Tuesday, November 24, 2009

Ubaguzi Mpaka kwenye Poster!

Wadau, hivi kribuni ilitoka sinema, Couples Retreat.

Walianza kuionyesha Marekani halafu walianza kuionyesha nchi za Ulaya. Producers (Universal Studios) waliamua kuondoa weusi katika bango la sinema. Hebu cheki bango la Marekani (picha ya juu), na bango la Ulaya (Picha ya chini). Waliona wakiweka weusi kwenye bango watu hawataenda kuoiona huko Ulaya nini? Baada ya zozo kubwa hapa Marekani waliamua kutumia ile bango la awali!Kwa habari zaidi BOYA HAPA:

9 comments:

Candy1 said...

niliona huku UK...na mbaya zaidi sikuona hiyo poster yenye couple weusi...weird

Anonymous said...

Ubaguzi upo tena ni wazi wazi.

Anonymous said...

So, Universal Studios is embarassed about having black people in their films?

Anonymous said...

Hata haya hawana! DUH!

Anonymous said...

Dada mimi ningependa "mdaharo" na wewe. Mimi naishi hapa New York, nasoma Columbia University. Naona kila mara kwa mara unagusia "Ubaguzi" nini maana ya Racism? wakati nafanya masters niliandika paper juu ya racism, maybe naweza kukutumia kama utapenda, nadhani sometimes hatupo sahihi, mbona kwenye BET kuna movies nyingine ambazo hazina wazungu, je huo pia ni ubaguzi?

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 10:04pm, Sinema ya weusi ambayo haina wazungu si ubaguzi. Pia sinema ya kizungu ambayo haina weusi si ubaguzi. Inakuwa ubaguzi wakizungumzia kudhalilisha weusi au wazungu kupakwa rangi wanaonekane weusi badala ya kutumia actors weusi (na ziko nyingi). Universal Studios wamefanya ubaguzi ya wazi kwa kuondoa weusi waliokuwa kwenye poster ya awali. Holla at chemiche3@yahoo.com.

Anonymous said...

Hivi watu weusi tutaacha kulia lia ubaguzi lini?kama watu wabaguzi na wewe wabague.Tunaona ni ubaguzi sababu tunawapa nguvu hiyo.kama mtu hataki kushare a piece of the pie,go get/make your own pie.Stop acting like you can't live without their pie.

Anonymous said...

Nadhani kama Universal wangetumia hiyo isiyo na weusi toka mwanzo kusingekuwa na maneno. Walivyofanya kweli ni kitendo cha kibaguzi.

Anonymous said...

hata huku Dubai nimeona wametumia hiyo poster ya pili isiyo na weusi lakini mimi sioni kama kuna ubaguzi hapo huwezi jua sababu ya wao kufanya hivyo na hata hivo ukitizama hiyo poster ya pili ni simple na inapendeza hiyo ya kwanza inaonekana mazagazaga mengi tu labda ndiyo sababu wakaibadilisha, siyo kila kitu tunakipigia makelele jamani, kuna mengi muhimu na tuyavalie njuga!
nawasilisha...