Saturday, June 07, 2014

Kweli Kanali Mwanakatwe Amefariki!

Na Happiness Katabazi
 
SIKU yangu ya Leo Juni 7 Mwaka 2014, Imeingiwa na dosari ya kuondokewa na Furaha niliyokuwa nayo tangu asubuhi baada ya kusoma ukusara wa Mtandao wa kijamii, wa Mwandishi  wa Habari za Michezo Mwani Nyangasi,saa 9:30 Alasiri, na kuona Habari Isemayo Aliyekuwa Kiongozi wa Michezo nchini, Kanali Mstaafu, Ally Mwanakatwe, amefariki Dunia.

Habari hiyo imenisikitisha na kuniaribia jioni ya Leo.Ili kujiridhisha  kuwa ni kweli Mzee wangu Mwanakatwe,kafariki nilichukua simu yangu na nikaipiga simu ya Mwanakatwe itapokelewa mtu  ambaye Hana sauti ya Mwanakatwe nikajitambulisha.

Nikamuuliza taarifa hizi za Mzee wangu Mwanakatwe Kuwa eti  amefariki, MTu Huyo ambaye alijitambulisha Kuwa ni shemeji wa Marehemu aitwaye Denis Mtegeti, Alisema ni kweli amefariki, Niliumia sana na kushusha pumzi na Kisha kuendelea kuongea na Denis.

Akasema Mwanakatwe alikuwa Ana historia ya Ugonjwa wa Shinikizo la Damu ila hadi Jana jioni alikuwa naye alikuwa ni mzima wa Afya na walikuwa wote Katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo wakimuuga za  mmoja wa ndugu Yao.

Lakini Leo Mwanakatwe wakati akiingia bafuni kwake kuoga,nyumbani wake Mbezi Beach Dar es Salaam,  alishikwa na Hali isiyokuwa ya kawaida, akiwa bafuni akawa makelele ya kuomba msaada huku akishika ukuta wa bafuni wakapata  msaada ambapo walimtoa bafuni na kumkimbiza Katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi  na kwamba alifia njiani Kabla akatikishwa Katika Hospitali hiyo na kwamba mwili huo umeishahifadhiwa Katika Hospitali hiyo na upo nyumbani KWA Marehemu Mbezi Beach, unaweza teremka Kituo Cha Makonde au Jogoo na Taratibu za Mazishi zinaendelea.

Binafsi nilimfahamu Mwanakatwe kupitia Kazi yangu ya uandishi wa Habari na pia Mwanakatwe alikuwa alifanya kazi na mama yangu Mzazi na baba yangu Mzazi pale Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi(JWTZ), ' NGOME', Upanga. Dar es Salaam.

Mara ya Mwisho kukutana na Mwanakatwe ni Mei Mwaka huu, Katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, Tulijadili mambo siasa za nchi hii, na tukakumbushiana Enzi zile wakati alipokuwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Jeshi, ilipo Posta Mpya Dar es Salaam.

Mwanakatwe wakati ni Mkurugenzi wa Makumbusho ya Jeshi,nilikuwa na kwenda kumtembelea Mara kwa Mara pale na alikuwa a kielelezo na kunifundisha mambo ya jeshi letu lilivyo.

Mwanakatwe na Marehemu Dittopile Mzuzuri wote Kwa nyakatip tofauti walikuwa wakiniasa sana, Kuwa Katika uandishi wangu ni sipende kuandika Habari za uzushi za kukichafua JWZT Kwani JWTZ siyo Chombo Cha kuchezewachezewa ovyo ovyo na kwamba Jeshi ni Chombo nyeti na kwamba raia tusione tunalala na tunaamka Kwa Amani tukae tukijua kuna watoto watu yaani Wanajeshi Wanajeshi macho kujilinda nchi hii isivamiwe na maadui.

 Siwezi Kusema yote niliyokuwa nikielezwa na kafundishwa na Mzee wangu Mwanakatwe hapa, ila aliyokuwa amenifundisha yalinisaidia sana Katika uandishi wangu na kufahamu  Vyema vyombo Vya Ulinzi na Usalama vinafanyaje Kazi na vyombo Vya Habari hatupaswi kuvishutumu bila Kuwa na Sababu za Msingi za kuvishutumu.

Mwanakatwe nitakukumbuka sana niliyokuwa nakuja pale NGoME na Makumbusho ya JWTZ wakati mwingine nilikuwa nakuja na mwandishi wa Gazeti la Habari Leo , Halima Mlacha ambaye ni mtoto wa Kanali Mnyani, Wanajeshi wadogo walikuwa wakitupokea vizuri na kutuia sisi ni " watoto wa Wanajeshi", hatuna madhara.

Nitamkumbuka Mwanakatwe Kwa utanishati wake, jamani Mwanakatwe alikuwa ni mtanashati hasa, ukiingiia ofisini kwake Ana Mti maalum, uliotundikwa uniform zake ,zimepigwa pasi ,zimenyooka, kiatu kinameremeta Kama Kiatu Cha Jeshi alichokuwa anavaa Mnadhimu wa JWTZ Mstaafu, Abdullahman Shimbo.Kwakweli ni watanashati Wanajeshi hawa licha simaanishi Kuwa Wanajeshi wengine siyo watanashati.

Mwanakatwe Ni miongoni mwa Wanajeshi ambao unajeshi ulikuwa Kwenye Damu yake, na alikuwa Mwanajeshi kweli hata unavyomtazama na kumsikiliza mazungumzo yake.

Hakina kifo Chako ni pigo KWA JWTZ, CCM, wapenzi wa Soka na familia yake Kwa ujumla.

Tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi.
 
The Late Colonel Ally Mwanakatwe
 
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi

Juni 7 Mwaka 2014.

No comments: