Tuesday, November 10, 2009

Ilela, Manda

Kijiji waliokaa mabibi na mababu zangu ni Ilela, Manda. Sehemu kubwa ya hicho kijiji kiko chini ya maji ya Ziwa Nyasa. Kijiji nilichojua nikiwa mtoto iko chini ya maji unayaoona pichani. Yaani hii beach unayoona ndo ilikuwa milima ya enzi zile. Nilikaa kwenye kiti nje ya tulipofikia na kutazama yale maji na kutoa machozi. Kijiji kilimezwa mwaka 1974. Natamani marine archeologists waende huko wachunguze hiyo eneo. Kumbe kuna Tsunami Afrika, tena kwenye ziwa! Na tulipokuwa kwenye meli kuelekea kijijini nilionja hasira ya Ziwa Nyasa, mawimbi makali kama bahari!

Marehemu bibi yangu, Gandula, kabla ya kufariki alisimulia hivi.... Walikuwa kijijini wanafanya shughuli zao. Ghafla wakaona zinga la wimbi la inakuja, walikimbia mlimani. Kijiji karibu chote kikamezwa. Maajabu hakuna aliyekufa wakati huo. Nyumba za wanavijiji, nyumba za mkoloni, miti, mibuyu, shule, makaburi, kila kitu kilimezwa na ziwa!

Wanasema kuna Mzee fulani, Mzee Kwiyanja, aliwaambia miaka mingi, hameni hapo Ilela, maana kijiji kitamezwa. Bibi alisema kuwa walikuwa wanamcheka yule Mzee na kumwona mwendawazimu. Yeye alihama na kujenga mlimani. Baada ya tukio wakamwona yule mzee kama mtume (prophet).

Kuna sehemu ya Ilela imebaki. Na nilipoenda kutembea nilikutana na wanavijiji wengi walionikumbuka hasa kwa ajili ya utundu wangu nikiwa mdogo. Picha zaidi za Ilela zinakuja.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Umenikumbusha mbali sana kutoka Manda kwenda Lundo sijui ni umbali gani maana huko ndo nilikozaliwa mimi. Ahsante kwa hadithi ya bibi na bahati mbaya kumbukumbu nyingine zimepotea. Taswira nzuri sana. Nasubiri picha nyingine.

John Mwaipopo said...

mandhari nzuri ya ziwa hii. beautiful beach, this one.