Monday, November 09, 2009

Malaria!

Wadau, nimerudi Boston. Siku ya jumamosi nilikuwa sijisikii vizuri nikiwa nyumbani kwa wazazi wangu pale Tangi Bovu. Ilikuwa nikitembea kidogo nachoka. Mama yangu kasema niende Massana Hospital kupima damu. Nilienda jumapili asubuhi kupima. Kweli nilikutwa na Malaria! Duh! Nikapewa tiba. na kuondoka mchana huo huo. Yaani nadhani niliambukiwa siku ya kwanza nilivyokuwa Dar.

Chandarua ya dawa, dawa ya kuzuia mbu ya kupaka, RUNGU, Anti-malarials (malarone) hazikuyfanya kazi!

Hata hivyo nategemea kurudi Tanzania mwakani na kukaa muda mrefu zaidi!

4 comments:

Anonymous said...

Pole sana Da Chemi. Ndo Tanzania hiyo. Homa! Homa! Homa!

Anonymous said...

Pole sana Da Chemi. Tunakuombea upate nafuu mapema ili utuhabarishe yaliyojiri huko nyumbani.

Anonymous said...

Pole sana kwa kupatwa na malaria.Pia pole kwa safari yako ya kufika hadi kijijini Manda.Umenikoga sana kwa kutembelea mahali ulikotokea.Unahitaji kupongezwa sana kwani wengi wanaoishi huku ughaibuni wakienda bongo huishia hapo Dar na kudharau kijijini walikokulia kuliko na bibi na babu zao.Nakutakia maandalizi mema ya safari ya mwaka kesho.Mungu akubariki sasa dada Chem

Mdau wa Minnesota

Yasinta Ngonyani said...

Pole sana dada. Na nakuonea wivu na nakusifu kwa kusema mwakani utarudi tena TZ na kukaa huko muda mrefu zaidi. Safi sana dada.