Friday, November 27, 2009

Mzee wa miaka 86 Ambaka Msichana mdogo Dar!

Duniani kuna mambo! Huko Kinyerezi, Dar es Salaam, Mzee mwenye miaka 86 kambaka msichana mwenye miaka mitano! KHAA! Yaani alishindwa kumpata hata malaya wa kumridisha! Na wanasema kuwa alimpenya huyo mtoto! Nadhani huyo mzee atafia jela hivi karibuni! DUH!

Kama miaka mitano iliyopita hapa Boston, kuna Babu mwenye miaka 83 alimtia mimba msichana mwenye miaka 9! Hapa watoto wengine wana vunja ungo mapema. Yule binti alikuwa anakwenda na kikundi fulani cha watoto kwenye nyumba za wazee kuwatembelea na kuwa marafiki na wazee. Si mnajua nyumba za wazee hapa ni nyumba za kusibiri kifo. Tulishangaa kusikia bado vinaongelea na umri huo.

*******************************************************************

Kutoka ippmedia.comhttp://www.ippmedia.com

Elderly man (86) charged with raping kid (5)
By Jacqueline Mosha
27th November 2009

An elderly man, Omari Kitambo (86), was on Thursday arraigned in the Ilala District Court charged with raping a five-year-old girl (name withheld).

The accused, a resident of Kinyerezi on the outskirts of Dar es Salaam, appeared before Resident Magistrate Joyce Minde.

According to Asma Shemweta who read the charge sheet, the accused had carnal knowledge of the girl.

The accused pleaded not guilty to the charges and was remanded in custody after failing to meet bail conditions.

3 comments:

Anonymous said...

Hii kali! Mzee wa umri hiyo kubaka! DUH! Yaani alishindwa kupata mwanamke hata kibibi kizee mwenzake?

Anonymous said...

Miaka 86! Huyo ni wakuondoka wakati wowote lakini keshapat raha yake kwa huyo mtoto. Mungu ampe nguvu huyu mtoto.

Matangalu said...

huyu mzee anatakiwa aadhibiwe vikali bila ya kuangalia umri wake. Inawezekana huyu atakuwa amebaka watu wengine wengi tuu isipokuwa arubaini zake zimemkutia uzeeni. Wanawake wengi sana hubakwa, na kubakwa mara nyingi unabakwa na ndugu wa karibu. Hii husababisha wanawake kuogopa kutoka mbele na kusema kwamba "fulani amenibaka". Mbakaji huendelea na tabia yake ya ubakaji kwa sababu anajua kwamba wanawake huwa hawasemi wanapobakwa kwa kuogopa aibu na fedheha ya kubakwa.

Kumbukeni kina dada; kama kuna yoyote kani yenu amewahi kubakwa na mtu mmoja, basi uwezekano mkubwa ni kwamba huyo mtu ni ndugu yako ambaye ulimuamini na kukaa naye katika mazingira ya hatari.

Kama umewahi kubakwa na kundi la watu; basi mara nyingi watu hawa huwa siyo ndugu zako na wanakuwa wamechukua nafasi kwa sababu labda umelewa, au umejiweka katika mazingira ya hatari.

Nini cha kufanya baada ya kubakwa?

Kwanza, akili ya kawaida inakutuma kujisafisha, labda kwa kuoga au kunawa. Hili ni kosa kubwa sana wanawake hufanya. Ukibakwa usijisafishe, kwa sababu kwa kufanya hivyo unaondoa ushahidi wote wa vinasaba vya wabakaji.
(Do not wash away their DNA)

Pili, usione aibu na wataarifu polisi haraka iwezekanavyo. Usiporipoti polisi basi unakuwa umempa ushindi mbakaji/wabakaji na wataenda kumbaka mtu mwingine.

Kina dada, hakikisheni ukibakwa mbakaji lazima aadhibiwe.

Matangalu