Wednesday, September 26, 2007

Ukweli kuhusu Sara aka Venus Hottentot

Mmewahi kusikia habari ya Saartje (Sara) Baartman, kutoka Afrika Kusini. Sara alifariki dunia mwaka 1815 nchini Ufaransa, lakini alizikwa mwaka 2002 kwao Afrika Kusini.

Alivyofariki mwaka 1815 akiwa na umri wa miaka 26, wanasayansi wa huko waligombania maiti yake. Walikata viungo vyake vya siri na kuviweka kwenye chupa za kuzihifadhi na kuwekewa kwenye nyumba ya maonyesha. Walisema eti mashavu ya huko mahala ni marefu.

Kisa cha kutokuzikwa miaka 187 ni kuwa Sara ndiye yule ambaye wazungu walikuwa wanamwita, 'Venus Hottentot'. Sara alikuwa na matako makubwa kweli kweli na wazungu walikuwa wanamshangaa. Kumbe kwa kabila lake ndo wanawake walivyo. (picha ya juu ni wax mold ya maiti yake, Aliwekwa kwenye circus na kutembezwa Ulaya kama mnyama kwenye zoo!

Wakati hayuko zoo walifanya ngono naye kwa ajili ya kutoka 'kuonja' maajabu yake!

Sara alichukuliwa ktoka kwao Afrika Kusini akiwa na miaka 21 kam mtumwa. Alipelekwa kwanza Uingereza na daktari fulani. Alifariki kwa ugonjwa na si ajbu ilikuwa ugonjwa wa zinaa!

Unaweza kusoma habari zake kwenye vitabu vilivyoandikwa kuhusu watu wa ajabu duniani kama yule Elephant Man, ambaye alikuwa na ugonjwa mbaya wa ngozi na mifupa.

Kuna michezo ya kuigiza kuhusu maisha ya Sara. Naona muda umefika watengeneze sinema kuhusu maisha yake na jinsi alivyoteswa na wazungu.

Mungu apumzishe roho yake mahali pema mbinguni. Amen.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.heretical.com/miscella/baker4.html

http://www.salon.com/books/review/2007/01/09/holmes/index_np.html


http://www.southafrica.info/ess_info/sa_glance/history/saartjie.htm

http://freaks.monstrous.com/the_hottentot_venus.htm

2 comments:

Anonymous said...

yaani Chemi umenifurahisha pale na wewe ulipojiweka kwenye watu wa matako makubwa na unajivunia nayo--Cheers

Anonymous said...

Okay ile sanamu ni kama mwili wa Sara ulivyokuwa. Sasa mbona sioni kama ana matako makubwa ajabu. Ama kweli wazungu wamezoea matako chapati.