Monday, November 09, 2009

Mukesh wa Tabora


Wadau waliosoma Tabora Girls/Boys, na kupitia Masange JKT wataelewa hii blog.

Siku ya jumamosi nilikutana na Mukesh aka. Al Wattan wa Tabora. Nilikutana naye kwenye maduka pale Tangi Bovu/Shule unapopanda mabajaji. Niliingia kwenye duka pale kutafuta mahitaji. Nilishangaa kwa nini jamaa hajui bei ya vitu kwenye duka lake. Kaniambia kuwa hilo duka ni la mke wake na anamshikia kwa muda kwani yeye anakaa Tabora. Nikamwambia mbona mimi nilishakaa Tabora. Alisema, kila mtu mjini Tabora anamfahamu fundi wa magari. Ndo kuongea tukakuta kumbe tunajuana siku nyingi, ila mara la mwisho kuonana ni 1984 nilipomaliza Masange JKT. Tukapeana story za enzi zile. Nilimtania, yaani hatukujuana kwa vile tumezeeka!

6 comments:

John Mwaipopo said...

down memory lane nzuri hii.

Mija Shija Sayi said...

Hadi raha...

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mnapendezaaaa!!!

Anonymous said...

Wow, mzee alikuwa anapenda sana wasichana, hasa Uhazili? sasa naona ameanza kuwa babu.

Anonymous said...

Kijana wa pale Ng'ambo kwa Bwana Boga alisoma uyui()

Anonymous said...

mbona unachelewa chukua mchuma huo!uzee ndo ubora wake.Old is gold mama eehn