Monday, September 24, 2007

Unapoguswa Gusika


Nimepokea hii shairi kwa E-mail. Ila haisema mtunzi ni nani.

Unapoguswa Gusika

Mtunzi?

Wengine hupenda chungulia, miguso isowahusu,
Na macho huyatoa kama mijusi, waonapo miguso,
Na sio tabia nzuri, kuchungulia yasowahusu,
Ni sharia ya mguso, unapoguswa gusika!!


Wawili wapendanapo, si ajabu kugusana,
Popote pale walipo, wazee hata vijana,
Ije mvua na upepo, mikono watashikana,
Fumbo kubwa la mguso, unapoguswa gusika!!


Wengine wanashituka, pale wao wanaguswa,
Pembeni wakaja ruka, kama wamekoswa koswa,
Wakabakia kucheka, hawajui la kupaswa,
Ni utamu wa mguso, unapoguswa gusika!!


Wapo wapenda mgongo, wakakigusa kiuno,
Kwa mbwembwe na kwa maringo, wakikenua na meno,
Wamejawa na usongo, yamewatoka maneno,
Mtetemo wa mguso, unapoguswa gusika!!


Wapo wapenda kifua, wakaligusa na tumbo,
Lengo lao twalijua, wanaamsha majambo,
Haraka wakipumua, utadhania mgambo,
Ladha kubwa ya mguso, unapoguswa gusika!!


Wapo wependa kugusa, visoguswa hadharani,
Wakayafanya makosa, wakajaitwa wahuni,
Mkitaka kuvigusa, mjifunguie chumbani,
Ni fahari ya mguso, unapoguswa gusika!!


Uguse aliye wako, karibu mshikilie,
U mguse atakako, asije akachukie,
Wa mwenzako huyo mwiko, tamaa usiwakie
Siri kubwa ya mguso, unapoguswa gusika!!


Ninawasihi wenzangu, msiogope kugusa,
Ni kipaji chake Mungu, ukiguswa nawe gusa,
Ukaondoa machungu, na machozi kupangusa,
Ni uhondo wa mguso, unapoguswa gusika!!

2 comments:

Anonymous said...

Mhh nahisi usiku umeingia maana haya mambo ya kugusa,sio umri wangu.

Haya dada Chemi Usije sema sijakuaga.Usiku mwema dada kesho eehee.

Ngoja nikaguse usingizi maana naisi na wenyewe umenigusa.

Alamsiki

Anonymous said...

DADA CHEM
TAARIFA NILIZOPATA ZISIZO RASMI MH JUMA KAPUYA WAZIRI WA ULINZI AMEPATA AJALI HUKO TABORA.

PLZ FUATILIA UTUPATIE TAARIFA ZAIDI.TAARIFA ZINADAI KAUMIA SEHEMU YA KICHWA.

NAMUOMBEA APATE KUPONA HARAKA.AMEN