Friday, November 13, 2009

Mikumi Kukavu!

Nilidhani nitaona wanyama wengi wakati basi niliyopanda kwenda Kyela inapita katika mbuga ya wanyama, Mikumi. (Mikumi National Park) mkoani Morogoro. Naona moto uliteketekeza mbuga hiyo. Ilikuwa kavu, mito imekauka kabisa, yaaani ilisikitisha kabisa kupita pale Mikumi. Ila niliweza kuona twiga watatu, punda milia mmoja na swala kama ishirini.Athari za moto
MAIN GATE MIKUMI

5 comments:

Anonymous said...

Kuna ukame na njaa Tanzania!

Bennet said...

Kwa sasa hivi sehemu kubwa ya nchi yetu hasa ukanda wa pwani umekumbwa na ukame, sehemu kama Tanga mvua zilinyesha kidogo watu wakapanda, lakini sasa hivi jua kama kawa na mahindi yamenyauka shambani, maji ni tabu kama uko jangwani

Anonymous said...

Chemi

Jambo usilojua uwe unauliza kwanza. Huo moto sio wa bahati mbaya au ukame.

Wanachoma moto ili kuwazuia wanayama waliokuwa wanafuata malisho ya nyasi kando ya barabara na kuvuka wasifanye hivyo tena.

Sababu ni kuwaokoa na kugongwa na magari, at the same time wanawazuia wapenda dezo kama wewe badala ya kwenda kulipia ili uone wanyama unataka uwaone bure ukiwa kwenye basi

Chemi Che-Mponda said...

Mdau wa 3:52am, asante kwa maoni. Ila nilishaingia pale Mikumi mara kadhaa na kulala Lodge wakati bado iko wazi. Baada ya kuona ukame, moto pale Mikumi na uhaba wa wanyama, kweli mtu atakuwa na hamu ya kulipa na kuingia. Nilisikia kuna wazungu walilipa na kuingia pale Mikumi na walidai warudishiwe hela yao kwa vile waliona kama wamepunjwa kutokana na uhaba wa wanyama. Mito mle imekauka na ku-crack kabisa. Tuombe mvua ije.

Anonymous said...

Ni kweli kuna ukame. Na huko Mikumi wanyama wameanza kufa shauri ya kukosa maji!