Thursday, November 12, 2009

Bandari ya Kyela

Meli MV Songea (Meli Kubwa)

Wadau, Ziwa Nyasa ni kubwa mno. Ni kama bahari. Ina mawimbi makali kama bahari. Nilitoka Dar es Salaam na basi, hadi Kyela. Nililala gesti (Pattaya Centre Hole) na asubuhi tuliondoka kuelekea bandarini. Kuna bandari mbili huko Kyela. Hii bandari tuliyoenda ni nje ya mji wa Kyela. Ukitaka kwenda Lupingu, Manda, Mbamba Bay na sehemu kadhaa unapanda meli hapo. Hiyo Meli inaendeshawa na Tanzania Railways.

Siku tuliyoondoka, Oktoba 29, 2009, ndo meli kubwa MV Songea ilikuwa inarudishwa katika huduma. Walikuwa wanaifanyia matengenezao ya mwisho mwisho. Walisema meli itaondoka saa 7 mchana, lakini iliondoka saa 11 jioni. Swahili Time kweli kweli. La sivyo ingebidi tupande meli ndogo MV Iringa kesho yake.

Muda wote huo wasafiri pale bandarini waliishia kuchomwa na jua kali. Yaani kali kuliko hata Dar es Salaam. Kulikuwa na akina mama na watoto wao wengi tu pale. Kivuli hakuna. Kulikuwa na vimiti, na pia kajumba. Hiyo jumba walisema inafunguliwa tu, kama kuna wasafiri wanaolala pale kungojea meli, mfano inachelewa kuondoka. Ofisi ya kuuza tiketi ni kontena.

Kundi la akina mama waliamua kwenda kupeleka watoto wao kuoga pale kwenye beach. Mimi mwenyewe nilitia miguu kwenye maji ili kupooza ile joto. Ajabu, polisi fulani mwenye cheo ndogo sana alitokea na kuwafukuza wale wakina mama na watoto wao pale kwenye maji. Halafu alikuwa anatukana matusi ya nguoni, ila watu wamsikie huko kavaa magwanda yake. Sijui alijiona mtu mkubwa sana kwa kitendo chake.

Ningeomba serikali waweke angalau kibanda chenye kivuli pale, bandari ili watu wasichomwe na jua.

Kuna akina Mama Ntilie pale, na wanapikaga dagaa safi sana!
Jua lina zama. Ziwa Nyasa imetulia.
Bado tuko Kyela

Chai kwa Mama Ntilie. Ndizi, dagaa na soda.




Vibanda Vya Mama Ntiliel. Nilipata wali/dagaa/maharage safi sana pale kwa shs. 1,200/-.



Bandari ya Kyela

Hao wazungu ni wanafunzi wa udaktari huko Muhimbili. Wanatoka Ujerumani. Walikuwa wanafanya backpacking. Tulisafiri nao kwenye meli, walikuwa wanaenda Mbamba Bay. Mmoja wao aligombezwa kwa kupiga picha ya meli, MV Songea.

9 comments:

son of alaska said...

you have made my day,what more can i ask-cheerio

Anonymous said...

HONGERA DADA CHEMI KWA KAVACTION KAKO KWA KWELI ULIFAIDI SANA , KWA KWELI NYUMBANI NI NYUMBANI TU ANGALIA VILE ULIVYO PENDEZA.
MDAU WAKO MASOUD CANADA

Anonymous said...

mmmmmmmm dada Chemi unaendelea kuniumiza roho yaani umenipeleka kwetu hadi naona wivu maana sijafika huko yapata miaka kumi sasa.Du wewe dada ubarikiwe sana.

Safari yako ya mwakani sitoikosa dada Chemi maana umenotoa kimasomaso hivyo sitochelewa na mimi lazima niingie huko.

Kwa ujumla hongera sana na asante sana kwa kutufikisha home

John Mwaipopo said...

this is too much. mpaka kyela my home! kwa mmliowahi kula dagaa wa ziwa nyasa kuna aina nyingine duniani ya dagaa watamu kama hawa dagaa wa nyasa? i must visit kyela one of these days.

Anonymous said...

Wazungu na kandambili. bab kubwa "common sense accordingly"; Nikivaa mimi kandambili mgambo wa jiji wananikamata, lakini akivaa mzungu poa tuu.

Anonymous said...

Kitambo sijakutia machoni ,Du yaani unazidi kuwa mrembo na afya kwenda mbele,Mambo yaelekea mazuri sana.Danny

Anonymous said...

Yaani ulilala Pattaya, next time tuwasiliane ... mimi asili yangu Manda lakini Kyela ndiyo home; ingawa niko ughaibuni. nitakucheck binafsi, ili next time ukaribie nyumbani pale Kyela.

Anonymous said...

dada za leo kwani umeolewa

zitto kiaratu said...

huyo askari po pote pale duniani anatandikwa tu isipokuwa bongo watu sijui tunaogopa nini? lazima kila mtu atakufa siku yake, na hicho kiaskari naona anaishi kwa pumzi ya mkopo, yo yote anaetesa watoto na wamama anahitaji kuadhibiwa tu!!!!