Thursday, September 06, 2007

Mawaidha kuhusu Ndoa - Sehemu ya Pili


SIFA ZA MWANAMKE (SIFA NJEMA)

1. Awe mwema - Mith 12:4, 31:10 -30
2. Mwenye hekima - Mith 14:1 16:5,24
3. Mwenye adabu - Mith 19:14, 11:16a
4. Mwenye busara - Mith 19:14
5. Awe mkarimu - Mith 22:9
6. Msafi (mwili na nyumba)
7. Mpole - Mith 15:1
8. Mwenye huruma
9. Mdadisi
10. Mvumilivu
11. Mcheshi (kiasi)Yampasa mke aanze siku kwa kauli nzuri hata kama anaumwa:-
- Amusalimie mume
- Amwage mumewe akimtakia kazi njema baada ya kumuandalia
(a) Maji ya kuoga
(b) Kifungua kinywa
(c) Nguo za kuvaa siku hiyo

Mume atokapo kazini:-
(a) Mkaribishe kwa tabasamu, mkaribishe kwa furaha.
(b) Mpigipige mgongoni
(c) Vaa nguo nzuri (mwanaume hupenda anachoona) macho huvutiwa kwa kuona
(d) Waeleze watoto wako unavyompenda baba yao ( watoto nao watawapenda wote)
(e) Kila mmoja wenu ajue kile anachopenda ua anachotaka

ILI KUMHESHIMU MUME
 1. Muombee kila siku - Yeye alivyo hekima, busara, ulinzi, baraka, ujuzi, kuelewa, kiroho, mafanikio, kushinda majaribu nk - angalia na tarajia majibu ya maombi - Mshukuru Mungu kwa kazi anayofanya kwa familia yako - Mshukuru Mungu kwa ajili ya Mume wako- ombea mtazamo wako.
 2. Kumbuka Mungu amemuweka mume wako kuwa kiongozi wa nyumba yako pamoja na wewe.
 3. Angalia sifa za mumeo na uzikubali na ongeza mara kwa mara
 4. Mwambie mumeo ni namna gani unamfurahia na kumpenda
 5. Usitoe sifa zake mbaya mbele za watu au kubisha
 6. Mtie moyo na kuwa msaaada wakati wa jambo gumuJihadhari na jinsi unavyomuuliza maswali
 7. Changamkia pale anapoonesha upendo
 8. Fikiria mambo mazuri juu ya mumeo
 9. Thamini vitu anavyovipenda na asivyovipenda Mith 12:4

KAWAIDA MWANAMKE
 1. Usitegemee starehe nyingi kama zile ulizokuwa unapata kwa wazazi wako au ndugu zako
 2. Utakuwa na juhudi katika kujenga nyumba ya mume wako uliye naye. Mith 14: 1 Kila mwanamke aliye na heshima.......................
 3. Hutakuwa mgomvi na mchokozi wala kumpiga mumeo kwa mwiko Mith 21:19
 4. Utampa mume wako haki yake 1Kor 7:3-5
 5. Thamani ya mumeo ni zaidi ya wanaume wote. Ez 16:32
 6. Umtii mumeo kwa Roho ya upole na unyenyekevu 1Pet 3:1-4
 7. Usimuruhusu mtu yeyote atambue kwamba unao wakati mgumu ( siri za ndani zisitoke nje) 1pet 5:9
 8. Utahaakikisha macho yako yanamwangalia mumeo wakati amevaa kabla ya kutoka kwenda kazini au kutembea
 9. Utajitoa na kumtii mumeo kwa moyo wote na kumruhusu kuwa kichwa cha nyumba Kol 3:18, 1pet 3:6, Ef 5: 33
 10. Utahakikisha mumeo ni bora kuliko watu wengine Fil 2:3, Wimb 5: 9-16
 11. Mwanaume ni dereva wa gari la ndoa na mwanamke anaweza akashauri na kupednekeza njia ya kupita na siyo kunyang'anya usukani

9. SIFA ZA MWANAUME
1. Mpole
2. Asiwe mwepesi wa hasira
3. Mcheshi
4. Anayeshaurika
5. Anayewajali watu wa nyumbani mwake (mahitaji)
6. Aliye na shukurani na kusifu (kwa lolote jema alilolitenda mkewe)
7. Anayeaga aondokapo kwenda matembezini au kazini au popote.

10. WAJIBU WA WA MUME KWA MKEWE

1. KUPENDA - kwa kiwango cha Kristo kwa kanisa Efe 5:25 matatizo mengi hutokea kwa sababu watu hawajui maana na jinsi ya kupenda kupenda ni matendo (action) siyo kujisikia au kuhisi ni kufanya vitu vizuri kama vile kutoa, kutabasamu, kusamehe nk Yohana 3:16
2. KIONGOZI (KICHWA) MTAWALA - Mume ni kichwa cha mke Efe 5:23 Naye atakutawala Mwanz 3:16c Amri hii hairekebiki kwa kelele za UWT kudai usawa ila utekelezapo maagizo ya Kristo amri amri ya kutawaliwa inakufa
3. MLINZI WA MKEWE - Kama chombo kisicho na nguvu, 1pet 3:7, Naye ni mwokozi wa mwili Efes 5:23 Mke hujiona salama awapo na mumewe Isay 4:1 Hivyo mume mlinde mkeo na maadui wa ndani na nje kama vile baba na mama, mashemeji/mawifi na marafik
4. KUTUNZA FAMILIA. Kuhakiki familia inapata chakula cha kutosha, malazi, mavazi na elimu kwa watoto Mwanzo 3: 17
5. KUMPAMBA MKEWE - mume sharti ampambe mkewe apendeze ili aweze kuvutia (amununulie vipodozi, nguo nk)

KAWAIDA MWANAUME:

 1. Utamheshimu mke wako kama mrithi pamoja na wewe katika neema ya uzima katika Kristo Yesu. 1Pet 3:7
 2. Mke wako ni mtu wa kwanza kwako siyo ndugu zako wala rafiki zako Mwanzo 2: 24 Mtaambatana na kuwa mwili mmoja
 3. Mara kwa mara utamwambia mke wako alivyo wa muhimu na thamani kwako Fil 2:3 , Mith 31: 10,11
 4. Utaendelea kumpenda kwa upendo ule wa kwanza wa wakati unampata. Wimb 5: m10 - 16
 5. Utakuwa kiongozi wa kusimamia nidhamu ya nyumba yako ukisaidiwa na mke wako. Efes 6:4
 6. Utakumbuka kutekeleza au kutimiza vile vitu vidogo ambavyo ulimwahidi mke wako kwamba utafanya Math 5: 37
 7. Macho yako yataelekea kwa mke wako tu na sivinginevyo. Mith 5: 15-20, Ayub 31:1, Yer 5:8
 8. Utafanya juhudi kusikiliza yale yaliyosemwa na mke wako. Mwanz 21:12
 9. Utambusu kila siku asubuhi kwa upendo. Wimb 8:1
 10. Hutakuwa mchungu likija swala la fedha. Est 5:3

12. WAJIBU WA MKE KWA MUMEWE KUTII - Kumtii mume kama kumtii kristo Bwana Yesu efe 5:22 watu huchanganya sana neon kutii na kuheshimu. Kutii kunakosemwa hapa ni kuwa endapo wawili mume na mke mmeshindwa kufikia uamuzi wa pamoja, basi,basi mke atatii uamuzi wa mumewe kama vile wamekubaliana awali

KULEA WATOTO (FAMILIA)
(a) Kuhakikisha afya ya mumeo na watoto
(b) Kuhakikisha kuwa chakula kinaliwa kwa wakati na kizuri
(c) Kuhakikisha usafi wa malazi, mavazi na miili yao
(d) Kufundisha watoto maneno ya Mungu
(e) Kuchunguza nyendo na tabia za watoto na mumeo na kuchukua tahadhari mapema.

KUMSHAURI MUMEO
Mke mwenye busara ni mshauri mwema kwa mumewe. Hatatoa ushauri wa kuleta maangamizi. Ushauri unafaa lakini ushauri mwingine upimwe kabla ya kufanyia kazi. Ona mashauri mabaya ya wanawake kwa waume zao

(f) Hawa kwa Adamu - Mwanza 3:17 (kula tunda)
(g) Sara kwa Ibrahimu - Mwanzo 16: 1-3 kulala na mjakazi (tabu ya mashariki ya kati)
(h) Yezebeli kwa mfalme Ahabu - 1Falm 21:22/2Falm 9:10
(i) Zereshi kwa Hamani mumewe kwa habari ya Mordekai Esta 5:14, 7:9-10
(j) Mkewe Ayubu kwa ayubu mumewe - Ayubu aliukataa ushauri wa mkewe. Ayubu 2:9

13. ADUI WA NDOA NI:-UTAJIRI - Tajiri hupendwa na wasichana na pia huwa na tamaa ya kutafuta fedha kiasi cha kukosa muda na mkewe

UMASKINI
- kazi ya kutafuta lishe ni ya baba, hivyo hushughulika sana na kujikuta amekuwa baba zaidi kuliko kuwa mume

MADARAKA - madaraka ya ofisini huyaleta hadi nyumbanini chukuzo kwa mume/mke. Maafisa hawana muda na wake zao kwa sababu ya makongamano/semina/ziara mbalimbali.
- Hivyo wake zao wengi hutumia madereva kukidhi haja zao za kimwili
- Mke ambaye ni ofisa humwachia house girl kazi za kupika, kufagia chumbani, kupeleka maji bafuni na hata kutandika kitanda, hivyo kusababisha mke kupinduliwa na house girl.

MAMBO YANAYOWAKERA WAKE ZETU
 1. Wababa wenye madaraka kuyapeleka madaraka nyumbani
 2. Wake kuwajibika na mambo ya nyumbani kwa vile wana mishahara minono
 3. Wababa kutotenga muda wa kutosha kukaa na wake zao ili kuongea yanayowahusu
 4. Mume kumwachia mke kulea watoto hasa wakati wa usiku
 5. Mume kutomtia moyo mke wakati wa ujauzito
 6. Mume kumchanganya mama na watoto wa kike wanapokosa
 7. Mume kutokuwa na maandalizi mazuri wakati wa kukutana kimwili na mkeo
 8. Mume kujijari mwenyeweMume kusaidia ndugu zake bila mke wake kujua
 9. Mume kubagua watoto
 10. Mume kuwa na upendo na ukaribu au kucheka na binti waishio nao huku yupo mke wake
 11. Mume kutomshirikisha mkewe katika huduma yake ya ili aweze kumwombeaKutoonesha shukrani wala kutokuwa na msamaha
 12. Mume kutomtazama mkeo usoni mkiwa chumban
 13. iMume kuongea kiutani na wanawake wengine mkeo akiwa hayupo.

8 comments:

Anonymous said...

Da Chemi hii article nzuri sana, hata hivyo ni rahisi sana kuyaongelea au kuwa na mjadala na haya mambo unless uko kwenye ndoa, yaani uingie ndani ya ndoa yenyewe ndio utaweza kuelewa.
Wanandoa si kwamba wanaamua kutozingatia maadili haya mema, isipokuwa hali ya maisha sasa hivi ni ngumu mno na mara nyingi tunafocuss kwenye stressess za maisha yetu zaidi na kujisahau, believe me or not it is very very tough being in a marriage na kama kuna mihangaiko kibao ya maisha, mimi binafsi naweza kusema kuwa key word hapa ni UVUMILIVU, wale wanaoona 50th annivessaries zao ni kwa sababu ni WAVUMILIVU kwenye ndoa zao, kuna wakati mgumu na kuna wakati wa raha. Ila asante kwa article hii, itatukumbusha sisi wenye ndoa our resposibilities!!!

Anonymous said...

Haya yote rahisi sana kama bado mko honeymoon. Ingia kwenye msondo wenyewe wa ndoa ndio utaona. Majukumu, kazi, watoto na maisha kwa ujumla yote haya yanasahaulika kirahisi, Ndoa ndoana bwana asikuambie mtu, waache wenye ndoa wenyewe waseme!!

Anonymous said...

Inatisha sana niliyonukuu sentensi hapa inaonyesha huyo mke ni wa mtu maskini.

Eti inasema "Amwage mumewe akimtakia kazi njema baada ya kumuandalia
Maji ya kuoga"

Bafu siku hizi ni Self Contained zinatoa maji baridi na moto na huhitaji mtu wa kumwandalia maji mtu mwingine.

Wake wa watu maskini wana shida sana.

Mimi ndiyo maana Chemi nilikataa kuolewa na mtu maskini kukataa mambo kama hayo.

September 07, 2007 2:57 AM

Anonymous said...

Da Chemi mbona huyo Bibi harusi kwenye picha ana macho kama shetani?

Anonymous said...

Tafadhali sana anony September 07, 2007 2:57 AM, chunga kauli zako! Kama wewe umebahatika mume tajiri shukuru Mungu, lakini tambua kwamba huyo huyo Mumeo leo ni tajiri (Mabafu self contained) kesho atakuwa ni masikini, maji ya kwenda kuchota kwa jirani! Shukuru Mungu kwa unachokipata leo, usiwakandie wenzio wasiokuwa navyo. Maisha sio kila mtu awe tajiri! Please heshimu hali ya wenzio, kwani HUJAFA HUJAUMBIKA!!!!!

Anonymous said...

Annonymous

Bibi Harusi hana macho kama shetani ila inavyoelekea amevaa shela lenye material kama mchelemchele yaani "shimmering", kama vile kitambaa cha Oganza kama unakijua mwanawani na mambo ya flash za camera tena ndio zikammuvuzisha macho yake.

Anonymous said...

da chemi mi nashukuru sana kwa mtoa mada naona ni mtu wa Mungu kweli kweli, lakini napenda kusema kwamba utajiri ,umaskini wote mtaishi maisha ya raha sana kama hiyo ndoa itamtegema Mungu kama ndio muweza kwa kila kitu. mimi nimeolewa na mume wangu tuna maisha mazuri sana tu lakini sie tumeamua kuwa kila tunachofanya Yesu ndo no 1 hivyo ni full enjoyment, napenda kuwatia moyo wengine kwamba ndoa inalindwa kwa maombi tu. jaribuni hiyo muone mkono wa bwana kweli kweli ni vicheko wakat wote. no vita wala ugomvi.

Ms GB

Anonymous said...

napinga hiyo kauli ya kusema ndoa ni ndoano kama wengine wasemavyo,ndoa ni takatifu mimi ni mkirsto nilieokoka ila napenda kusema kwamba wakina mama na wakina baba si kweli ndoa ndoano,biblia inasema ndoa ni takatifu sijaona mahali walipoandika ndoano kwenye biblia hiyo ni ibilisi anawaingia watu kusema ndoano, yani unakuta mtu anaingia kwenye ndoa na watu wanamwambia uingie uyaone, usikubali mtu akutabirie mabaya hata siku moja kataa hapo hapo hata kama ni kimoyo moyo tu. alaf kuna sehemu kwenye biblia inasema utashiba maneno ya kinywa chako,uzima na mauti vipo kwenye ulimi wako, ukitamka ndoano unaharibu kabisa maana siku utakuja kuona hiyo ndoano si umetabiri mwenyewe kwa kinywa chako, jaman ndoa ni paradiso na ni takatifu whether unaishi maisha ya aina gani lkn juu ya yote maombi ni mlinzi tosha. niwape siri moja ukitamka mema siku zote unapata mema, tujifunze kusema mema jamani wandugu

Ms G Bennett