawe wakulima,wafanyabiashara au wafanyakazi,wachungaji au masheikh wawe mjini,kijijini au kwenye nchi zilizoendelea kama Kanada.Hawabadiliki "mtizamo pagani wao" inapokuja masuala ya wake.

Nadhani kabla ya hicho kitabu kukitoa itabidi utuletee tukiangalie vizuri isije kuwa kimeandikwa kwa pambio za kikiristo lakini kimejaa mitizamo ya kipagani.

koloboi@yahoo.com

Aginiwe Mbilinyi said...

Hahaaa ivi huku mliishia wapi hizi mambo nimekumbuka nilipo kuwa skuli