![]()  | 
| Flora Mbasha na Mume Wakewakiwa na furaha kabla ya Skendeli | 
Kutoka VIJIMAMBO BLOG:
Mpasuko  wa  ndoa  ya  wasanii  wa  nyimbo  za  Injili, Emmanuel  Mbasha
  na  mkewe  Florah  umewagawa  wachungaji  wa  makanisa  mbalimbali  
nchini  baada  ya  kibao  kumgeukia  Flora  kwamba  ndiye  anadaiwa  
kusuka  mpango  wa  kumwangamiza  mumewe  ili  afungwe  kwa  kosa  la  
ubakaji…..
Wakizungumza  na  wanahabari  wetu  kwa  nyakati  tofauti,  wachungaji  
hao  walisema  endapo  itabainika  ni  kweli  Flora  ameshiriki  
kumsaliti  mumewe  kwa  kutembea  na  mmoja  wa  wachungaji  maarufu    
nchini  hapatakuwa  na  haja  ya  kumwalika  kwenye  huduma  zao  kwani 
 hawawezi  kuhudumiwa  na  mwimbaji  mzinzi.
Mchungaji  Ambonile  Mwakipesye  na  Amani  Joseph  wa  makanisa  ya  
Tanzania  Assemblies  of  God ( TAG)   walisema  kuwa  kama  kulikuwa  
na  matatizo  kwenye  ndoa  yao  walipaswa  kuwaona  watumishi  wa  
Mungu  na  kusuluhisha  badala  ya  kutengenezeana  mitego  na  
kuingizana  majaribuni  kama  inavyodaiwa  kutokea  kwa  Mbasha….
Wakati  wachungaji  hao  wakisema  hivyo, mchungaji  Thomas  Methew  
yeye  alisema  kuwa  ukweli  wa  jambo  hilo  wanaujua  wanandoa  
wenyewe  kwani  mpaka  sasa  hakuna  anayelijua  tatizo  kubwa  mpaka  
wakafikia  hatua  ya  kutengana.
**********************
 Kutoka Jamii Forum
SIKU chache baada ya tuhuma za ubakaji na mzozo wa familia ya mwimba Injili mahiri nchini, Flora Mbasha na mumewe, Emanuel Mbasha, mambo mengine yameibuka.
Mwimba Injili mahiri nchini, Flora Mbasha
Yaliyoibuka safari hii ni taarifa kwamba, juzikati, Flora alivamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake, Tabata Kimanga jijiini Dar dakika chache baada ya yeye kuingia na gari akitokea mafichoni anakoishi kwa sasa.
Kwa mujibu wa chanzo, siku ya tukio ilikuwa saa 9.15 alasiri ambapo Flora aliingia nyumbani kwake na kufunguliwa geti kubwa kisha kuingiza gari ndani na geti kufungwa tena.
“Flora aliingia na gari akitokea hotelini anakoishi kwa sasa. Alikuwa ameshaingia na geti likafungwa. Ghafla, watu wakafika na kugonga geti hilo kwa nguvu huku wakisema watalibomoa geti kama wenyeji hao hawatafungua,” kilisema chanzo.

Mwimba Injili mahiri nchini, Flora Mbasha akiwa na mumewe, Emanuel Mbasha,
Chanzo kikazidi kudai kwamba, ilibidi Flora apige simu polisi ili wafike kumuokoa yeye na familia yake.
“Polisi wawili walifika haraka sana wakiwa na bunduki na kukuta wale watu wamekimbia maana walimsikia Flora akiongea na polisi kuomba msaada.
“Lakini polisi wenyewe ilibidi watumie nguvu kubwa kugonga geti na kujitambulisha ndipo akatokea Flora na kuchungulia nje kupitia dirisha dogo. Alipowaona polisi akafungua mlango,” kilisema chanzo hicho.
Akihojiwa na polisi hao, Flora alisema watu hao walikimbia na hakuwajua kwa sura wala hawakujitambulisha ni akina nani.
Alizungumza na gazeti hili baada ya tukio, Flora alisema: “Unajua kwa sasa nina hofu sana na nilihisi wale watu walikuwa wakinifuatilia kwa karibu kila sehemu, sasa naogopa kuendelea kuishi hapa, wanaweza kurudi na sijui lengo lao.”
Hata hivyo, baada ya askari hao kuondoka katika eneo hilo, Flora naye aliingia kwenye gari lake akiwa na mdogo wake na kuondoka.
Mume wa Flora, Mbasha naye yupo mafichoni baada ya kudaiwa kumbaka binti wa miaka 17 ndani ya nyumba yao huku utata ukitawala kuhusu ukweli wa tukio hilo ambalo limeigawa jamii.




No comments:
Post a Comment