Sunday, July 07, 2013

Anaomba Ushauri - Ndugu Yake Ameingizwa Kwenye Uzinzi!

 Nimepokea kwa E-Mail:

Na Mdau A.R.

Jamaa yangu mmoja ameajiri na kampuni inayomilikiwa na mme na mke.
mke immediate bosi wa kijana huyu ambaye hata hajaoa
Siku moja akapewa pesa laki moja akimwambia atafute usafiri na maekezo kwa wakutane hoteli fulani kuna kazi anataka wafanye mahali tulivu.
Kijana alijua mambo ya kiofisi, kachukua usafiri hadi kaenda kule hotelini; kufika kamkuta mama akimsubiri mapokezi, akampokea na kumeleka chumbani, kijana na laptop yake hajui hili na lile.
Mama kakaa, kitandani kijana kwenye kochi, mama yule bosi akaanza kusimulia matatizo ya mumewe, kwamba yupo busy na mambo ya biashara ampi tunda.  Kijana pamoja na kwamba hajaoa, akaanza kumpa shule jinsi ya kumfanya mmewe ampe atakacho, kabla ya kijana kumaliza maelezo yake yule mama akamwambia hata hamwelewi anamwambia nini maana anajisikia hamu sana ya kufanya ni muda mrefu.
Yule kijana kwa hofu akasema ngoja nikimbie pale famasi labda kuna dawa za kutuliza hamu nikuchukulie umeze; mama akasema hataki dawa, mara akaingia chooni maana chumba alichokua kilikuwa na choo ndani.
Alipotoka huko alikuja mtu nguo zote kaacha huko chooni, kijana akataka kutoka nduki, mama akamdaka na kumrusha kitandani huku huku akimpa ishara ya kutokupiga kelele, kammkwangua sruali na ile kitu ya Ludoviki, kijana naye akapa hamu, wakacheza. Walipomaliza mama akampa yule kijana miloni moja na kumwambia asante sana kwa kazi nzuri
Asubuhi ofisini kijana anaona aibu hata kumwangalia lakini mama hajari hata kidogo, siku tatu baada ya ile kapewa laki tena na maelekezo ya kwenda kule hotelini, kijana katii amri ya bosi na kwenda hotelini kutoa dozi
SASA yamekua mazoea lakini si mapenzi maana anapewa aamri. sasa anahisi bosi mkubwa (mme) kajua sasa anataka kuacha kazi maana mkubwa anamuogopa sana. sasa aniomba ushauri nami sina, mwenye uzoefu katika haya anisaidie nimuokoe maana kuacha kazi na kuja kupata nyingine kasheshe

15 comments:

Anonymous said...

Hii kali. Kijana amewekwa wakati mgumu hasa. Ni rahisi sisi tulioko nje kusema afanye hili au lile ila ni tofauti na mazingira aliyonayo yeye.

Kuna uwezekano wa dogo kuwa naye anafurahia! Unakumbuka theory yangu ya kuwa mwanaume anahitaji nguvu za kimwili na kiakili? Asingekuwa anafurahia asingeenda dede....

Anonymous said...

Huyu mama anawakilisha wanawake wengi ambao ni majeruhi ktk ndoa. Kwa mfano kuna madai kuwa wanawake sita kati ya kumi hawafiki kileleni wakati wa tendo la ndoa! Sasa huyu sio tu hafiki bali hapati na kuolewa maana yake tendo lenyewe! Kibaya halipati! Ndio maana mama kaenda kuhemea kwa kijana. Hapa kosa ni la mwanaume

Anonymous said...

Huyu dogo inabidi aache kazi fasta,ikiwezekana achomoke ghafla bila hata kuaga

Kwani alikuomba wewe ushauri?isije ikawa sitaki nataka!

Anonymous said...

Hapo sasa ndio pagumu, raha mwisho wake karaha. Sasa kijana lazima atafute kazi fasta atoke hapo salama maana itafika mahali kijana akimkatalia huyo mama atamchomea utambi kwa mme kuwa kijana anamtaka kimapenzi na kazi itaharibikia hapo, ama atadai anataka kumbaka. Hizi kesi zimekua nyingi mwisho wake sio mzuri. Sugar mamy ishakuwa style ya maisha ya wazee .

J. K. said...

Tatizo, kijana ana mapenzi na mama maana kama nilivyoeleza ni kama amri, unapewa hela unaambiwa taafuta usafiri tukutane sehemu basi, hakuna mjadala wa leo labda nataka kwenda sehemu fulani wala nini. Tatizo ni kazi tu hapo, umepi kwata na mfuko wa kaki miaka miwili, mungu bariki umepata kazi, alafu unakumbana na hii!

Anonymous said...

Huyu kaka mdogo, the first thing aende akapimwe, asije akawa kabeba Mkubwa (HIV). Halafu kisha achomoke ghafla tena kabisa, bila kuaga. He should leave that job and move to another company.

Askofu Dhakri Kikobe said...

Ninahisi kama vile huyu mama anayesemwa hapa ndiye huyu Da Chemi. Chemi achana na ndogo ndogo, tafuta mkubwa mwenzio.
Onea bujii, gombe ogopa enhee?

Chemi Che-Mponda said...

Wewe unayejiita Askofu Kikobe, nina kaa Boston, USA siko Bongo. Sina haja na dogo dogo wakati saizi yangu wako tele!

Theo said...

Hii kesi ngumu kivitendo. Kinadharia rahisi.
Huyo mama ameolewa ndoa gani? Inaruhusu talaka ama ni hizi till do us apart? Maana hapo kama talaka hairuhusiki huyu kijana yuko hatarini kutolewa macho na kucha bila ganzi.
Yambidi aamue sasa kuwa mpango wake ni kuendelea na mama ama ni kuoa kijana mwenzie! Kama anahitaji maisha mengine na kijana mwenzie basi hapo ni kutafuta kazi mapema hii ili atoke hapo kwa huyo mama akiwa salama. La sivyo huyo mume kama kweli ampenda mkewe???? Hala hala mti na macho.

Anonymous said...

Mhh mie bado sijashawishika kijana hafurahii huo mchezo aliouingia. Kwanza kabisa after every service anayotoa, mama anamkatia kamilioni shilingi (nani asiyetaka pesa ya haraka haraka hivyo bila kodi?), Pili katika mchezo wote na yeye anafikishwa kileleni. Hofu ya huyu kijana ni mume wa hyu mama akilijua hili itakuwaje. Ushauri wangu kwa kijana ni kuacha kazi haraka, maana mama amenogewa na haonekani kuwa na hofu tena ya mmewe kugundua biashara inayoendelea kati yake na kijana. Lakini pale hyu baba atakapong'amua siri iliyopo kijana ndiyo utakuwa wa kwanza kushuhulikiwa then atafuata mke. Kwa mantiki hyo acha kazi na ufute mawasiliano na huyu mama completely kwa uhai wako. Kumbuka "MKE WA MTU SUMU", utapoteza maisha yako ama kupata kilema cha kudumu kwa kuendekeza ngono kwa malipo ya milioni

Anonymous said...

Quote: "Wewe unayejiita Askofu Kikobe, nina kaa Boston, USA siko Bongo. Sina haja na dogo dogo wakati saizi yangu wako tele!"
SAFI SANA DA CHEMI KWA KUWA MUWAZI

Anonymous said...

Huyo mama inaelekea ni mtu influential kwa hiyo amtafutie dogo kazi sehemu nyingine ili aweze kumtafuna vizuri bila kuhofia kufukuzwa kazi na mumewe.

Anonymous said...

Kijana kanogewa huyo, mwongo anatamani uhondo usiiishe. Anaweza kujenga nyumba kabisa na hizo hela.

Anonymous said...

Mazito. Lakini huyo kijana sijui kama kweli anataka kuacha uhondo.

Anonymous said...

KIJANA AMUOMBE PESA HUYO MAMA, THEN AKAANZISHE BIASHARA YAKE MKOA MWINGINE, ASIWE MTUMWA WA MAPENZI, THEN ATAFUTE MCHUMBA WAKE AOE, NAMTAKIA UELEWA WEMA WA USHAURI